KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Safari hii itakuwa ya kushangaza sana jinsi waTanzania tusivyochukulia kwa uzito sahihi mambo mazito yanayohusu nchi yetu.
Mtu kutoka nyumbani asubuhi na mapema kwenda kupanga mstari kumchagua mtu kama huyu ambaye hafichi kabisa tabia zake!
Na sababu ya kumchagua. anajenga barabara; kana kwamba barabara zimeanza kujengwa na yeye, na atakapochukuliwa na muumba wake Tanzania hakutajengwa barabara tena!
Huyu alitakiwa waTanzania wamkatae kwa kura nyingi, kiasi kwamba hata angetumia nguvu kulazimisha ushindi ingeonekana dhahiri mbele za macho ya dunia. Kura atakazopewa zitakuwa nyingi hata kama hatashinda, na hii itampa nguvu ya kutumia mabavu kubaki madarakani.
Ataivuruga sana nchi hii, sio ndani ya nchi tu, bali hata juu ya mahusiano yetu na nchi nyingine.
Ni kama waTanzania hawakujifunza lolote katika miaka yake mitano inayomalizika sasa!
Kwa hali ya kawaida huyu hastahiri kubaki madarakani hata kwa dakika moja zaidi baada ya Oktoba 28.