pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Kenya tupo kwenye Pool B, pamoja na S.Africa, Ireland na Canada. Sheria zimerejea kama zilivokuwa hapo awali, baada ya malalamishi kutoka kwa mashabiki kote duniani. Timu mbili zitakazo ongoza kwenye pool zao zitaingia moja kwa moja kwenye nane bora.
Shujaa, timu ya Kenya Raga7s ilitua Kenya jumanne kutoka Sydney, Australia ambapo walishiriki kwenye mchuano wa Sydney 7s. Hiyo ilikuwa ni '4th leg' ya msururu wa World Rugby7s Series Circuit 2020. Kabla ya hapo walikuwa kule Hamilton 7s, ambapo waliibuka kwenye nafasi ya nane. Ndio mwanzo tu, Los Angeles 7s itakuwa kutoka Feb. 29- Machi 3. Baada ya hapo Shujaa watamenyana na wenzao kwenye '6th leg', Vancouver 7s, kisha Paris7s. Shujaa drawn against SA, Ireland and Canada in Los Angeles 7s