Kwa uzoefu wangu wa kusoma boys tupu toka form 1 mpaka form 6, ningekushauri:
Kwanza, mpeleke shule ya kutwa.
Sababu: mwanao anaingia adolescence. Anahitaji muongozo wa kiafya, kihisia na kijamii sasa kuliko wakati wowote. Boarding ataupata toka kwa watoto wenzie, nyumbani atupata toka kwenu wazazi wake. So, kupanga ni kuchagua.
Pili, Mpeleke shule ya mchanganyiko.
Sababu: Shule za jinsi moja ni scam. Maisha halisi hayapo hivyo. Wengi waliosoma huko kwa muda mrefu tuna struggle kuwaelewa wenzetu wa upande wa pili huku ukubwani, kwa vile ule muda wa kuwaelewa tuliukosa.
Kuna mambo ya hovyo tuliaminishana mabwenini na unconsciously yanasumbua mpaka sasa.
So, aende mixture huyo.