robbyr
Senior Member
- Apr 8, 2017
- 129
- 221
Katika kasi ya mabadiliko ya mtaala niliona shule binafsi kama chachu kwa sababu ya uwezo wa kuweka miundo mbinu kwa ajili ya kuisaidia serikali ila kwa mazingira haya naona giza.
Siandike kuweka data ila kwa uzoefu wa miaka minne ni udhibitisho tosha.
Unanyanyasaji wa walimu, baadhi ya shule zinanyanyasa walimu hasa kwenye malipo hii ni kutokana na idada kubwa ya wahitaji wengi hivyo aliyepo kazi kutishiwa kufukuzwa endapo ataka mshahara. Pili malipo kuchukua muda, ni kweli kuendesha shule binafsi ni gharama ila kumekuwa na wamiliki kijiweka mbele wao na kupuuza wafanyakazi.
Serikali itazame hili suala ili pia wafanyakazi wa shule binafsi wawe sehemu ya taifa hili Katika mabadiliko ya elimu.
Mizigo mikubwa, licha ya wazazi kujitoa kulipa ada bado shule za binafsi zimeendelea kuajiri walimu wachache sana ambapo ningumu kufikia watoto kwa ubora zaidi. Maana yangu ni kwamba wazazi wamepeleka watoto huko wapate ahueni. Maoni, naona wazazi wa shule husika waunde kamati na iwe sehemu ya shule ili waone kama watoto wao wanatendewa haki ipasavyo.
Nimeshuhudia darasa la kwanza la watoto 40 yupo mwalimu mmoja tu na anafundisha masomo yote.
itaendelea