Putting it mildly....
- Is it selfish for a mother to prioritize financial security over romantic love? or is it heroic and self sacrifice for the benefit of her kids
"Materialist or Martyr? A Mother's Sacrifice."
Je asifiwe kwa kujinyima furaha ya roho yake, hata kwenda kwa mtu asiyempenda au kupendezwa nae kama it means security ya watoto hata watakaokuja, au avumilie na kufurahia furaha ya moyo huku akijua kina Junior watateseka na Ulimwengu wa dhiki ? i.e
Is Choosing Family Security Over Love: A Noble Sacrifice?;
The Mother's Choice: Security for Her Children vs. Her Own Happiness. Je sisi kama watazamaji tuna haki ya ku-judge bila kuvaa viatu vyake ?
Mkuu unajua jamii zetu za kiafrika kwa sasa zipo katika kipindi cha mabadiliko. Tupo katika kipindi ambacho wanaume na wanawake tuna mgongano katika namna ya ku-implement hii nadharia ya usawa wa kijinsia.
Wakati wanawake wameenda kwenye ule mkutano wao beijin na ajenda yao ya haki sawa, kuna kitu hawakukijua/hawakukielewa/hawakukifikiria. Kitu chenyewe ni kwamba haki sawa wanayoitaka itakuja na wajibu sawa pamoja na kupoteza privilege zote walizokua wanazipata kutoka kwa mwanaume.
Matokeo ya wanawake kushindwa kukiona hicho kipengere ndio inasababisha hizi chaos tunaziona kwenye dating pool na ndoa leo hii.
Wanaume wameshtuka na kujiuliza kama mwanamke nae anapewa access zote kama sisi, kuanzia elimu, ajira, kumiliki mali, uongozi n.k kwanini bado tuwajibike kubeba jukumu la kuwahudumia na kuwaandalia mustakabali wa maisha yao?
Wanawake nao wanataka usawa wa kijinsia lakini zile privilege za provision na protection kutoka kwa mwanaume hawataki kuziachia. Elimu, ajira, uongozi haki sawa. Haya mama umepewa access zote kama mimi bill hizi hapa twende na kanuni ile ile ya 50/50 hapo ndipo wanawake hawapataki.
Unapewa elimu ili upate maarifa ya kutafsiri mazingira na kuyaishi. Unapewa ajira ili uondolewe kwenye kundi la watu tegemezi. Sasa kuna maana gani ya mwanamke kupewa ajira na elimu kama hatma ya kupewa hizo haki ataishia kuwa liability kwa mwanaume.
Katika andiko lako umemchora mwanamke wa zamani ambaye hana access ya kupata elimu au ajira. Ofcourse huyu lazima mwanaume awe nguzo ya mustakabali wake. Lakini katika zama za leo za usawa wa kijinsia mwanaume na mwanamke wanatakiwa kushirikiana, sio mwanamke kuwa opportunistic.
Kwahiyo hili swali lako lijibiwe kwa ukamilifu, tunatakiwa turudi nyuma na kuangalia ideology gani tuibebe kujenga ustawi wa jamii yetu. Twende na mfumo dume, usawa wa kijinsia au tuchukua advantage za mfumo dume na zile za usawa wa kijinsia halafu kuzisuke kuja na ideology yetu mpya.
Lakini hiki tunacholazimisha kukifanya kwamba mwanaume acheze role yake ya kubeba jumumu zima la mustakabali wa mke na familia. Wakati mwanamke yeye acheze role yake kama feminism inavyomfundisha, ndoa zitaendelea kuvunjika na single mothers wataendelea kushamili kwenye jamii yetu