Shule ya awali na msingi inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora yaungua moto

Shule ya awali na msingi inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora yaungua moto

Zinajengwa kienyeji sana bila kutumia wataalam wa ujenzi
Tizama maoni ya ukurasa wa kwanza utagundua ni kwanini Tanzania ni miongoni mwa nchi za ajabu sana duniani.
 
Zinajengwa kienyeji sana bila kutumia wataalam wa ujenzi
Siyo sababu ya kujitosheleza, kuzifanye nyingi ziungue ndani ya mwaka mmoja, zikiwa katika mikoa tofauti...

Kwann zisiungue shule zetu zenye miaka 55, na nyaya zinaning'inia kila kona, majiko ya kuni e.t.c.

Binafsi nahisi, kuna kikundi cha watu, wanaofaidika na hii misaada ya kitaasisi, nafikiri wanatafuta mbinu ya kupata pesa, haiwezekani shule zaidi ya 3 ziungue ndani ya mwaka mmoja.

Wanatafuta ufadhili na pesa kwa nguvu, wabinafsi, hawajali maisha ya watoto wetu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Isije ikawa kuna Boko Haram ya Bongo isiyoamini mfumo wa kupata Elimu Dunia kwa watoto wa Kiislam! Ni vyema mamlaka husika zikaacha kufanya kazi kwa mazoea.

Waingie kazini kufanya uchunguzi wa kina na matokeo ya huo uchunguzi yawekwe hadharani ili Wananchi wote tujue chanzo cha hayo yote. Kuendelea kushuhudia vifo vya watoto wetu na uharibifu mkubwa wa mali, ni jambo lisilo vumilika hata kidogo.
 
WAZAZI MLIO NA WATOTO KTK SHULE ZA KIISLAM, ONDOENI WATOTO WENU HUKO KWA USALAMA WA WATOTO WENU! HII PIA ITASAIDIA KUPELEKA UJUMBE KWA WAHUSIKA WACHUKUE HATUA STAHIKI..! SI SHWARI TENA KTK SHULE HIZO..HATUKO TAYARI TENA KUSHUHUDIA VIFO VYA UCHUNGU KAMA VILE VYA WATOTO KUMI WASIO NA HATIA HUKO KAGERA.
 
Siyo sababu ya kujitosheleza, kuzifanye nyingi ziungue ndani ya mwaka mmoja, zikiwa katika mikoa tofauti...

Kwann zisiungue shule zetu zenye miaka 55, na nyaya zinaning'inia kila kona, majiko ya kuni e.t.c.

Binafsi nahisi, kuna kikundi cha watu, wanaofaidika na hii misaada ya kitaasisi, nafikiri wanatafuta mbinu ya kupata pesa, haiwezekani shule zaidi ya 3 ziungue ndani ya mwaka mmoja.

Wanatafuta ufadhili na pesa kwa nguvu, wabinafsi, hawajali maisha ya watoto wetu.

Everyday is Saturday............................... 😎
Tupe uhusiano wa hizo shule zote zilizoungua nje ya kiimani ukiukosa uhusiano wao, ni kheri ukanyamaza mkuu.
 
hili jambo lisifumbiwe macho.....kwa nini linaendelea?! kuna nini?! kwa nini?!
jeshi la polisi tafadhali sana toeni majibu haraka na kwa wakati. kwa mtiririko huu wa haya matukio ya kuungua moto si ishara nzuri kabisa .....uchunguzi ufanywe kwa haraka na taarifa itolewe, lkn pia kuna haja ya viongozi wa shule kuchukua tahadhari, wekeni ulinzi wa kutosha kwenye shule zenu

kama ni uchakavu wa miundobinu ya umeme tufahamishwe. au kama kuna uhalifu pia itolewe taarifa
Mkuu ukishafahamishwa kuna lolote utachangia?
Vipi ukijua kwamba shule nyingi za kiislamu zinajengwa kwa donation za ndani ya misikiti ambazo hazikidhi kabisa kuajiri wakandarasi wa ujenzi na umeme?
 
Tupe uhusiano wa hizo shule zote zilizoungua nje ya kiimani ukiukosa uhusiano wao, ni kheri ukanyamaza mkuu.
Mkuu inaonekana unajua nini kipo nyuma ya pazia weka ukijuacho jukwaani, watu waelewe.

Mada imesema shule ya KIISLAM, uelewe wangu mdogo hii ni shule ya 4 nafikiri ndani ya 2020. Unataka niunganishe na shule zipi kwa kipimo kipi??

Una jambo unalolijua shea, mie nimeshea fikira zangu binafsi, hili jukwaa huru..
Sipangiwi cha kuongea maadam sijatusi.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Katika kila shule lazima awepo mwana usalama ila naona mnatutafuta ila sisi waislam tumetulia hatutaki Shari na MTU
Tunajua malengo yenu mtu gombanishe ili mukamate waislam ugomvi wetu kwenu mtaji hatugombani kama mmeshindwa kuchunguza tupeni wenyewe tuchunguze
 
Nashauri shule zote za dini hasa bweli zilindwe na polisi
 
Shule ya awali na msingi inayomilikiwa na Taasisi ya Kiislam ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora imeungua kwa moto usiku wa kuamkia leo Septemba 27. Hakuna madhara yoyote kwa binadamu yaliyotokea kwa tukio hilo.

=====

Shule ya Awali na Msingi ya Taasisi ya Kiislamu ya Istiqaama iliyopo mkoani Tabora imeungua moto usiku wa kuamkia leo na kuteketeza baadhi ya vitu vya wanafunzi katika bweni moja.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa amethibitisha kutokea kwa tukio la kuungua kwa moto kwa shule ya msingi.

Akizungumza na EATV / Radio Digital hii leo Septemba 27, 2020 Kamanda Mwakalukwa amesema kuwa moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.

''Ni kweli shule imeungua moto, hakuna madhara yoyote kwa binadamu lakini kuna bweni moja ambalo walikuwa wanakaa wasichana 45 vitu vyao vimeungua moto,” amesema RPC Mwakalukwa

Aidha Kamanda Mwakalukwa amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo.

View attachment 1582350View attachment 1582351View attachment 1582352

Hawa wenye siasa za matukio Chadema waangaliwe kwa jicho la pili katika haya matukio ya moto. Ikiwa walichoma ofisi yao kule Arusha, watashindwa kuchoma taasisi zingine ili kuleta taharuki na chuki kwa nchi na waislam

Hawa hawafai kabisa
 
Pole mzee
 
Mkuu ukishafahamishwa kuna lolote utachangia?
Vipi ukijua kwamba shule nyingi za kiislamu zinajengwa kwa donation za ndani ya misikiti ambazo hazikidhi kabisa kuajiri wakandarasi wa ujenzi na umeme?
Mkuu mwanzoni nilivyoyasoma majibu yako nikajua tuko pamoja unatumia kichwa ku think ila sasa nimeelewa kuna waya unatoka moja kwa moja kutoka kwenye Medula oblongata hadi kwenye WOWOWO lako

Hongera sana kiongozi wangu hayo nayo ni mapinduzi
 
Binafsi naamini ni hila za mabeberu na si kwa shule za kiislam tu wanaweza pia kufanya hivyo mahospitalini makanisani au popote

Mfano huko uarabuni wanalipua misikiti

Ila naamin serikali yetu sikivu ipo kazini
 
Huu ni mwendelezo wenye kutia mashaka sana.
Yaani kuanzia mwezi April mpaka September kuna zaidi ya shule tano za kiislamu zimeteketea kwa moto. Binafsi ninaamini haya sio matukio ya bahati mbaya (Accident) huenda ni matukio ya kupangwa!

Embu waza tu.
1. Ni matukio ya mfululizo.
2. Ni shule za kiislamu tu.
3. Hakuna uchunguzi wowote wa kina.
4. Hakuna ripoti yoyote kuhusu chanzo.
5. Hakuna wahusika waliochukuliwa hatua.
 
Siyo sababu ya kujitosheleza, kuzifanye nyingi ziungue ndani ya mwaka mmoja, zikiwa katika mikoa tofauti...

Kwann zisiungue shule zetu zenye miaka 55, na nyaya zinaning'inia kila kona, majiko ya kuni e.t.c.

Binafsi nahisi, kuna kikundi cha watu, wanaofaidika na hii misaada ya kitaasisi, nafikiri wanatafuta mbinu ya kupata pesa, haiwezekani shule zaidi ya 3 ziungue ndani ya mwaka mmoja.

Wanatafuta ufadhili na pesa kwa nguvu, wabinafsi, hawajali maisha ya watoto wetu.

Everyday is Saturday............................... 😎
Inawezekana pia Wachomaji wa Hizi Shule wanatoka nje ya dini husika
 
Back
Top Bottom