SoC01 Shule maalumu za Sayansi kwa wanawake za Mama Samia Hassan Suluhu

SoC01 Shule maalumu za Sayansi kwa wanawake za Mama Samia Hassan Suluhu

Stories of Change - 2021 Competition

kipenseli2021

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2021
Posts
1,390
Reaction score
1,431
Kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi MUNGU kwa ajili ya Rais wetu mpendwa Mama Samia Hassan Suluhu ambaye ni Rais wa Kwanza Mwanamke katika Taifa letu pendwa Tanzania na Afrika Mashariki.

Pili nitoe pongezi zangu za dhati kwa upeo wake mkubwa na nia ya dhati ya kuendeleza nchi yetu pendwa Tanzania,tatu nimpongezi kwa utaratibu alio jiwekea wa kukutana na makundi mbalimbali katika jamii na kuwasilikiliza kero na mapendekezo yahoo kwa ajili ya kuzitatua changamoto hizo,

Safari yake ya kukutana na makundi maalumu yalianza pindi tu ameapishwa alipo kutana na wazee wa Dar es salaam ambao walikuwa wanawakilisha wazee wot Mei 7 mkutano huu ulio fanyika jijini dar es salaam

Katika kuendeleza utaratibu wake mzuri wa kukutana na makundi mbalimbali katika jamii,tarehe 7 june Rais Samia Hassan Suluhu alikutana na kufanya mkutano na wanawake Dodoma.



Katika mkutano huo Rais Samia Hassan Suluhu aliaidi kujenga shule maalumu za sayansi kwa ajili ya wanawake

Nukuu “Mwezi Julai mwaka huu tutaanza kujenga shule za Sekondari za Mabweni kwenye kila mkoa kwa ajili ya kufundisha masomo ya sayansi kwa wanawake.” Amesema Rais Samia”

Pasipo kupotosha jamii natambua nia ya dhati ya serikali ni kuongeza idadi ya wasichana/wanawake katika Nyanja ya Sayansi tupate wahandisi wengi wa jinsi ya kike na kada nyingine za sayansi



MAPENDEKEZO YANGU JUU YA NAMNA GANI HIZI SHULE ZIWE HILI KUTIMIZA LENGO HILO LA KUWA NA WANASAYANSI WENGI WASICHANA

Napenda kupendekeza mambo yafuatayo katika shule hizo tarajiwa za sayansi kwa wasichana,

Mapendekezo haya yanalenga katika vitu vifuatavyo


Mgawanyo wake
  • Kwa kuwa shule hizi zitajengwa katika kila mkoa lakini zote zikiwa na lengo moja basi nashauri zijengwe kwa lengo tofauti katika kila mkoa nikimaanisha kuwa tugawe Mikoa na katika kila mkoa basi tulenge kuwa katika mkoa huu basi lengo kubwa liwe kutoa wasichana ambao watakuwa wabobezi kwenye mambo ya Teknolojia ya sayansi na Habari ,mkoa mwingine tuwe na lengo la kutoa wasichana ambao watakuwa wamebobea katika Nyanja ya Utabibu/Madaktari na mkoa mwingine kuwa tunataka tutoe wasichana watakao bobea katika mambo ya Uhandisi wa Mitambo na Umeme hivyo hivyo tugawe mikoa kulingana na hitaji la kuandaa wasichana watakao kuwa wazuri kwenye Nyanja(Field) Fulani ya sayansi.
Udahili wa wanafunzi/wasichana
  • Udahili wa wanafunzi hawa uzingatie mambo mbalimbaili ikiwemo kipaji cha mwanafunzi kwenye mambo ya sayansi na kumuendeleza kulingana pia uzingatie ufaulu wake wa masomo ya sayansi tangu shule ya msingi.
Mitaala na mafunzo
  • Napendekeza shule hizi ziwe na mitaala tofauti nah ii inayo tumika,katika mitaala hii ya shule hizi maalumu za kuandaa wanasayansi wasichana basi mitaala hiwe imelenga kumjenga mwanafunzi katika ubunifu na vitendo kwa sayansi ime base kwenye ubunifu na vitendo (Practical and creativity)
Mgawanyo wa masomo
  • Katika shule hizi napenda mgawanyo wa masomo huwe kama ifuatavyo,kwanza mwanafunzi aruhusiwe kuchukua masomo matatu tu ya sayansi na somo moja liwe somo la Nyanja Fulani ya sayansi mfano
  • Mwanafunzi achukue
  • Fizikia
  • Hisabati
  • Kemia
Programming mfano (Java,Physon,C-programming)
Au achukue Fizikia,Hisabati,Kemia na Uhandisi wa Mitambo (Mechanics) au Ujenzi (Civil)
Mfano mwingine mwanafunzi achukue Fizikia,Biolojia,Kemia na somo moja la ujuzi Fulani mfano Anatomy nk
Hili kuweza kumjenga vizuri katika Nyanja Fulani ya sayansi
Mfano katika mataifa ya wenzetu wanafunzi wanaanza kujifunza program za kompyuta wakiwa na miaka kuanzia saba hivyo wanapata programmer wazuri kuliko kwetu mtu anaanza kujifunza akiwa na miaka 22-30 hakiwa chuo kikuu.
Walimu na rasilimali watu
  • Katika shule hizi kwa kuwa zimelenga kuandaa wanasayansi wa kike basi walimu wanatakiwa wawe na ujuzi wa vitendo (Practical) mfano Wahandisi,Madaktari nk hili kuwaaanda wasichana hawa waweze kuwa wanasayansi wazuri.
Majengo/Maabara
  • Shule hizi ziwe na majengo ya maabara yenye hadhi kubwa na vifaa vya kutosha vya kujifunzia mambo mbalimbali ya kisayansi.
  • HITIMISHO
  • Mimi nashauri shule hizi tarajiwa tuzibadilishe na kuwa mpango wa Taifa wa kuandaa wanasayani wa wasichana hivyo ziwe na sura tofauti tusiziendeshe kama Sekondari za kawaida kwani mtu anaweza somea masomo ya sekondari ya sayansi lakini hakifika kwenda chuo anaenda kusomea masomo ya biashara hivyo bado tutasuha suha
  • SHUKRANI:
  • Nampongeza Rais Mama Samia H.Suluhu kwa wazo lake zuri hivyo tunategemea watendaji wake watafanyia kazi hazima yake hiyo nzuri
  • Imeandaliwa na mimi kipenseli.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom