Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Kukiwa na bonanza au marathon tujulishane. Naona miamba imekata 90km kimasihara tu.
Adjustments.JPG
Adjustments.JPG
 
Nilisimama mazoezi kwa wiki moja kutokana na kuwa na dalili za kirusi kipya, nipo fit nimerudi kwa upya
Tuendeleze na tuyapende mazoezi na kuzingatia lishe
 
Nilikuwa na kilo 98 bonge la kitambi,Bonge la paja,bonge la mkono,...watu mtaani wakaanza kuniita bonge...hamna kitu kiliniuma kama kuitwa bonge...nkaanza mazoez nkashindwa mwlili mzito viungo vinauma...jaribu diet nikashindwa njaa inauma mpaka kizunguzungu nkakata tamaa....mda ukapita ...watu wanazid kuniita bonge...

Nikaenda gym nkaambiwe nilipie elfu 80 kwa mwezi...nkaenda benk kuchukua pesa...huwez hamini niliiangalia ile pesa mkononi nkasema yaani naenda kutoa elfu 80 gym wakati viwanja viko bure tuu!?[emoji848]...nkazama mtumbani nkanunu raba rut ikaanza...Kimbia sana mwez mzima nkapungua kilo 3...nkasema ahaaa kumbe inawezekana nkapata na elimu ya lishe....ratiba ikawa hivi

....Nikapunguza vyakula vya wanga yaani ugari nilikuwa nakula saizi ya ngumi yangu...mboga za majani kwa wingi sna yaana
.....Nilikuwa nakula pale nnapojisikia njaaa(watu weng tumezoea kula mara tatu kwa siku lakini chakula tunachokula ni kingi so kinakutana tumbon) Ki afya unaruhusiwa kula hata mara sita kwa siku lakini kidogo kidogo(unapojisikia njaa$

.....Nikaacha kabisa soda na nyama nyekundu(baadae sana nkaanza kutumia maana ukiwa kwenye mazoez ya kupunguza mwil kuna kitu kinaitwa 'cheating day'

......Ratiba yangu ya mazoez ilikuwa kila sku asubuhi saa kumi na moja nkiamka kufanya ibada naamkia kiwanjani ...kukimbia,kuruka kamba,na mazoez ya viungo(Asikuambie mtu zoez la kukimbia ndo zoez bora la kupunguza uzito
....Jioni nkirud kazini naingia tena kiwanjani

....Nkawa fiti kuna kipind nkawa na uwezo wa kukimbia mpaka round 30 za kiwanja....nkisem nkimbie road work nnawez kimbia mpaka km 20,15
...Nikapungua kilo pamoja na uzito nkawa na mwili mdogo na wa kawaida....nikawa na enjoy maisha

...Kutokana na hari ya kuwa na pumzi ya kutosha nakanza kucheza football
Sasa mpira wetu wa uswahilini upati mda wa kujiandaa unatoka nyumbani kiwanjani....sipati mda mwing wa kufanya mazoez sana(nacheza beki ya kati)...ka mwili kamerud kidooogo sema ka kawaida sio mnene[emoji2]
...MUHIMU...ukiitaka kupunguza uzito

...Punguza ulaji wa sukar na wanga
....kula sana mboga za majani kunywa sna maji
.....fanya mazoez
Ukipungua kwa kufanya mazoez na kufuata lishe unakuwa phyisical...ukifanya tu diet unapingua kama mgonjwa mgonjwa hivi...haui physical yaani[emoji23]...so fanya yote

Ukishachanganya mazoez chagua siku ambayo utaaita 'cheatind day' hii siku usifanye diet wala usifanye mazoez yaan kula tu junk...masoda kula chips kula,nyama hata kilo we kula(japo unywe maji meng).....huo ndo ushuhuda wangu wakuu...na kipind unajizuia kula vitu vya sukari utakuta mwili unatamani kula vitu vya sukari...tumia Tende zitakupunguzia tamaa ya kula sukari
....vitu vingine namna ya kunywa maji...kunywa maji nusu saa kabla ya kula na nusu saa baada ya kula....nini faida yake?....

kunya maji kabla ya kula kutakufanya upunguze hamu ya kula...hivo hutokula chakula kingi....kinywa baada ya kula kutakusaidia digestion ifanyike kwa urahisi...tumezoea kunywa maji tukimaliza tu kula hii nimbaya maana inaifanya utumbo kuwa mtepemtepe hivo kupunguz digestion
....kula matunda kwanz alafu chakula na sio chakula alafu matunda

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh umenipa hamasa sana

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Kesi ya
Nina urefu wa sentimita 167 uzito wangu ni 70 kg najiona mzito sana . Je nifanyaje nipungue nashindwa sana sana kufanya mazoezi deily.
Kesi yako ni rahisi sana, chagua mazoezi unayoyaweza kama kukimbia, kuruka kamba, kutembea no yafanye mara 3-5 na anza kwa dakika 30 utaongeza kadri utakavyomudu

Punguza chakuka cha wanga na uki place kwa kula matunda

Kwako jitahidi angalau upunguze kg 3 , wenzio wanapambana kupungua kg 40! Wewe ni almost 3kg tu
 
Habarini waungwana katika jukwaa hili tukufu la utanashati na ulimbwende, miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mlolongo wa tiba lishe, madawa, na mbinu nyinginezo za kupunguza uzito wa mwili, jambo ambalo bado halijaleta ufanisi kinyume na matarajio.

Hivyo kwa uzi huu naomba tupate mbinu, njia, lishe kwa wote waliofanikiwa kupunguza uzito kwa kutegemea lishe na mazoezi.

Hii itaongeza hamasa kwa kila aliye na matarijio ya kudhibiti uzito.

Karibuni
Siri kubwa ya kupunguza uzito ni kuangalia mpangilio wako wa unavyoishi nikimaanisha kabla ya yote chakula na kukaa kutwa kwenye''sofa'' huchochea sana kuongezeka uzito vyakula vya wanga na sukari husaidia sana kuongeza uzito hata ukifanya mazoezi vipi na ukawa unatumia vitu hivyo kwa kiasi kubwa basi kupungua itakuwa ni shida,pia hata kama huli hivyo vyakula hakikisha unakula kiasi kidogo na si kifusi halafu fanya mazoezi hasa kama kutembea angalau km 1 kwa siku 4 kwa wiki au kukimbia.Mazoezi mengine kama vile kubeba vyuma vizito vyenye uzito mkubwa ,kupiga sana pushup au squat huweza kukusababishia mazara unapokuwa na umri mkubwa . Pia unaweza ukawa unakula kifungua kinywa na chakula cha mchana na usile chakula cha usiku,utakuta uzito unapungua ,tatizo la kula chakula kingi usiku ni kukosa kuyeyuka kwa kuwa mwili haufanyi kazi yoyote.
 
Back
Top Bottom