Shopppers Masaki hawana utu kwa wateja wao

Shopppers Masaki hawana utu kwa wateja wao

KINSasante

Member
Joined
Jul 1, 2024
Posts
6
Reaction score
28
Wakuu,

Nimekusanya mahitaji yangu na kwend sehemu ya malipo na kufanya malipo kwa njia ya TIGOPESA MASTERCARDS.

Nikapokea msg ya kukatwa kwa malipo niliyofanya na nikawa najiandaa kuondoka na mzigo wangu nikapigwa stop,kwamba hawajapata malipo.

Nikaenda sehemu ya muhindi anayehusika nikamuonyesha kuwa nimelipia na nimeshakata lakini hao hawajapa msg,nikaambiwa nisubiri mpaka nipate msg.

Nimekaa kama nusu saa pale nimepiga simu TIGO wakaniambia ni kweli umelipa na hela imeshaenda kwao,lakini hawajapata msg kwasasabu ya network yao inashida hivyo chukua namba hizi waambie kuwa watrack kuona kuwa umeshafanya malipo.

Nikampa muhindi yule lakini akawa mkali na kusema hapana,rudisha mzigo bado sijapata msg,nikawaambia sasa naachaje mzigo wakati mmeshakata hela yangu.

Tumerumbana kwa kama 45mins, na kupiga simu kama mara 5 kwq TIGO kuongea nao lakini wapi wakakataa katakana kuelewa na kuambiwa niache mzigo mpaka wao wapate msg wakati mimi pia nimeshakatwa.

Nikaondoka na kuwaachia mahitaji yangu huku nikiwaza!Hivi ndio hela za kampeni zinatafutwa, kweli maskini unaweza kudhurumiwa haki yako hivihivi na wala usipate msaada wowote.

Nasubiri masaa 72 waliyosema kama hela itarudi kwangu au Kwasasabu imeshakatwa basi ndio imekula kwangu.
 
Tigo Leo walikuwa jau sana ..

Usiwalaumu sana hao jamaa maana nao wanalinda bidhaa zao zisiondoke bila kuona Hela maana analinda kibarua chake mkuu..

Bado tunasafari ndefu sana km taifaaa
 
Wakuu,

Nimekusanya mahitaji yangu na kwend sehemu ya malipo na kufanya malipo kwa njia ya TIGOPESA MASTERCARDS.

Nikapokea msg ya kukatwa kwa malipo niliyofanya na nikawa najiandaa kuondoka na mzigo wangu nikapigwa stop,kwamba hawajapata malipo...
Hivi unatumiaje mtandao wenye tusi??? Kingine wewe siyo mstaarabu yaani una akili za kimaskini. Cha kwanza ulipaswa uombe radhi. Cha pili ungelipa tena na kuwaambia in case transaction ya kwanza ikisoma mtanirudishia hela even baada ya siku kazaa. Cha tatu ungewaachia contact zako with some ID copy wakutafute in case hela haijaingia. Ila wewe haukufanya hivyo vyote zaidi ya kuwa na lugha ya utapeli.

Mi kuna siku nilikuwa nanunua samaki 10kg sangara og toka musoma pale bamaga, basi muuzaji akanipa mzigo bahati mbaya sikuwa na enough cash so nikamwambia twende kwenye gari nichukue simu nilipe, aisee alistuka sana. Sasa kutokana na status yangu nikamshangaa kwanini anaona ajabu, basi kwa wasiwasi ikabidi abebe mzigo tukatoka kwenda kwenye gari nikamuuliza tatizo.

Akasema mapolisi wengi huwa wanafika wanachukua samaki then wanamwambia waende kwenye gari wampe hela basi wakiingia kwenye gari wanawasha na kuondoka, hakika nilijisikia vibaya sana kwa sababu tabia ya watu wachache mnaonekana wote matapeli.
 
Back
Top Bottom