Ikiwa leo ni maadhimisho ya miaka 59 muungano wa Tanganyika na Zanzibar, tunatambua kazi kubwa inayofanywa na viongozi wetu Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu na Rais Dkt. Hussein Mwinyi katika kuleta maendeleo ya Tanzania.
Tanzania ilipata mkopo wa ahueni ya UVIKO-19 na maelekezo ya Rais Samia ni pesa hizi ziende kuboresha sekta za elimu, afya na maji. Katika mgawanyo wa pesa hizo serikali ya Zanzibar ilipatiwa Shs. Bilioni 231.0 ambazo zilienda kubadilisha sekta hizo.
Miongoni mwa shule zilizojengwa kupitia pesa hizo ni skuli ya msingi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imejengwa kisasa lakini kwa kuzingatia wanafunzi wenye mahitaji maalum.