Dukuduku juu ya maximo
Mambo vipi kaka michuzi,
Napenda kuonesha kero yangu ya wazi ili wanasoka wenzangu wanisaidie hili ni kuhusiana na Timu yetu ya Taifa na Uwezo wa kocha wetu marcio Maixmo.
Kwanza nasikitika sana sana kwa timu yetu kutolewa katika mashindano ya kombe la chalenji. Pia napenda nihoji uwezo wa Maximo katika kufundisha soka. Ni wazi kuwa Maximo amekuwa mstari wa mbee katika kufundisha timu zetu za taifa yaani Kilimanjaro star na Taifa stars na amepewa uhuru wa kutosha kama inavyotakiwa kwa kocha yeyote yule. Isitoshe Maximo amefanya kazi hii huku kukiwa na udhamini mnono kutoka Serengeti lager, Nmb benki na wadhamini wengine kibao ambao wamejitoa kwa hali na mali pamoja na kuungwa mkona na wadau wengi wa soka ikiwemo serikali. Lakini cha kusikitisha ni kwamba ni takribani mwaka mmoja sasa na ushee hivi Maximo hajapata kikosi cha Taifa star cha kudumu. Amekua akitapatapa na nadhani kuwa uwezo wake umefikia mwisho na amekua akibahatisha katika uteuzi wa timu ndio maana kila kukicha hasiti kuoa sababu za malengo yake ya miaka kumi ijayo ndo tutarajie mafanikio ya soka.
Kwa hili nampinga Maximo kwa nguvu zote, kwani matarajio hayo ni malengo ya kuchukua au hata kushiriki kombe la dunia lakini kwa saizi ya makombe kama chalenji kwa muda aliokaa na kufanya kazi kama kocha mkuu Maximo alitakiwa kuhakikisha kuwa Kombe la chalenji linabaki nchini, kwani hili ni saizi yetu tangu hapo awali kama tulivyo litwaa miaka ya nyuma.
Kwa kumbukumbu zangu za haraka haraka nakumbua soka la TZ lilikwaga halina mdhamini wala wachezaji walikua hawana motisha wowote lakini tulifanikiwa kulitwaa kombe ili hali maandalizi pia yalikuwa ya zimamoto. Iweje leo Maximo atuambie anahitaji miaka kumi kujiandaa ili tutwae kombe la chalenji? wakati tukiwa na udhamini mnono na muamko nzuri wamashabiki?
inanipa wasiwasi na mkanganyiko wa mawaozo. maximo kila kukicha kikosi kipya na kambi ya brazili na ulaya ndio kimbilio lake then vijana wanakwenda kutalii brazili? kweli? wakijahuku anaachwa katika timu yataifa anachagua washamba wengine anawapeleka brazili kutalii kwa mtindo huu maximo hataweza kupata timu itakayo himili mikikimikiki ya ulimwenguu wa soka zaidi ya kuongeza idadi ya watalii kwa mwaka nchini kwake.
Ninaimani kuwa hata Mkwasa angepewa kikosi cha timu ya taifa wanaumena akapata udhamini na kuungwa mkono na wadau ange weza kuivusha taifastars hatua hiiwaliyofikia kombe la chalenji na angeipa timu mafanikiomakubwa na ingesheza mpira safi kuliko hata ulioonyeshwa na Timu yaTaifa wanawake Twiga Stars.
Ni wazi kuwa huwezi kulinganisha mpira uliochezwa na kilimanjaro starsna ule uliochezwa na Twiga stars wakina dada walionyesha soka safi nalakuvutia.
Asante kwa kunipa shavu humu globuni
Ndimi
Paul kabewa