Shuhuda za waliofanikiwa kupunguza uzito kwa mazoezi na lishe

Lkn Mtaalamu mmoja wa mambo ya lishe aliwahi kuniambia kuwa Mazoezi bila kupunguza kula ni Kazi bure,ni bora hata anayefanya diet kuliko wa Mazoezi pekee,kumbe Mazoezi yaende pamoja na diet.
 
Ni mwanzoni mwa mwaka....muda muafaka wa kuanza upya maisha ya kupunguza uzito na vitambi....
 
73Kg now from 85kg,am enjoying my flat tummy...
 
December mwaka Jana nilikuwa na 87kg
nilitumia wiki 3 hadi ile ya 4 kufikisha 80kg
Kulingana na kimo cha urefu wangu napaswa kuwa na 76 hadi 77.6kg
hivyo nimebakisha 3 to 4kg.
Wakati naanza hata Ofisini walinambia wacha tuone!
Ila
Moja ya kitu nachomshukuru sana Mungu ni kunipa huo uwezo wa KUJIACHIA na KUJIPUNGUZA
coz hii sio mara ya kwanza wala ya Pili.
Nakumbuka
Nilijiachia hadi 100 na zaidi kg
Ila nikaziondoa
Leo nikimuona mtu anaesema kuwa hawezi kupungua
huwa namshangaa sana!!!!
Coz anaweza na huo uwezo anao ila labda tu hajaamua.
Lishe + zoezi (kutembea tu kila siku Asubuhi 30 mis
na Jioni 30 mins
almost saa nzima)
 
Kutoka 85 to 75 nilitumia kama mwaka,ila kutoka hapo 75 to 73 nimekwenda taratibu sana takribani miaka 4,huwa napanda na kushuka hivyo sizidishi 75...
Hongera sana aisee.

Jitahidi ule kidogo,kula chakula chochote kile ila usile saaaana utaenjoy life
 
Uliwezaje mkuu? Mbinu zipi unatumia?
 
Hongera sana umepungua kg 24 kwa miezi sita! Ushuhuda poa sana
 
Lkn Mtaalamu mmoja wa mambo ya lishe aliwahi kuniambia kuwa Mazoezi bila kupunguza kula ni Kazi bure,ni bora hata anayefanya diet kuliko wa Mazoezi pekee,kumbe Mazoezi yaende pamoja na diet.
Yaani mchawi chakula kaka mazoezi ni nyongeza tuu. Wee ukitaka kujua mchawi chakula ebu kaa wiki nzima bila kula na wala usifanye zoezi uone kama hujapungua.

Tatizo wengi wanafanya zoezi lakini hamna mabadiliko kwenye aina na wingi wa chakula wanachokula
 
Uliwezaje mkuu? Mbinu zipi unatumia?

Okay ni vizuri sana kuujua ABC kuhusu UNENE,

Hivyo kabla ya yote ni lazima utambue mambo ya msingi:

Ni vizuri kutambua uzito unaopaswa kuwa nao kulingana na urefu wako

Ila tambua pia kuwa:

Chakula unachokula kikilingana na uzito wa kazi unazofanya basi hapo HAUTAPUNGUA WALA KUONGEZEKA (nenepa).

Chakula unachokula kikiwa kingi
kuliko uzito wa kazi unazozifanya basi hapo UTANENEPA.

Chakula unachokula kikiwa kiasi kidogo kuliko uzito wa kazi unazozifanya basi hapo UTAPUNGUA kwa wengi tunaiita utakonda.

Tambua kuwa unene ulionao hayo ni mafuta (Fatty),
ambayo hayo mafuta pia hicho ni chakula unachokula ndiyo kinabadilishwa na kuwa mafuta mwilini.

Mfano unapokula wali, kuku, samaki, n.k
Mwili hauwezi kuhifadhi wali kama wali mwilini bali hicho chakula huwa baada ya mmeng’enyo hubadilishwa na kuwa katika mfumo wa mafuta.

Na hayo mafuta sasa ndiyo yanayohifadhiwa mwilini ambacho huwa ni chakula ulichokula.
Kinahifadhiwa kama ziada tu.
Ndiyo maana huwa tunasema ukimchukua mtu mnene na mtu mwembamba alafu uwafungie bila kuwapa chakula
ni dhahiri atakaeanza kuaga dunia basi ni yule mwembamba.

Kwanini?
Ni kwa sababu yule mnene tayari ana chakula kilichopo mwilini mwake ambacho ni cha ziada ila tu kimehifadhiwa mwilini katika mfumo wa mafuta.

Sasa baada ya kupata ABC hizo kuna vitu sasa ni lazima uvifanye ili upungue,
ili kupunguza ziada ya hayo mafuta ama chakula kilichohifadhiwa mwilini.

Mbaya zaidi ni mifumo yetu ya ulaji iliyo mibaya ndiyo maana mara nyingi tunajukuta na vitambi hahaha!
unene usiokuwa na tija pia.

Hivyo sasa ni lazima upangilie na ubadilishe pia ulaji wako.
 
Kabla ya mazoezi nilikuwa na kg98 kitambi kama ujauzito wa mapacha 10, nina urefu wa cm 169. Nina kula kutwa mara 3 nina fanya mazoezi siku 5 kwa wiki kwasasa nina kg 70.
Amini kuwa Kupunguza uzito si kujinyima kula.
Kula vizuri uwezavyo ukizingatia milo 3 protein,vitamins na wanga kisha fanya zoezi jepesi.
 
Mkuu kula uwezavyo ili upungue uzito unahitaji uwiano wa chakula maji na mazoezi.
 
Mkuu kula uwezavyo ili upungue uzito unahitaji uwiano wa chakula maji na mazoezi.
Huitaji mazoezi bwana wewe. Ondoa vyakula vya kukaaga masoda juice na kula wali/ugali sahani nzima imejaa....wee kula size ya ngumi yako uone kama hujanywea fasta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…