Shuhuda za namna watu walivyopona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

mudushi

Senior Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
151
Reaction score
86

Ndugu zangu wanaJF poleni na Mihangaiko ya kila mara na haya na yale yanayoendelea humu kwetu. ni upepo utapita tu.

Mwaka jana nilipost humu jamvini thread kuomba msaada wa tiba ya nguvu za kiume. Kwa kweli ni tatizo lililonisumbua kwa muda mrefu. Sikuwa naweza hata kusimamisha kwa dakika. Kabla ya kuja jamvini nilikuwa nimetembea kwa waganga wengi mnoooo. Nilikula dawa zao za kutosha. Nilienda Mwanza, Arusha, Mbeya, Kenya, DSM, Dom na kwingine kwengi tu. Sikupata hata nafuu kidogo. Nilipokuja humu jamvini nilipata ushauri na hata waganga wengine walinialika nitumie dawa zao kwa kunihakikishia kuwa ni tiba sahihi kwa 100%. Sitawataja kwa sababu ya maadili na kwa kuwa wako kazini na kwa kuwa nimekujatoa ushuhuda. Ukweli ni kuwa nimenunua hizi dawa za hawa waganga nyingine kwa Tshs, USD, rand n.k na nilizitumia kwa uaminifu mkuwa kabisa. Tofauti na nilivofikiri kwa kweli ckupata nafuu hata kidogo.

Kuna jamaa mmoja alinitonya kuwa nenda hispital umwone Dr wa hiyo issue yako. Niliamua kwenda MNH ingawa kwa aibu kubwa mnooo. Wakati najieleza Dr alikatisha maelezo yangu akaniuliza km nna sukari, pumu, k/kikuu nk. Nikamwambia hapana, tatizo langu ni hili hapa. Akaniambia kapime hivi haafu ulete majibu, ckujua ninini. Nilienda kwa vipimo nikachukuliwa damu baada ya muda nikapewa majibu na nikauliza walipima nn. Mtaalamu wa vipimo akaniambia alipima hormones mwilini bac nikarudi kwa dr. Dr baada ya kupitia majibu akaniambia hormones za kiume (testosterone) zimeshuka. Nikamwambia sasa? Akajibu zipandishe. Akaniandikia dawa za miezi mitatu. Kwa kweli nilitumia dawa kuanzia mwezi August 2012 na kufikia september mambo yalianza kubadilika kabisa na mpaka sasa natoa ushuhuda mm ni mwingine kabisa. Sasa nazingatia mlo na mazoezi (gym).

Ushauri wangu kwa wengi wenye hii issue ni kuwa nendeni hospital mkajue ni nni hasa tatizo ndo muanze tiba. Najua Waganga wa humu JF hamtaipenda hii lakini tukubali ukweli, ili watu wasipoteze muda na pesa nyingi km mm nilivofanya.

Mudushi

SHUHUDA ZA WADAU WENGINE WALIOFANIKIWA KUPONA TATIZO HILI
 
Mkuu,

Hilo ni janga kubwa especially for men of 35 yrs and above ila wengi hawawezi kuconfess ukweli wanabaki wanajitutumua mara Konyagi mara mihogo mibichi basi tu ilimradi.

Kwa msaada wa wale wenye aibu ya kuku PM ungewaambia hizo testorene energizer ulizotumia zinaitwaje watu wanusuru ndoa.
 
Umetoa ushuhuda mzuri wa kupona kwako lakini umeacha maswali mengi hayana majibu, kama ni mhimbili, ni dokta gani, anapatikana kitengo gani jina lake nani, anapatikana mda gani, hadi apointment au kawaida.kwa kuwa hapa tunaelimishana usingetumia utaratibu wa pm.
 
I had the same problem 2 years ago! Testosterone level was low! Daktari anayetibu tatizo hili anaitwa endocrinologist! Anakuwa ni mtaalamu aliyesomea mfumo wa homoni, sababu za kushuka kwa hizi homoni ni nyingi Kama poor diet, ulevi na kadhalika.
 
Mkuu
hilo ni janga kubwa especially for men of 35 yrs and above ila wengi hawawezi kuconfess ukweli wanabaki wanajitutumua mara konyagi mara mihogo mibichi basi tu ilimradi...

Inkoskaz,

Mimi ushauri wangu ni kuwa watu waende hospital wazungumze na MaDr. Then maDr watawaeleza nini cha kufanya labda wakapime au hata ushauri. MaDr ndo watawaandikia dawa. Hapana Inkoskaz cwezi kukuambia utumie dawa gani, siuzi dawa, Dr atakuambia.

Hospital ni nyingi nenda hospital za rufaa km uko mkoani. Ila mimi nilienda Muhimbili.

Mudushi
 
I had the same problem 2 years ago! Testosterone level was low! Daktari anayetibu tatizo hili anaitwa endocrinologist! Anakuwa ni mtaalamu aliyesomea mfumo wa homoni, sababu za kushuka kwa hizi homoni ni nyingi Kama poor diet, ulevi na kadhalika.

Sokwe,

Vipi baada ya matibabu kuna chochote? Je na wewe ulisumbuka km mm? Kikombe cha Babu ulikunywa?

mudushi
 
Wewe mudushi; Hili tatizo lako ulifikisha hata kwa MziziMkavu;???? Na tiba yake haukupata kusikia?

Kama umepata tiba tumshukuru MUNGU!
Mkuu LiverpoolFC Atafikaje kwangu huyu mudushi wakati alikuwa na matatizo ya (hormones mwilini) yeye akawa anakwenda kwa waganga kujitibu nguvu za kiume?.@mudushi Wanaokuja kwangu wanakuwa

wamesha kwenda mpaka hospitali kuangalia na inakuwa huko Hospitali imeshindikana ndio

wanakuja kwangu mimi mtu akini P.M. Au kunitumia Barua ya Email jambo la kwangu huwa namrudisha

Hospitali aende kuangalia je Anayo matatizo mwilini mwake?akisha rudi hospitali na kumuangalia kuwa hana

matatizo ndio mimi huwa ninamtibu Matatizo ya Ukosefu wa nguvu za kiume.

Mambo yanayochangia upungufu wa nguvu za kiume.


Msongo wa mawazo:
Ni dhahiri kuwa akili na tendo la ngono vinategemeana sana. Inajitokeza mara nyingi sana kwa watu wenye matatizo katika biashara, kazini na sehemu nyingine hujikuta hawako katika hali ya kuwa na hamu ya tendo la ndoa mpaka pale watakapotulia. Hii inaweza kuwapata watu wa rika zote na tatizo hili linaweza kuisha haraka kutegemeana na shughuli zao zinavyorudi katika hali ya kawaida

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
. Mzunguko wa damu mwilini una maana sana kwani kama damu haizunguki vizuri itachangia uume kutosimama vizuri kwa sababu usimamaji hutegemea kiasi na kasi ya damu inayoingia kwenye mishipa ya sehemu hiyo. Dawa zinazotumika kutibu shinikizo la damu huchangia pia kupungua kwa nguvu za kiume.

Unywaji pombe kupita kiasi:
Pombe inaweza kuathiri mishipa ya damu na mishipa ya fahamu kwa wakati mmoja. Wakati mwingine mtu akilewa sana huathiri ubongo na kukata mawasiliano kisaikologia na hivyo kushindwa kuwa katika hali ya kuwa na hamu ya ngono na hivyo kutosimamisha.

Unene.
Unene huwa unaambatana na mafuta mengi mwilini. Mafuta hayo wakati mwengine huzidi kwenye kuta za ndani za mishipa ya damu na hivyo kupunguza ukubwa wa mrija kiasi kwamba damu inipita kidogo na kwa shida. Hii huchangia kupungua kwa nguvu za kiume kwa sababu kiasi cha damu kinachotakiwa kisimamisha uume kitakuwa kidogo sana. Wakati mwingi uume unaweza kusimama kidogo na kulala kabla shughuli haijakamilika.

Kutokufanya mazoezi:
Tusipofanya mazoiezi pia mzonguko wa damu kutokuwa mzuri na hivyo kutoparuhusu damu ya kutosha kusimamisha uume. Kwa watu wanaotembelea magari na shughuli za kukuaa maofisini mda mrefu na hasa kama hawafanyi mazoezi asubuhi au jioni wako kwenye hatari zaidi kuliko watu wanotembea kwa miguu mwendo mrefu na kufanya kazi ngumu za kuuchosha mwili.

Matatizo ya kisukari:
Kisukari ni ugonjwa unaoathiri mishipa ya fahamu na kufanya mishipa ya damu kutofanya kazi yake viuri ili kuruhusu damu kujaa kwenye uume. Hii himfanya mgonjwa wa kisukari kushindwa kusimamisha hata kama ana hamu ya kufaya tendo hilo.

Umri:
Inaelezwa kuwa kadri umri unavyopanda ndio uwezo wa nguvu za kiume utaendelea kupungua. Baadhi ya watu huanza kuona tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40 na kuendelea na hasa kama maisha yao hayakuwa na mazoezi ya mwili. Sababu nyingine ni kama utumiaji madawa ya kulevya, kuumia katika uti wa

mgogongo, uvutaji sigara nk. Sababu nyingi zinachangia kupungua kwa nguvu za kiume zinaepukika kwa hiyo tunashauriwa kuwasiliana na wataalamu ili kujifunza jinsi ya kujikinga au kutibu matatizo hayo.

MWENYE KUTAKA DAWA YA NGUVU ZA KIUME.

Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Maalim Saad Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Ukweli ubaki kuwa ukweli tu kuwa watu wanataka tiba na tiba ipo. Sasa sitaki niingilie BIASHARA yako wala kuizungumzia ila mimi nimeeleza maumivu, uzoefu na karaha nilizopitia. sitaki niwataje waganga wa humu jf waliojitamba kuwa wanaweza kila kitu na kunilisha mivumbi ya miti.

Fikiria hii karaha bac 1. mganga mmoja wa jf alinidirect shinyanga nikafika kumbe kwa sangoma. 2. mwingine akanipeleka mbeya kufika naambiwa nipigwe ramli kwanza. hao waganga wamo humu humu na kazi yao nikusubiria matatizo ya watu. jamani tuhurumiane.

Nawasilisha.

Mkuu LiverpoolFC Atafikaje kwangu huyu mudushi wakati alikuwa na matatizo ya (hormones mwilini) yeye akawa anakwenda kwa waganga kujitibu nguvu za kiume?.@mudushi Wanaokuja kwangu wanakuwa ....
 
LiverpoolFC,

Nakubali kabisa watu wana madawa wala sibishi. Mimi nimeeleza uzoefu wangu na nimeamua kuwashirikisha wadua. Nikiandika hapa kila kitu unaweza amua kupitisha mchango ili angalua kunipa pole kwa jinsi nilivosumbuka. Nnachojua kwa ufupi hakuna dawa sijala ndugu yangu. Nnampnago wa kufanya checkup nione athari za hizi pumba za miti nilizokula.

Kha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaa!!
Sasa mbona nimeongea na MziziMkavu na kasema ya kwmb haujawahi kumpa habari yako kama ulivyosema? mudushi; Watu wana madawa wewe!
 
WanaJF,

watu wengi wamekuwa wakiniPM na kuniuliza nilitumia dawa gani na ni dr gani alinitibu. Kwa ufupi ni kuwa twende hospital tujieleze kwa maDR haafu wenyewe ndo wataamua wafanye nini. waweza pewa ushauri, dawa na hata vipimo.

Mimi sina dawa yeyote ya kutibu hii issue zaidi ya kukushauri na kukuhimiza uende hospital. pia waweza enda hospital kubwa sanasana za rufaa. mm nilienda MNh. zaidi labda ntakupa contacts za personal dr wangu.

kila la heri ndugu zangu
 
Mkuu Inkoskaz watatumiaje hizo testorene energizer pasipo na ushauri wa Daktari?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mudushi Utakwendaje kupigia Ramli wakati wewe umekwenda kwa mganga ili akupe Dawa za Nguvu za kiume?Ilikuwa wewe kabla ya kwenda kwa mganga ungelikwenda hospitali ili Daktari akupime Mwili wako huenda una Ugonjwa wa Kisukari au Maradhi ya Moyo,au Mafuta Mengi Mwilini (High Cholesterol), Uvutaji Sigara, Matumizi ya Madawa ya Kulevya, Matatizo katika Uhusiano, Mawasiliano Duni na Mwenza wako, Matatizo ya Kisaikolojia, Msongo wa Mawazo, Wasiwasi (Anxiety),Unywaji

Pombe,Upungufu wa Homoni aina ya Testerone, Kuongezeka Uzito au uzito Uliopitiliza, Tabia ya Kujichua kwa Muda Mrefu Punyeto (Masturbation)
Na kadhalika hizo ndio sababu kuu za upungufu wa Nguvu za kiume ukiwa huna hayo matatizo basi waweza kwa mganga wa kienyeji akupe Dawa za nguvu za kiume Mkuu.@mudushi chanzo MziziMkavu Email yangu hii hapa fewgoodman@hotmail.com
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…