Elections 2015 Shuhudieni CCM walivyoshangilia tishio la kupotezwa kwa Watanzania wenzao wenye mawazo tofauti, halafu eti tunashangaa ndugu zetu wapinzani kupotea!

Elections 2015 Shuhudieni CCM walivyoshangilia tishio la kupotezwa kwa Watanzania wenzao wenye mawazo tofauti, halafu eti tunashangaa ndugu zetu wapinzani kupotea!

Roho mbaya saana!!
Fikiria ikafikia hata wale waliomsukumizia madaraka wanaogopa kumkosoa. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alimpigia kampeni Mwinyi lakini Mwinyi alipoanza kuboronga na kuigeuza Ikulu sebule ya wakwepa kodi hakunyamaza, alimkemea.

Hivyo hivyo Mwalimu pamoja na kuzunguka mikoa yote nchini akimnadi Mkapa (RIP) ambaye hakujulikana kabisa lakini siku Mkapa alipoanza kuuza hovyo mashirika yetu pamoja na benki yetu kwa bei ya chee, Mwalimu hakunyamaza, alimkemea.

Nina hakika Mwalimu kama angekuwa hai hangenyamaza wakati wa Kikwete na hangenyamaza wakati huu wa Magufuli. Lakini Mwinyi, Mkapa na Kikwete, kwa Magufuli walikuwa kimya kama waliomwagiwa maji baridi huku wananchi wakipotezwa.

Hakuna hata moja aliyekuwa na ujasiri wa kumkosoa hata pale alipoonekana kuwa tayari kuvunja hata Katiba aliyoapa kuiheshimu, kuitetea na kuilinda. Walinyamaza hata pale wapinzani walipozibwa midomo na waliokaidi kupigwa risasi au kupotezwa.

Hakika hii miaka mitano haitasahaulika katika historia ya taifa hili. Tanzania iliyoheshimika na kusifiwa duniani kama kisiwa cha amani hivi sasa inawekwa kundi moja na zile nchi za Kiafrika ambazo toka kujipatia uhuru hazijaweza kuwa na amani, inasikitisha.
 
Kinachoogofya zaidi ni huyu mtu kupewa miaka mingine mitano licha ya kwamba hapendwi kabisa. Waoga, wanafiki na walafi wameamua kuvitumia vyombo vya dola kumsukumizia miaka mingine mitano, je tutapona? Hilo ndilo swali ambalo kila Mtanzania itabidi ajiulize...

Lissu anashida Mkuu.
Weka kwenye kumbukumbu hii
 
Naam, hiyo ndiyo Tanzania na hao ndio viongozi wa chama tawala wanaotaka tuwape ridhaa ya kuendelea kututawala kwa miaka mingine mitano. Cha ajabu ni kwamba wapo Watanzania wenzetu ambao wako tayari kutoa ridhaa hiyo bila hata kuhoji..
Mkuu Mag3 naomba utuwekee video katika mfumo tunaoweza kudownload please not as a link. Niko na watu kibao ndugu zangu nikiwaeleza ukatili wa huyu bwana huwa hawanielewi
 
Hizi ni mbinu tu. Toa video yote ili tujuwe kasema nini.Wewe umetoa sentenso moja na hatujui qualifier za aliyoyasema zikoje. Hii wapelekee wajinga ndiyo watakuamini!
Lakini si unaweza kutoa hata wewe ndugu? Kama huna video unaweza kuandika hapa hizo qualifier za kuzungumza ukatili hadharani ukimtanguliza na Mungu. Please tuwekee hapa hizo qualifiers
 
Kajinyinge? Ushamba na ulimbukeni utawamaliza. Mitano mingine ni ishara tu ya laana kuongezeka na hata hiyo ikiisha anaweza akapata hata mingine kumi, si amekamata mpini? lakini iko siku atatoka tu. Idi Amin Dada wa Uganda alidai kuota ndoto iliyomwezesha kujua hata siku yake ya kufa hivyo hatishiki. Naye alikuwa na wafuasi wanaofanana na wewe. Siku yake ilifika na akaikimbia nchi yake. Alikuja kufia mafichoni mbali kabisa na nchi yake.
Wasikusumbue Hawa wote unaowaona humu wakipiga kelele mitano Tena Ni watoto wa dada zake yaani wapwa. Hawa Ni kina Dotto na nduguze wanajaribu kujimultiply kwa ID za kutosha JF
 
Hakika huyu Bwana ni muuaji, kwa maana halisi ya neno ya anayepoteza watu!
 
Vitisho mbele ya uhai wa Taifa letu..., kama mtu anayo chembe hata hafifu ya uzalendo ndani yake, ni wakati wa kusimamia uzalendo huo.

Hawa wote wanaopewa maelekezo, wakiyakataa, atawafukuza kazi wote?
Abadani, hawezi..!!

Kila kitu kiko very well planned..

Nakuhakikishia, watu watarajie mshangao wa karne..

Watu wawe tayari kuuona uwezo na utukufu wa Mungu..

Daudi ameshamwangusha Goliath..!!
Mkuu najua ni vigumu sana lakini ni wakati wa kila mtu kusema hapana. Nakuapia huyu kama kila mtu akikataa uovu na kuunganisha nguvu ataanguka vibaya sana sana. Anachukiwa kupita maelezo na tatizo lipo tu ni nani aanze... Miaka ya nyuma CCM ilikuwa na nguvu vijijini lakini mwaka huu vijijini ndiyo watu hawaitaki kabisa. Kuna jamaa zangu wengi walikuwa wana CCM wa kweli na washabiki waliokubuhu kila kipindi cha uchaguzi lakini safari hii hawataki kumsikia huyu rais kabisa. Polisi na hata jeshini watu wanafuata amri kwa shingo upande lakini likitokea tukio moja dogo tu linaweza ku-activate chain of reactions na Magufuli akaanguka vinaya sana.

Hakika ndivyo itakavyokuwa..

Imeandikwa, mtaziona ishara na dalili zote za "ule mwisho"..

Ishara ya kwanza kubwa, ni utawala wa CCM kukosa KIBALI cha UMMA na MUNGU mwenyewe..

Magufuli hana kibali kabisa. Magufuli na CCM yake wanapumulia artificial oxygen machine..

Wao wanajua, wananchi wanajua na Tanzania na dunia yote inajua...!
 
Naam, hiyo ndiyo Tanzania na hao ndio viongozi wa chama tawala wanaotaka tuwape ridhaa ya kuendelea kututawala kwa miaka mingine mitano. Cha ajabu ni kwamba wapo Watanzania wenzetu ambao wako tayari kutoa ridhaa hiyo bila hata kuhoji.

Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba tukifanya makosa tena, safari hii tutalia sana kwani kama alivyowahi kuonya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP), aliyeonja nyama ya mtu haachi.
Mchakato wa kampeni imenifundisha mambo mengi nimeweza kuwatambua watu wenye roho za chuki na unyama. Kwa kupenda kuona watu wengine wanapigwa na kunyanyaswa ni kipimo kizuri kujua huyu ni mtu wa namna gani.
 
Abadani, hawezi..!!

Kila kitu kiko very well planned..

Nakuhakikishia, watu watarajie mshangao wa karne..

Watu wawe tayari kuuona uwezo na utukufu wa Mungu..

Daudi ameshamwangusha Goliath..!!


Hakika ndivyo itakavyokuwa..

Imeandikwa, mtaziona ishara na dalili zote za "ule mwisho"..

Ishara ya kwanza kubwa, ni utawala wa CCM kukosa KIBALI cha UMMA na MUNGU mwenyewe..

Magufuli hana kibali kabisa. Magufuli na CCM yake wanapumulia artificial oxygen machine..

Wao wanajua, wananchi wanajua na Tanzania na dunia yote inajua...!
Sahihi kabisa
 
Abadani, hawezi..!!

Kila kitu kiko very well planned...
Ndugu yangu Kuna watu wengi bado wako gizani, leo nilienda posta nikahudumiwa na mama mmoja anayejiandaa kustaafu mwaka huu akiniuliza utampigia Nani kura? Nikamjibu yeyote aliye kwenye karatasi lakini sio Magufuli.

Alinishangaa akaniambia ndio zenu vijana kwani huoni maendeleo yote haya? Nikajua mama huyu naye amejazwa woga wa kupindukia zaidi ya MKE wangu ambaye akisikia tu umetaja jina Magufuli anakimbilia kufunga madirisha majirani wasisikie tukadhurika.. hofu hofu kila mahali
 
Sitashangaa kama baada ya tishio lake hili lililoonekana kuungwa mkono na uongozi wa juu wa CCM ndio kikosi cha wasiojulikana kikaundwa. RIP Ben Saanane, RIP Azory Gwanda, RIP Watanzania waliopotezwa katika hiyo miaka mitano.

Tarehe 28/10/2020 na bado siku mbili tu tuhakikishe tunakomesha kabisa ukatili huu tulioushuhudia. CCM na mgombea wake OUT!
Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu wa Mbinguni
 
Mkuu Mag3 naomba utuwekee video katika mfumo tunaoweza kudownload please not as a link. Niko na watu kibao ndugu zangu nikiwaeleza ukatili wa huyu bwana huwa hawanielewi
Unaweza kuisave tu kwa njia ya kawaida na kumrushia mtu yeyote yule kwa simu au kwa laptop, mbona hakuna shida? Huyu mtu hatufai Watanzania, period!
 
Wapinzani wanahitaji njia sizizokuwa za kawaida kukitoa chama dola madarakani. Kura ni kuhalalisha udhalimu wa CCM tu. Hivi watu kama wale waliomtoa Karume madarakani 1972 hawapo tena nchi hii?

Wapemba wana asili ya uarabu lakini mbona wanakosa ujasiri wa Waarabu? Wangekuwa Waarabu tangu 1995 wanaonewa, wangekuwa wamekwishajilipua na mtu. Hawa wa Pemba, vipi? Wataka eti wamtoe dhalimu kwa kura!
 
Ndugu yangu Kuna watu wengi bado wako gizani, leo nilienda posta nikahudumiwa na mama mmoja anayejiandaa kustaafu mwaka huu akiniuliza utampigia Nani kura? Nikamjibu yeyote aliye kwenye karatasi lakini sio Magufuli...
Wapo binadamu wakatili wengi tu waliowahi kutisha kuliko huyu lakini mwisho ulipofika hawakuwa na chao. Huyu hata ikitokea miujiza akapona hawezi kuwa tena na amani, atasononeka muda wote.

Amesikia, ameona na anajua sasa kwamba amezungukwa na watu wasiompenda, amezungukwa na watu ambao siku akianguka watasherehekea anguko lake na hawataweza tena kuficha furaha yao.

Sasa imebaki kwa vyombo vya dola, hao ndio mpaka sasa wanampa kiburi lakini hata wao wanaanza kujiuliza hadi lini wataendelea kuwaumiza ndugu zao? Kwa nini waendelee kuwaumiza Watanzania wenzao wasio na hatia?
 
Naam, hiyo ndiyo Tanzania na hao ndio viongozi wa chama tawala wanaotaka tuwape ridhaa ya kuendelea kututawala kwa miaka mingine mitano. Cha ajabu ni kwamba wapo Watanzania wenzetu ambao wako tayari kutoa ridhaa hiyo bila hata kuhoji.

Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba tukifanya makosa tena, safari hii tutalia sana kwani kama alivyowahi kuonya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP), aliyeonja nyama ya mtu haachi.
Big Salute Mkuu...
 
Magufuli anaelekea huko Tena kwa kiasi Sana
 

Attachments

  • IMG_20201015_054818.jpg
    IMG_20201015_054818.jpg
    100.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom