Elections 2015 Shuhudieni CCM walivyoshangilia tishio la kupotezwa kwa Watanzania wenzao wenye mawazo tofauti, halafu eti tunashangaa ndugu zetu wapinzani kupotea!

Elections 2015 Shuhudieni CCM walivyoshangilia tishio la kupotezwa kwa Watanzania wenzao wenye mawazo tofauti, halafu eti tunashangaa ndugu zetu wapinzani kupotea!

Safari hii itakuwa ya kushangaza sana jinsi waTanzania tusivyochukulia kwa uzito sahihi mambo mazito yanayohusu nchi yetu.

Mtu kutoka nyumbani asubuhi na mapema kwenda kupanga mstari kumchagua mtu kama huyu ambaye hafichi kabisa tabia zake!
Na sababu ya kumchagua. anajenga barabara; kana kwamba barabara zimeanza kujengwa na yeye, na atakapochukuliwa na muumba wake Tanzania hakutajengwa barabara tena!

Huyu alitakiwa waTanzania wamkatae kwa kura nyingi, kiasi kwamba hata angetumia nguvu kulazimisha ushindi ingeonekana dhahiri mbele za macho ya dunia. Kura atakazopewa zitakuwa nyingi hata kama hatashinda, na hii itampa nguvu ya kutumia mabavu kubaki madarakani.

Ataivuruga sana nchi hii, sio ndani ya nchi tu, bali hata juu ya mahusiano yetu na nchi nyingine.

Ni kama waTanzania hawakujifunza lolote katika miaka yake mitano inayomalizika sasa!

Kwa hali ya kawaida huyu hastahiri kubaki madarakani hata kwa dakika moja zaidi baada ya Oktoba 28.
 
Sitashangaa kama baada ya tishio lake hili lililoonekana kuungwa mkono na uongozi wa juu wa CCM ndio kikosi cha wasiojulikana kikaundwa. RIP Ben Saanane, RIP Azory Gwanda, RIP Watanzania waliopotezwa katika hiyo miaka mitano.

Tarehe 28/10/2020 na bado siku mbili tu tuhakikishe tunakomesha kabisa ukatili huu tulioushuhudia. CCM na mgombea wake OUT!
Watu wanachukulia kimzahamzaha mambo mazito kama haya.

Huyu ni kiongozi wa juu kabisa wa nchi, anatoa matamshi kama haya, tena hadharani na watu wanashangilia, kama walivyoshangilia alipomtaja Lissu kuwa "msaliti" ambaye alistahiri kuuawa. Watu bado hawaelewi?

Nadhani matamshi kama haya ni muhimu yawekwe kama ushahidi, iwe sehemu ya rekodi zitakazotumika wakati watu watakapoendelea kupotezwa.

Mtu, tena kiongozi, unayatamka haya maneno kwa minajili ipi, kutisha/kuogopesha watu, au kuna sababu ipi inayofanya haya maneno yasemwe mbele ya kadamnasi!
 
Amina na hakika..

Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) sina hakika kama litaingia moja kwa moja labda kwa sura nyingine..

Nililo na uhakika nalo ni hili, kuwa, serikali yote kwa maana ya Idara na taasisi zake kubwa kwa ndogo, watumishi wote kuanzia mfagizi hadi mawaziri wanayo maagizo ya kuhakikisha Magufuli anashinda "mitano tena"..

Na ofcoz hatuna option, isipokuwa ktk hatua hizi za awali tunatii na kutekeleza maagizo yake kwa sababu bado ana mamlaka na nguvu ya madaraka ya urais..

Lakini mioyo yetu tuliowengi iko mbali naye. Kwenye field tunatenda kinyume chake kabisa...

Ni kwamba, tunatamani ashindwe sawia kwa sababu ni utumwa mbaya sana kufanya kazi chini ya bosi asiye na utu, mbinafsi, anayejijali na kujiangalia mwenyewe tu, asiyejali hisia za watu wengine na anayetaka kuabudiwa na kusujudiwa kama vile yeye ni Mungu fulani hivi...

Ninasema hili kwa uhakika wa 100% maana mimi pia ni mtumishi wa serikali hii na ni msimamizi wa uchaguzi huu na kwa kiasi kikubwa naelewa kila kinachoendelea ndani ya serikali..!

Ametutishia kuwa, kama ikitokea akashinda na akawa Rais na yeyote yule aliye serikalini na anasimamia uchaguzi huu ikatokea katika eneo alilopewa kusimamia kusaidia ushindi wake ameshindwa kutimiza lengo, basi ajihesabu hana kazi..!!!

Hiki ni kitisho cha kwelikweli, wala siyo mzaha. Na hawa wengi wanapigania vibarua vyao kwa gharama yoyote. Wako tayari kuua watu hawa...

Kitisho hiki kiko kwa maRPC, DCs, OCDs, wakurugenzi wa majiji/manispaa/miji/wilaya (ambao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo), wakuu wa idara na taasisi za umma kama TISS, CID nk, maafisa tarafa na watendaji wa kata..

Wote hawa wanatetea ugali na chakula chao. Na pesa iliyoachiliwa kufanikisha hili ni nyingi ajabu mtu hawezi kuamini..

Na tunaposema kuwa, uchaguzi huu ni wa KUFA ama KUPONA mtu maana yake ni hii..

Hata hivyo, si wote hawa wanaunga mkono. Si wote tunakubaliana naye eti tu risk maisha yetu kutetea UOVU WA MTU MMOJA tu..

Si ajabu hii kitu inayoendelea sasa ika back fire kwa kiwango cha juu..

Na Moshi mweupe kumpa "go ahead" Tundu Lissu kuwa kiongozi wa nchi hii, unaonekana kidogo kidogo na utadhihiri kabisa ifikapo tarehe 28/10/2020 saa 5:59 usiku..

Hii itawashangaza wengi. Wengi watapigwa na butwaa kubwa. Hawataamini kabisa kuwa, kumbe yaliyo magumu kwa binadamu, kwa Mungu Yehova ni rahisi sana..

Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla kumshinda Magufuli na CCM yake machoni mwa binadamu inaonekana kama vile sawa na sisimizi kulidondosha jengo lefu la ghorofa la UBUNGO PLAZA..!

Lakini huu ndiyo wakati wa sisimizi kufanya muujiza, ni wakati wa sisimizi kudondosha ghorofa lefu na kubwa la mfano huu..

Tuzidi kuomba na kumwombea huyu mtu ambaye Mungu ameamua kupitia kwake wanadamu Watanzania wakombolewe..
 
Kitisho hiki kiko kwa maRPC, DCs, OCDs, wakurugenzi wa majiji/manispaa/miji/wilaya (ambao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo), wakuu wa idara na taasisi za umma kama TISS, CID nk, maafisa tarafa na watendaji wa kata..

Wote hawa wanatetea ugali na chakula chao. Na pesa iliyoachiliwa kufanikisha hili ni nyingi ajabu mtu hawezi kuamini..

Na tunaposema kuwa, uchaguzi huu ni wa KUFA ama KUPONA mtu maana yake ni hii..
Vitisho mbele ya uhai wa Taifa letu..., kama mtu anayo chembe hata hafifu ya uzalendo ndani yake, ni wakati wa kusimamia uzalendo huo.

Hawa wote wanaopewa maelekezo, wakiyakataa, atawafukuza kazi wote?
 
Kweli huu ni uuaji wa makusudi! Anathubutu kusema angepoteza watu kwa kumtanguliza Mungu mbele kwa sababu tu wameonyesha msimamo tofauti na wake? This is very very serious case! Na hayo manyumbu yenye kijani yakashangilia kwa nguvu kama yamepewa zawdi.

Uzuri ni kuwa baada ya kutoa hili tamko kuna miongoni mwa hao hao waliokuwa wanashangalia walikuja kupambana na uovu wake. Asante sana kwa hii clip. Imeondoa shaka zote kuwa ni nani mhusika wa watu kupotea kwa watu huku akijinasibu kuwa anamtanguliza Mungu mbele.
 
Safari hii itakuwa ya kushangaza sana jinsi waTanzania tusivyochukulia kwa uzito sahihi mambo mazito yanayohusu nchi yetu.

Mtu kutoka nyumbani asubuhi na mapema kwenda kupanga mstari kumchagua mtu kama huyu ambaye hafichi kabisa tabia zake!
Na sababu ya kumchagua..., anajenga barabara; kana kwamba barabara zimeanza kujengwa na yeye, na atakapochukuliwa na muumba wake Tanzania hakutajengwa barabara tena!

Huyu alitakiwa waTanzania wamkatae kwa kura nyingi, kiasi kwamba hata angetumia nguvu kulazimisha ushindi ingeonekana dhahiri mbele za macho ya dunia. Kura atakazopewa zitakuwa nyingi hata kama hatashinda, na hii itampa nguvu ya kutumia mabavu kubaki madarakani.

Ataivuruga sana nchi hii, sio ndani ya nchi tu, bali hata juu ya mahusiano yetu na nchi nyingine.

Ni kama waTanzania hawakujifunza lolote katika miaka yake mitano inayomalizika sasa!

Kwa hali ya kawaida huyu hastahiri kubaki madarakani hata kwa dakika moja zaidi baada ya Oktoba 28.
Kalamu1
Wale wote watakaokwenda na kumpigia kura huyu dhalimu Jiwe, nao watapata laana katika maisha yao yote..................

Kwa kuwa Mungu wetu ni wa haki, hivyo huyu Jiwe, Mara kwa Mara kujifanya kuwa anamuhofu Mungu, ni utapeli wa hali ya juu Sana
 
Amina na hakika..

Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) sina hakika kama litaingia moja kwa moja labda kwa sura nyingine..

Nililo na uhakika nalo ni hili, kuwa, serikali yote kwa maana ya Idara na taasisi zake kubwa kwa ndogo, watumishi wote kuanzia mfagizi hadi mawaziri wanayo maagizo ya kuhakikisha Magufuli anashinda "mitano tena"..

Na ofcoz hatuna option, isipokuwa ktk hatua hizi za awali tunatii na kutekeleza maagizo yake kwa sababu bado ana mamlaka na nguvu ya madaraka ya urais..

Lakini mioyo yetu tuliowengi iko mbali naye. Kwenye field tunatenda kinyume chake kabisa...

Ni kwamba, tunatamani ashindwe sawia kwa sababu ni utumwa mbaya sana kufanya kazi chini ya bosi asiye na utu, mbinafsi, anayejijali na kujiangalia mwenyewe tu, asiyejali hisia za watu wengine na anayetaka kuabudiwa na kusujudiwa kama vile yeye ni Mungu fulani hivi...

Ninasema hili kwa uhakika wa 100% maana mimi pia ni mtumishi wa serikali hii na ni msimamizi wa uchaguzi huu na kwa kiasi kikubwa naelewa kila kinachoendelea ndani ya serikali..!

Ametutishia kuwa, kama ikitokea akashinda na akawa Rais na yeyote yule aliye serikalini na anasimamia uchaguzi huu ikatokea katika eneo alilopewa kusimamia kusaidia ushindi wake ameshindwa kutimiza lengo, basi ajihesabu hana kazi..!!!

Hiki ni kitisho cha kwelikweli, wala siyo mzaha. Na hawa wengi wanapigania vibarua vyao kwa gharama yoyote. Wako tayari kuua watu hawa...

Kitisho hiki kiko kwa maRPC, DCs, OCDs, wakurugenzi wa majiji/manispaa/miji/wilaya (ambao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo), wakuu wa idara na taasisi za umma kama TISS, CID nk, maafisa tarafa na watendaji wa kata..

Wote hawa wanatetea ugali na chakula chao. Na pesa iliyoachiliwa kufanikisha hili ni nyingi ajabu mtu hawezi kuamini..

Na tunaposema kuwa, uchaguzi huu ni wa KUFA ama KUPONA mtu maana yake ni hii..

Hata hivyo, si wote hawa wanaunga mkono. Si wote tunakubaliana naye eti tu risk maisha yetu kutetea UOVU WA MTU MMOJA tu..

Si ajabu hii kitu inayoendelea sasa ika back fire kwa kiwango cha juu..

Na Moshi mweupe kumpa "go ahead" Tundu Lissu kuwa kiongozi wa nchi hii, unaonekana kidogo kidogo na utadhihiri kabisa ifikapo tarehe 28/10/2020 saa 5:59 usiku..

Hii itawashangaza wengi. Wengi watapigwa na butwaa kubwa. Hawataamini kabisa kuwa, kumbe yaliyo magumu kwa binadamu, kwa Mungu Yehova ni rahisi sana..

Tundu Lissu na CHADEMA kumshinda Magufuli na CCM ni machoni mwa binadamu inaonekana kama vile sawa na sisimizi kulidondosha jengo lefu la ghorofa la UBUNGO PLAZA..!

Lakini ni wakati wa sisimizi kudondosha gjorofa lefu la mfano huu..

Tuzidi kuomba na kumwombea huyu mtu ambaye Mungu ameamua kupitia kwake wanadamu Watanzania wakombolewe..
Mkuu najua ni vigumu sana lakini ni wakati wa kila mtu kusema hapana. Nakuapia huyu kama kila mtu akikataa uovu na kuunganisha nguvu ataanguka vibaya sana sana. Anachukiwa kupita maelezo na tatizo lipo tu ni nani aanze... Miaka ya nyuma CCM ilikuwa na nguvu vijijini lakini mwaka huu vijijini ndiyo watu hawaitaki kabisa.

Kuna jamaa zangu wengi walikuwa wana CCM wa kweli na washabiki waliokubuhu kila kipindi cha uchaguzi lakini safari hii hawataki kumsikia huyu rais kabisa. Polisi na hata jeshini watu wanafuata amri kwa shingo upande lakini likitokea tukio moja dogo tu linaweza ku-activate chain of reactions na Magufuli akaanguka vinaya sana.
 
Kalamu1
Wale wote watakaokwenda na kumpigia kura huyu dhalimu Jiwe, nao watapata laana katika maisha yao yote..................

Kwa kuwa Mungu wetu ni wa haki, hivyo huyu Jiwe, Mara kwa Mara kujifanya kuwa anamuhofu Mungu, ni utapeli wa hali ya juu Sana
Kura atapigiwa na watu wachache. Wanaomkataa ni wengi. Kazi ipo kwenye kujumlisha na kutoa matokeo. Kwenye kukataliwa kwa kura wale tusiwe na shaka. Shaka tuweke kwenye namna ya kulinda ushindi na kuhakikisha kura za bandia hazipenyezwi.
 
The Palm Tree
Hakika umetufungua macho na masikio yetu..........

Ninadiriki kusema kuwa huyu Jiwe ni jambazi sawasawa na majambazi wengine wanaowaua watu kwa silaha.......

Hakika wale wote watakaosaidia udhalimu huo wa kuiba kura, watapata laana katika maisha yao yote!
 
Hii nchi siku hizi imekuwa ya kishenzi sana. Huu ushenzi ulianza zamani ila sasa umefikia kiwango cha kutisha.
 
Kweli huu ni uuaji wa makusudi! Anathubutu kusema angepoteza watu kwa kumtanguliza Mungu mbele kwa sababu tu wameonyesha msimamo tofauti na wake? This is very very serious case! Na hayo manyumbu yenye kijani yakashangilia kwa nguvu kama yamepewa zawdi. Uzuri ni kuwa baada ya kutoa hili tamko kuna miongoni mwa hao hao waliokuwa wanashangalia walikuja kupambana na uovu wake. Asante sana kwa hii clip. Imeondoa shaka zote kuwa ni nani mhusika wa watu kupotea kwa watu huku akijinasibu kuwa anamtanguliza Mungu mbele.
Ukweli ni kwamba Magufuli anachukiwa hadi vijijini, anachukiwa hadi ndani ya familia yake, anachukiwa hadi na watoto wadogo, anachukiwa hadi ndani ya vyombo vyetu vya dola na anachukiwa hadi na watu aliowateua yeye mwenyewe.

Tatizo lipo kwa kijundi kidogo cha watu aliowapa madaraka makubwa yanayowazidi uwezo kama yeye alivyosukumiziwa na hivyo utii wao haupo kwa taifa bali kwa huyo mtu kwa sababu kwa namna fulani wanazo tabia kama zake.

Fikiria watu kama Ole Sabaya, watu kama Makonda, watu kama Gambo Mrisho, naam watu kama hao. Juzi tu huyo Bashite kajaribu bahati yake kugombea ubunge ndani ya CCM hiyo hiyo lakini hata huko wananchi wakamkataa.

Sasa unabaki unajiuliza Magufuli aliona nini kwake hadi kumpa cheo kikubwa kama hicho. Je aliwezaje kupewa ukuu wa Mkoa tena wa jiji kama Dar es Salaam? Hebu mumsikilize tena alivyowajibu wana Kagera baada ya tetemeko lililowakumba.

Kwa kweli huyu mtu hatufai, hatufai, hatufai...tunahitaji kulikomboa taifa kutoka mikononi mwake!
 
Ukweli ni kwamba Magufuli anachukiwa hadi vijijini, anachukiwa hadi ndani ya familia yake, anachukiwa hadi na watoto wadogo, anachukiwa hadi ndani ya vyombo vyetu vya dola na anachukiwa hadi na watu aliowateua yeye mwenyewe. Tatizo lipo kwa kijundi kidogo cha watu aliowapa madaraka makubwa yanayowazidi uwezo kama yeye alivyopewa na hivyo utii wao haupo kwa taifa bali kwa huyo mtu kwa sababu kwa namna fulani wanazo tabia kama zake.

Wanaomtetea ni watu wabinafsi na wanafiki ambao wanaamini bila yeye hawangekuwa walipo. Fikiria watu kama Ole Sabaya, watu kama Makonda, watu kama Gambo Mrisho, naam watu kama hao. Juzi tu huyo Bashite kajaribu bahati yake kugombea ubunge ndani ya CCM hiyo hiyo lakini hakuweza kupenya. Sasa unabaki unajiuliza aliwezaje kupewa ukuu wa Mkoa tena wa jiji kama Dar es Salaam? Hebu mumsikilize tena alivyowajibu wana Kagera baada ya tetemeko lililowakumba.

Kwa kweli huyu mtu hatufai, hatufai, hatufai...tunahitaji kulikomboa taifa kutoka mikononi mwake!
Ila watanzania nao tuna nafasi ya lawama. Anapokuwa anatema ugoro kama huu bado kuna watu wanamshangilia na kucheka na yeye alivyo mtupu anafikiri ameongea jambo la maana. Kwa mfano hapa yeye anasema haoni uhusiano kati ya tetemeko na kukosekana kwa chakula!

Huyu ni msomi mwenye Phd! Aliniacha tena hoi siku moja alipokuwa anahoji Kenya walipoweka curfew ya kutembea usiku eti ''kwani virus wa corona wanaambukiza usiku tu?'' Such a foolish comment from Phd holder.
 
Ila watanzania nao tuna nafasi ya lawama. Anapokuwa anatema ugoro kama huu bado kuna watu wanamshangilia na kucheka na yeye alivyo mtupu anafikiri ameongea jambo la maana. Kwa mfano hapa yeye anasema haoni uhusiano kati ya tetemeko na kukosekana kwa chakula! Huyu ni msomi mwenye Phd! Aliniacha tena hoi siku moja alipokuwa anahoji Kenya walipoweka curfew ya kutembea usiku eti ''kwani virus wa corona wanaambukiza usiku tu?'' Such a foolish comment from Phd holder.
Ndugu yangu kuna vyombo kama TBC. Hiki chombo kinachosikika hadi vijijini lakini 24/7 kinarusha sifa za mtu moja. Viko vyombo vya usalama ambavyo vinatakiwa kuwalinda wananchi na mali zao lakini vimegeuka vyombo vya ukandamizaji, vinamlinda mtu moja.

Tunavyo vyombo rasmi vya uwakilishi vya kipekee duniani kwani utii wake ni kwa serikali na mtu moja, si wananchi. Tunavyo vyombo rasmi vya kutoa haki lakini vimegeuka na kuwa vyombo vya kuwanyang'anya wananchi haki zao za msingi kwa maelekezo ya mtu moja.

Badala yake na ili kuhakikisha kelele za wananchi haziwanyimi usingizi hawa watawala wetu, vimeundwa vyombo vingine visivyo rasmi. Hivi naweza kuvifananisha na vyombo vya giza, havionekani wala havijulikani lakini matokeo ya unyama wao yanatisha.
 
Naam, hiyo ndiyo Tanzania na hao ndio viongozi wa chama tawala wanaotaka tuwape ridhaa ya kuendelea kututawala kwa miaka mingine mitano. Cha ajabu ni kwamba wapo Watanzania wenzetu ambao wako tayari kutoa ridhaa hiyo bila hata kuhoji.

Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba tukifanya makosa tena, safari hii tutalia sana kwani kama alivyowahi kuonya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP), aliyeonja nyama ya mtu haachi.
Hizi ni mbinu tu. Toa video yote ili tujuwe kasema nini.Wewe umetoa sentenso moja na hatujui qualifier za aliyoyasema zikoje. Hii wapelekee wajinga ndiyo watakuamini!
 
Kinachoogofya zaidi ni huyu mtu kupewa miaka mingine mitano licha ya kwamba hapendwi kabisa. Waoga, wanafiki na walafi wameamua kuvitumia vyombo vya dola kumsukumizia miaka mingine mitano, je tutapona? Hilo ndilo swali ambalo kila Mtanzania itabidi ajiulize.

Mh. Tundu Antiphas Lissu hakuogopa kukabiliana naye face to face na akamiminiwa risasi za kumwangusha tembo lakini Mungu akakataa na hakuanguka, aliendelea kusimama! Na sasa karudi kuendeleza mapambano na safari hii, nadhani hata Jeshi Letu tukufu litatumika.

Wacha Mungu yatubidi tusali sana, shetani atatumia silaha zote lakini Mh. Lissu keshatukumbusha giza si kitu mbele ya mwanga. Lazima tuwe jasiri, historia haitatusahau, itatukumbuka.
Kisha pata mitano. Kajinyinge.
 
Naam, hiyo ndiyo Tanzania na hao ndio viongozi wa chama tawala wanaotaka tuwape ridhaa ya kuendelea kututawala kwa miaka mingine mitano. Cha ajabu ni kwamba wapo Watanzania wenzetu ambao wako tayari kutoa ridhaa hiyo bila hata kuhoji.

Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba tukifanya makosa tena, safari hii tutalia sana kwani kama alivyowahi kuonya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP), aliyeonja nyama ya mtu haachi.
Anajaribu kumtanguliza Mungu, tuanze kujiuliza Mungu anayemsema ni yupi?
 
Kisha pata mitano. Kajinyinge.
Kajinyinge? Ushamba na ulimbukeni utawamaliza. Mitano mingine ni ishara tu ya laana kuongezeka na hata hiyo ikiisha anaweza akapata hata mingine kumi, si amekamata mpini?

Lakini iko siku atatoka tu. Idi Amin Dada wa Uganda alidai kuota ndoto iliyomwezesha kujua hata siku yake ya kufa hivyo hatishiki. Naye alikuwa na wafuasi wanaofanana na wewe. Siku yake ilifika na akaikimbia nchi yake. Alikuja kufia mafichoni mbali kabisa na nchi yake.
 
Back
Top Bottom