Shule nchi nzima zimefungwa kama hazijafungwa

Shule nchi nzima zimefungwa kama hazijafungwa

Kikwava

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2015
Posts
1,741
Reaction score
1,068
Kutokana na mwenendo wa shule hizi (msingi/sekondari) kwa miaka hii ya Sasa kutokufunga kabisa hasa kwa madarasa ya mitihani nashauri yafuatayo:

1. Badala ya kukaa na watoto kwa kipindi cha mwaka mzima bila likizo ya kurudi makwao basi wawape watoto kazi za nyumban kipindi cha likizo (home parkage) ambazo zikachukua maeneo yote muhimu ya kusoma.

2. Wafanye tafiti kutafuta ulinganifu wa ufaulu wa watoto kipindi ambacho shule zilifungwa kweli kweli na kipindi hiki ambacho ratiba inaonyesha kufungwa kwa shule lakini bado watoto wanaonekana mashuleni. Na Matokeo ya tafiti yawekwe wazi kwa watoto.

3. Nawapa hongera Walimu kwa kazi nzuri, HONGERENI WALIMU POPOTE MLIPO KWA KUJITUMA.
 
Hata ugali ukikosea kuupika mwanzoni haijalishi uongeze unga kiasi gani,

Shule ziwe zinaweka bidii kufundisha wanafunzi na kuhakikisha wanafunzi wanatia bidii huko chini, haya mambo ya kuwabakiza mashuleni wakati wa likizo yana msaada kidogo sana.

Nimesoma shule kama hizi, mtu kama hakuwa na msingi mzuri huko nyuma atafeli tu, kumbakiza likizo haimsaidii
 
Unawajua wanafunzi wewe😂 umpe homework for holidays alaa tuliowahi kupitia shule njooni tutoe ushahidi Yani ukae shuleni miezi 5 halafu upewe likizo aisee 😅

Any way it's better wakawapumzisha pia kuna muda akili inafika to the extent inagoma kabisa kwa kuconcetrate na kitu kimoja hasa masomo
 
Kwani Dkt. Kagasheki Msukuma yeye anasemaje?

Elimu
Elimu
Elimu

Ntarudi baadaye kuongeza nyama nyama kwenye maelezo.

Sasa hivi tuna-deal na bandari huku.
 
Kutokana na mwenendo wa shule hizi (msingi/sekondari) kwa miaka hii ya Sasa kutokufunga kabisa hasa kwa madarasa ya mitihani nashauri yafuatayo:

1. Badala ya kukaa na watoto kwa kipindi cha mwaka mzima bila likizo ya kurudi makwao basi wawape watoto kazi za nyumban kipindi cha likizo (home parkage) ambazo zikachukua maeneo yote muhimu ya kusoma.

2. Wafanye tafiti kutafuta ulinganifu wa ufaulu wa watoto kipindi ambacho shule zilifungwa kweli kweli na kipindi hiki ambacho ratiba inaonyesha kufungwa kwa shule lakini bado watoto wanaonekana mashuleni. Na Matokeo ya tafiti yawekwe wazi kwa watoto.

3. Nawapa hongera Walimu kwa kazi nzuri, HONGERENI WALIMU POPOTE MLIPO KWA KUJITUMA.
Barua ya serikali na maelekezo kukataza masomo wakati wa likizo yalipuuzwa ????
 
Back
Top Bottom