Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Mimi nawashangaa wale wote wanaoziponda kura nyingi anazopata Dr Slaa katika kura za maoni kupitia mitandao mfano Daily News, Mwanahalisi na hata humu JF. Jibu ni rahisi shule.
Wanaompa Dr Slaa kura hizo ni watu ambao angalau wamekwenda shule, wanaweza kuchambua mambo wao wenyewe bila kuburuzwa na wanaweza kutumia Internet. Hawa ni watu ambao tunaweza kusema linaanza kuliimarisha lile tabaka la jamii la Kati (middle Class) la wasomi, wenye kipato cha wastani, na ni tabaka ambalo hupiga kura kutokana na maamuzi ya vichwa vyao, na si miyoyo yao (voting from the head and not from the heart).
Watanzania wengi bado ni mambumbumbu watu wa kuburuzwa tu na ukichanganya na umasikini wao, basi hufanywa kuwa vuno kubwa la CCM wakati wa uchaguzi.
Wewe angalia tu maeneo ambayo tabaka hili linapatikana na uone nguvu ya Dr Slaa huko: Kilimanjaro, Arusha, Kagera Dsm, na maeneo ya ukanda wa ziwa.
Kwingineko ni uburuzaji tu fulana, T-Shirt, Sh elfu tano tano etc ndiyo hufanya kazi zaidi kuliko proper reasoning ya kutoka vichwani.
CCM inaliogopa sana taabaka hili, kwani likizidi kukua litaitokomeza CCM na hivyo uburuzaji wa watu kama makondoo utakwisha.