Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 1,710
- 8,690
Wasaalam.
Napenda kutoa Shukrani zangu za dhati kwa maelfu ya wana JF wa Jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko waliojitokeza kwa wingi kushiriki mjadala tajwa hapo juu ambao, niliupandisha jana jioni 22 Julai, 2025.
Hakika, uwingi wa wachangiaji hadi kufikia takribani 9K leo mchana na maoni karibu 800 na yanaendelea, ni ishara tosha kuwa, mada hii inagusa sehemu kubwa ya jamii na inahitaji kupewa uzito unaostahili ili, kuirejesha jamii yetu hususan eneo la mahusiano ya kike na kiume kwenye kufahamu wapi wanapishana kimtazamo, lugha, ushirikiano na nyanja zingine zote ili, wajirekebishe kwa ajili ya kulinda ustawi chanya wa familia na hususan watoto.
Aidha, nimejitahidi kushiriki mjadala kwa kujibu, kufafanua, kuelezea na kupokea maoni mengi ambayo, yako chanya kwa ajili ya kufanyia kazi kimkakati hata hivyo, siyo rahisi kupitia yote kwa sasa, nitaendelea.
Naahidi, kusajili maoni yote ya mjadala huu hapa JF na ya Instagram na ya FB kisha, kuyafanyia uchambuzi kwa ajili, ya kuandaa vipindi vya jamii tuzungumze eneo hili ili, tuamshe ari ya jamii kutambua na kutoa yaliyo maoni yao pande zote yaani wanawake na wanaume ili, hatimaye mafunzo yatokanayo na mijadala hii kwa njia mbalimbali, yaokoe fikra zetu na kesho ya mahusiano yetu kwa maslahi ya watoto wetu wasio na hatia.
Shukrani kwa wote waliotoa mchango chanya na hata hasi vilevile kwani, tunatofautiana mitazamo ingawa, wote tunakuwa na nia njema ya kujenga.
Kupitia mjadala huu, tumeokoa muda na gharama kubwa za kutafuta maoni hata kama uwakilishi haukuwa na uwiano mzuri zaidi wa wanawake na wanaume, si haba, bado tumepata kianzio kikubwa cha wapi tuelekee ili, kuhuisha fikra za jamii yetu eneo hili.
Mungu awabariki wote wanajukwaa na waendeshaji wa jukwaa hili hapa JF.✍️