Shock up za Crown Athlete

Shock up za Crown Athlete

Buti la mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
312
Reaction score
850
Habari za jion, naomba kupewa ufahamu juu ya hili,

Leo nilienda garage flani kwa ajili ya kubadilisha shockup gari ni crown athlete na ni shockup za rear wheel, sasa baada kumuelezea fundi na kuikagua gari akasema shockup zangu ni za umeme na pair zinauzwa laki 8.

Lakin sikuridhika na maelezo yake nikatafuta fundi mwengine naye akaikagua gari yeye akasema shockup zake pair ni laki 3 na kuhusu umeme kasema hapana hakuna umeme ila zile zinazo pachikwa kwa juu baada ya kufunga shockup ni sensor ambazo zinaelekeza uelekeo wa taa za gari kama ukikata kona na n.k.

Naomba kufahamishwa ukweli ni upi mana imenibidi swala la kubadili niache kwanza ili nipate kujiridhisha juu ya hili.
 
Inategemea na mambo kadhaa!

1. Status/ hadhi ya garage uliyokwenda kubadilisha.

2. Mji uliopo, hizo spare zinapatikana kwa urahisi?

Kuna gereji kubwa na za kisasa!! Kila ukiingia kucheki gari bili si chini ya laki tano!!

Ingia zako Gerezani pale, mafundi wazuri na bei chee!!
 
Huwa nawaambia mnapenda Toyota kwasababu ya fake spares ona bei ya genuine parts
Screenshot_20210328-214824.png
Screenshot_20210328-214728.png
 
Habari za jion, naomba kupewa ufahamu juu ya hili..
Leo nilienda garage flani kwa ajili ya kubadilisha shockup gari ni crown athlete na ni shockup za rear wheel, sasa baada kumuelezea fundi na kuikagua gari akasema shockup zangu ni za umeme na pair zinauzwa laki 8.

huyo aliyekuambia kwamba ni shock up ya umeme wala hajakudanganya.

Tena ukipata genuine kwa pair inaweza kuwa zaidi ya 1m.
 
huyo aliyekuambia kwamba ni shock up ya umeme wala hajakudanganya.

Tena ukipata genuine kwa pair inaweza kuwa zaidi ya 1m.
Kumbe jamaa alikuwa sahihi. Mkuu naomba elimu japo kidogo, mechanism yake ipoje mana toka nimeagiza hyo gari hii ndio mara yngu ya kwanza kubadili shockup. So sijui chochote kuhusu shockup za umeme
 
Kabla haujabadilisha Shock up jaribu kwenda gereji nzuri na fundi aangalie kugonga kwa gari kuna sababishwa na nini.

Gari yangu ilikuwa inagonga pia. Na kuna fluids zilikuwa zinatoka. Nilifikiri ni shock up, nilivyoenda kwa fundi wakacheki kumbe zilikuwa ni bushes tu.

Fluids zilisababishwa na kuchoka kwa grisi zilizokuwa kwenye rubber boots zilizopasuka. Nikazibadili.

Pia nilisikia kama shock up zimekufa basi gari litakuwa linakita / kunesa vibaya huo upande wa shockup mbovu hasa ukipita rough road, ila sio kugonga.
 
Kumbe jamaa alikuwa sahihi. Mkuu naomba elimu japo kidogo, mechanism yake ipoje mana toka nimeagiza hyo gari hii ndio mara yngu ya kwanza kubadili shockup. So sijui chochote kuhusu shockup za umeme

Boss usiumize kichwa. Toyota catalogy yao ipo online ingiza chassis number gari yako itakuja na utaenda kuchagua spare unayotaka na namba yake, hakuna haja ya kuagua kwa waganga.

ukishapata namba yake, tafuta madukani ukiwa na number ya part unayotaka
 
Kumbe jamaa alikuwa sahihi. Mkuu naomba elimu japo kidogo, mechanism yake ipoje mana toka nimeagiza hyo gari hii ndio mara yngu ya kwanza kubadili shockup. So sijui chochote kuhusu shockup za umeme
Zinatumika kwenye magari ambayo yanakuwa na adaptive suspension system.

Kwa kifupi hiyo shock up inakuwa na mfumo ambao unacontrol flow ya oil kulingana na mazingira ya barabara ambayo unatembea.

Unaweza kuwa unatembea barabara ambayo iko rough lakini ndani unafeel kawaida tu.

Kwa kifupi inakupa uwezo wa kuchagua namna ambavyo unataka suspension yako iwe kulingana na barabara unayotembea.

Nimeona hii kitu kwenye toyota alphard pia.
 
Back
Top Bottom