Uliwezaje mkuu? Mbinu zipi unatumia?
Okay ni vizuri sana kuujua ABC kuhusu UNENE,
Hivyo kabla ya yote ni lazima utambue mambo ya msingi:
Ni vizuri kutambua uzito unaopaswa kuwa nao kulingana na urefu wako
Ila tambua pia kuwa:
Chakula unachokula kikilingana na uzito wa kazi unazofanya basi hapo HAUTAPUNGUA WALA KUONGEZEKA (nenepa).
Chakula unachokula kikiwa kingi
kuliko uzito wa kazi unazozifanya basi hapo UTANENEPA.
Chakula unachokula kikiwa kiasi kidogo kuliko uzito wa kazi unazozifanya basi hapo UTAPUNGUA kwa wengi tunaiita utakonda.
Tambua kuwa unene ulionao hayo ni mafuta (Fatty),
ambayo hayo mafuta pia hicho ni chakula unachokula ndiyo kinabadilishwa na kuwa mafuta mwilini.
Mfano unapokula wali, kuku, samaki, n.k
Mwili hauwezi kuhifadhi wali kama wali mwilini bali hicho chakula huwa baada ya mmeng’enyo hubadilishwa na kuwa katika mfumo wa mafuta.
Na hayo mafuta sasa ndiyo yanayohifadhiwa mwilini ambacho huwa ni chakula ulichokula.
Kinahifadhiwa kama ziada tu.
Ndiyo maana huwa tunasema ukimchukua mtu mnene na mtu mwembamba alafu uwafungie bila kuwapa chakula
ni dhahiri atakaeanza kuaga dunia basi ni yule mwembamba.
Kwanini?
Ni kwa sababu yule mnene tayari ana chakula kilichopo mwilini mwake ambacho ni cha ziada ila tu kimehifadhiwa mwilini katika mfumo wa mafuta.
Sasa baada ya kupata ABC hizo kuna vitu sasa ni lazima uvifanye ili upungue,
ili kupunguza ziada ya hayo mafuta ama chakula kilichohifadhiwa mwilini.
Mbaya zaidi ni mifumo yetu ya ulaji iliyo mibaya ndiyo maana mara nyingi tunajukuta na vitambi hahaha!
unene usiokuwa na tija pia.
Hivyo sasa ni lazima upangilie na ubadilishe pia ulaji wako.