Boda boda msomi
Member
- Oct 7, 2024
- 18
- 23
Habari za muda huu watanzania wenzangu.
Kuna jambo ambalo kiukweli halipo sawa ukilinganisha umri tulionao kama nchi kutokea tupate uhuru kutoka kwa mkoloni mpaka sasa.
Leo nataka nizungumzie suala la uchakavu, ufinyu au hata kukosekana kwa baadhi ya miundombinu muhimu hasa kwenye baadhi ya shule za kata.
Nitatolea shule ya msingi Keko Mwanga iliyopo kata ya Keko, Manispaa ya Temeke kama mfano kwa sababu nilifanikiwa kuitembelea kwa nyakati tofauti na ni moja ya shule za hapa mjini.
Shule ile pamoja na nyingine nyingi hazina madawati, madarasa yake sakafu imeharibika utafikiri sio shule inayotakiwa kuwaandaa wasomi na watanzania wa kizazi kijacho.
Pia, shule nyingi hasa za kata hazina waalimu wa kutosha ni kama zimesahaulika.
Je, ni kwamba zimesahaulika, au hakuna fedha za kuweka miundombinu rafiki kwenye shule za kata?
Kwa akili ya kawaida observation yangu nimeifanya mjini najiuliza vipi huko vijijini hali itakuwaje?
Nawaomba viongozi wa serikali mzikumbuke shule hizi za kata.