Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Kukiwa na bonanza au marathon tujulishane. Naona miamba imekata 90km kimasihara tu.
 
Nilisimama mazoezi kwa wiki moja kutokana na kuwa na dalili za kirusi kipya, nipo fit nimerudi kwa upya
Tuendeleze na tuyapende mazoezi na kuzingatia lishe
 
Duh umenipa hamasa sana

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Kesi ya
Nina urefu wa sentimita 167 uzito wangu ni 70 kg najiona mzito sana . Je nifanyaje nipungue nashindwa sana sana kufanya mazoezi deily.
Kesi yako ni rahisi sana, chagua mazoezi unayoyaweza kama kukimbia, kuruka kamba, kutembea no yafanye mara 3-5 na anza kwa dakika 30 utaongeza kadri utakavyomudu

Punguza chakuka cha wanga na uki place kwa kula matunda

Kwako jitahidi angalau upunguze kg 3 , wenzio wanapambana kupungua kg 40! Wewe ni almost 3kg tu
 
Siri kubwa ya kupunguza uzito ni kuangalia mpangilio wako wa unavyoishi nikimaanisha kabla ya yote chakula na kukaa kutwa kwenye''sofa'' huchochea sana kuongezeka uzito vyakula vya wanga na sukari husaidia sana kuongeza uzito hata ukifanya mazoezi vipi na ukawa unatumia vitu hivyo kwa kiasi kubwa basi kupungua itakuwa ni shida,pia hata kama huli hivyo vyakula hakikisha unakula kiasi kidogo na si kifusi halafu fanya mazoezi hasa kama kutembea angalau km 1 kwa siku 4 kwa wiki au kukimbia.Mazoezi mengine kama vile kubeba vyuma vizito vyenye uzito mkubwa ,kupiga sana pushup au squat huweza kukusababishia mazara unapokuwa na umri mkubwa . Pia unaweza ukawa unakula kifungua kinywa na chakula cha mchana na usile chakula cha usiku,utakuta uzito unapungua ,tatizo la kula chakula kingi usiku ni kukosa kuyeyuka kwa kuwa mwili haufanyi kazi yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…