Shukrani kwa Jamii Forums kwa kunipa Tuzo 🙏🏽

Salaam kwenu wanajukwaa.

Ningependa kuwashukuru Jamii Forums (JF) kwa tuzo hii ya kipekee.

Ni fahari yangu kutambuliwa kuwa kiongozi anayepokea maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi kupitia majukwaa ya kidijitali.
Pia, ni heshima kwa Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyeniamini na kunipa nafasi na fursa ya kutumikia jamii kupitia wizara hii ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu.

Vilevile, heshima hii iende kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu na watumishi wake wote na wale wa kisekta ambao, hupokea na kuyafanyia kazi maelekezo yangu kufuatia maoni na hoja za wananchi ambazo nimekuwa nimezipokea kutoka kwenye Jukwaa la Jamii Forums.
Vilevile, Heshima hii iende kwa familia yangu na mume wangu mpenzi Advocate Gwajima ambaye, amekuwa akinipa ushirikiano mkubwa wakati wote wa kutumia hata muda wa familia kwa ajili ya kufuatilia hoja za wananchi kwenye Jukwaa hili.

Naahidi kuendelea kujitahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi ili kuhakikisha sauti zote zinasikilizwa na kufanyiwa kazi inapowezekana.
Kila mmoja wetu ana nafasi muhimu katika mchakato wa uamuzi, na ni wajibu wetu kama viongozi kusikiliza na kujibu yale yanayohitaji majibu ya wananchi.

Tunapofanya kazi pamoja, tunafanikisha kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wetu.
Ningependa kutoa shukrani za pekee kwa Jamii Forums (JF) na watanzania kwa ujumla kwa utambuzi huu.

Majukwaa kama JF ni muhimu kwa ajili ya kuleta uwazi na ushirikiano, na ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana katika kujenga jamii bora zaidi.

Shukrani nyingi kwenu wanaJukwaa wote na wote ambao mmewahi kutoa hoja kuhusiana na eneo langu la kazi, kwani hakika, mmekuwa sababu ya mimi kupata Tuzo hii adhimu. Naomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii ya maendeleo.

Mbarikiwe🙏🏽🇹🇿
Cookie mbona sijakuona kweny picha leo
 
Mheshimiwa naomba unikopeshe buku 15 hapo... kuna mchongo masikilizia hapa kesho kutwa uwakika nakurudshia
 
Hongera sana kiongozi wetu kwa kuwa sehemu ya hii familia muhimu kwa ujenzi na ustawi wa taifa letu. Naamini tuzo hii itakuwa alama na taa kwa mawaziri wengine ambao pengine wizara na sekta wanazozisimamia zinahitaji masikio mengi ya kusikiliza kuliko ilivyo wizara yako na sekta zake. Mwenyezi Mungu aendelee kukuinua na kuendelea kukuweka karibu na wananchi
 
Salaam kwenu wanajukwaa.

Ningependa kuwashukuru Jamii Forums (JF) kwa tuzo hii ya kipekee.

Ni fahari yangu kutambuliwa kuwa kiongozi anayepokea maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi kupitia majukwaa ya kidijitali.
Pia, ni heshima kwa Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyeniamini na kunipa nafasi na fursa ya kutumikia jamii kupitia wizara hii ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu.

Vilevile, heshima hii iende kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu na watumishi wake wote na wale wa kisekta ambao, hupokea na kuyafanyia kazi maelekezo yangu kufuatia maoni na hoja za wananchi ambazo nimekuwa nimezipokea kutoka kwenye Jukwaa la Jamii Forums.
Vilevile, Heshima hii iende kwa familia yangu na mume wangu mpenzi Advocate Gwajima ambaye, amekuwa akinipa ushirikiano mkubwa wakati wote wa kutumia hata muda wa familia kwa ajili ya kufuatilia hoja za wananchi kwenye Jukwaa hili.

Naahidi kuendelea kujitahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi ili kuhakikisha sauti zote zinasikilizwa na kufanyiwa kazi inapowezekana.
Kila mmoja wetu ana nafasi muhimu katika mchakato wa uamuzi, na ni wajibu wetu kama viongozi kusikiliza na kujibu yale yanayohitaji majibu ya wananchi.

Tunapofanya kazi pamoja, tunafanikisha kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wetu.
Ningependa kutoa shukrani za pekee kwa Jamii Forums (JF) na watanzania kwa ujumla kwa utambuzi huu.

Majukwaa kama JF ni muhimu kwa ajili ya kuleta uwazi na ushirikiano, na ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana katika kujenga jamii bora zaidi.

Shukrani nyingi kwenu wanaJukwaa wote na wote ambao mmewahi kutoa hoja kuhusiana na eneo langu la kazi, kwani hakika, mmekuwa sababu ya mimi kupata Tuzo hii adhimu. Naomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii ya maendeleo.

Mbarikiwe🙏🏽🇹🇿
Hakika we ni kiongoz ambaye jf tunaweza kujivunia tunakupenda sna wazir
 
Ninakupongeza sana kwa kulipa nafasi hili jukwaa. Tunahitaji viongozi wanaofikika kwa njia zote na kufanyia kazi mambo yanayoibuliwa.

Naamini kupitia humu itakupa chachu na ubunifu katika uongozi wako.

Hongera sana mh waziri.
 
Salaam kwenu wanajukwaa.

Ningependa kuwashukuru Jamii Forums (JF) kwa tuzo hii ya kipekee.

Ni fahari yangu kutambuliwa kuwa kiongozi anayepokea maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi kupitia majukwaa ya kidijitali.
Pia, ni heshima kwa Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyeniamini na kunipa nafasi na fursa ya kutumikia jamii kupitia wizara hii ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu.

Vilevile, heshima hii iende kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu na watumishi wake wote na wale wa kisekta ambao, hupokea na kuyafanyia kazi maelekezo yangu kufuatia maoni na hoja za wananchi ambazo nimekuwa nimezipokea kutoka kwenye Jukwaa la Jamii Forums.
Vilevile, Heshima hii iende kwa familia yangu na mume wangu mpenzi Advocate Gwajima ambaye, amekuwa akinipa ushirikiano mkubwa wakati wote wa kutumia hata muda wa familia kwa ajili ya kufuatilia hoja za wananchi kwenye Jukwaa hili.

Naahidi kuendelea kujitahidi kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Wananchi ili kuhakikisha sauti zote zinasikilizwa na kufanyiwa kazi inapowezekana.
Kila mmoja wetu ana nafasi muhimu katika mchakato wa uamuzi, na ni wajibu wetu kama viongozi kusikiliza na kujibu yale yanayohitaji majibu ya wananchi.

Tunapofanya kazi pamoja, tunafanikisha kuchochea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wetu.
Ningependa kutoa shukrani za pekee kwa Jamii Forums (JF) na watanzania kwa ujumla kwa utambuzi huu.

Majukwaa kama JF ni muhimu kwa ajili ya kuleta uwazi na ushirikiano, na ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushirikiana katika kujenga jamii bora zaidi.

Shukrani nyingi kwenu wanaJukwaa wote na wote ambao mmewahi kutoa hoja kuhusiana na eneo langu la kazi, kwani hakika, mmekuwa sababu ya mimi kupata Tuzo hii adhimu. Naomba tuendelee kuwa pamoja katika safari hii ya maendeleo.

Mbarikiwe🙏🏽🇹🇿
Mheshimiwa naomba unieleweshe kidogo kama huta kadirika, hivi wewe ni mke wa Josephat Gwajima.
 
Ila muheshimiwa hapo ulikuwa pambe sio kwa kupendeza huko

Anyway mimi mlokole uwe wa asili achana na mawigi

Last we mwamba sana unatukosha wabongo kwa kujibu mada tata kwa weredi Mungu akupe maisha marefu uwe mfano wa kuigwa

Dkt. Gwajima D
 
Hujambo mwanangu? Ukweli utabaki hivi, yeye ndiye aliyeniteua tena kwenye Awamu yake ya uongozi na kunipa nafasi ya kutumika kwenye serikali yake hadi hapa nilipo sasa. Asingeniteua na kunipa nafasi kwenye serikali yake na kunipa haya majukumu, huenda nisingepata nafasi ya kutumikia jamii kwa hatua hii. Ni vema kuwa na mioyo ya shukrani siyo tu kwa Mwenyezi Mungu bali kwa Kila aliyekuamini na kukupa nafasi utumike hapo unapotumika. Ndiyo maana hata watoa hoja za humu jukwaani nimewashukuru pamoja na wewe ndugu yangu mwema🙏🏽
What humble words from humble super woman.
 
Bado sijaona kiongozi anayepokea ishu/ maoni kupitia digital platforms na kuzifanyia kazi zaidi yako.

I hope hii tuzo itawaamsha na wengine.

Hongera Mheshimiwa.
Kuna mmoja alikuwa kule Twitter (x) akawa akitofautiana na watoa maoni anaishia kumwaga matusi. Mzee wa goli la mkono. Sasa hivi yupo benchi
 
Mnatukwaza sana,Kila neno lazima mseme serikali inayoongozwa na .........

Kwani Kuna asiejua.
Mnatumia nguvu kumtajataja Kuna nn au ndo kujipendekeza mh.

Kila mwanaccm,hamwezi hata kutaja jina la Mungu kabula hajatanguliza Bibi,bibi,bibi,bibi.
Sijui mtakuja kujielewa Karne gani.
All in all hongera,ila sio Kila inshu lazima umtaje Rais.
Kiufupi,ccm ilifeli mda mrefu mjitafakari Mpo kwa maslahi yenu na sio ya Taifa.
 
Back
Top Bottom