Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Kuna dhana ya uzushi iliyojaa uwongo, kuwa viongozi wa CHADEMA huwa hawakai mbele wakati wa harakati za chama hicho kama vile maandamano.
Lakini ushahidi upo kuwa mara zote wakati wa maandamano ni viongozi wa CHADEMA ndiyo hukamatwa kwa kuwa huwa wanakuwepo kwenye maandamano tena mstari wa mbele.
Sasa hoja ya kusema hutanguliza wengine inatoka wapi tena? Au hoja ya kuhoji watoto wao wapo wapi siyo ya kijinga kweli?
Nani kasema kuwa ni lazima watoto, wenza ama ndugu wanatakiwa wafanye mambo kwa mfanano Kila wakati?
Hivi nani amewahi kuuliza ndugu za wachezaji Mpira kama huwa wanakuja uwanjani wakati wa mechi? Simba ilipofungwa 5-1 na Yanga nani aliuliza ni kwa nini mke wa Aishi Manula hakumsaidia kudaka?
Kuanzia Sasa inatakiwa CHADEMA wakiandamana Mwenyekiti wa CCM, na viongozi wengine wa chama hicho ndiyo watoke kuwazuia CHADEMA wasiandamane?
Hivi wakati Lissu anakamatwa IGP alikuwepo? Kwa nini kwenye mambo ya CHADEMA huwa CCM wanataka viongozi wa CHADEMA wawepo?