Wameudharau wimbo wa taifa, watu hawapo serious kabisa mwengine wamekaa, mwengine kasimama kashika kidevu, wengine wanatabasam, wengine wametanua miguu, yaani kwa kifupi full dharau. Mimi nakumbuka nipo msingi Umoja jeshini yaani kitendo cha kusikia wimbo wa taifa unatakiwa usimame kiukakamavu hata kama umechelewa, jitie mjanja ukimbilie mstalini utachezea fimbo kwa walimu wote waliokuwa zamu na hata wanajeshi wakipita kuelekea kazini, wakisikia wimbo wa taifa lazima wasimame. Ila si shangai kadri siku zinavyoenda thamani ya huu wimbo unashuka, hasa ktk shule hizi za international mfano Atlas primary,iliyopo karibu na mabibo hostel hawaimbi kabisa ( nina mpwa wangu anasoma hajui wimbo wa taifa) , najua wanachukilia poa lkn ule wimbo unatakiwa uheshimiwe na Watanzania wote wa kila rika, kwani ni alama ya taifa letu.