Shule 10 bora matokeo kidato cha sita 2021 hizi hapa

Chama langu Tabora Boys, heading Tanzania kama kawa.
 
HKL wameupiga mwingi sana

Leocadia Mbukilo ndiye aliyeshika nafasi ya kwanza kutoka shule ya Sekondari Machame Girls (Kilimanjaro) katika mchepuo wa HKL, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Isack Sanga kutoka Kisimiri Sekondari (Arusha).

Nafasi ya tatu hadi ya kumi imechukuliwa na wavulana kutoka sekondari ya Dareda (Manyara) na nafasi ya tatu imechukuliwa na Deogratias Maendeleo, akifuatiwa na Rafael Daqaro, aliyechukuwa nafasi ya nne huku nafasi ya tano ikichukuliwa na Brayan Minja (HGL).

Giliad Msungu ameshika nafasi ya sita huku nafasi ya saba ikichukuliwa na Rashidi Behero na nafasi ya nane ikichukuliwa na Salimu Ismail wote mchepuo wa HKL.

Nafasi ya tisa amechukua Ibrahim Makongoro (HKL) huku Aidan Daniel kutoka HGL akichukuwa nafasi ya 10.
 
Hivi Ile nlisoma ilikua ni shule kweli ama madrasa tu....maana hata 100 bora huwa siioni ....πŸ€”
Enzi zile nilipambana sana walau niibebe shule lakini wapi ,nikaambulia four nzuri.
 
Hivi hii imekaaje, yani kitaifa Mkoa ulioongoza ni Singida,, lakini kwenye top ten hamna shule ya singida hata moja.
 
Mungu mwema binti yangu no.4 kalipa one ya baba yake kweli historia inajirudia. Tabora Girls
 
Pugu, azania, tambaza n.k zinazalisha vilaza tu siku hizi
Umeuliza swali nililotaka kuuliza nikiongezea Kibaha na Ilboru

NB: Nimeangalia raw data, inaonekana Kibaha na Iliboru pia walipiga ila walikuwa na walifyata wengie kidogo, kwa hivyo wastani ukawa chini. Hata hivyo baada ya kupitia data za shule nyingi, nina wasiwasi kuwa huenda standard imetelemka kidogo kupunguza failure rates kwani Div I ni nyingi sana kuliko wastani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…