Travis_Kitengo
JF-Expert Member
- May 19, 2021
- 329
- 919
Wakuu, nilikuwa sehemu nikakuta wazazi wanalalamika kuwa wamepeleka watoto shule ya English medium Mlowo iliyopo Mbozi mkoa wa Songwe ambayo inapokea wanafunzi wa day na boarding.
Sasa muda wa likizo uongozi wa shule umedai wanafunzi wa darasa la nne hakuna kufunga wataendelea na masomo kuanzia asubuhi hadi saa nne usiku kwa malipo ya ziada Tshs. 50,000/=!
Huu ni utesaji wa watoto hawa watoto watapumzika muda gani? Serikali iangalia hizi shule za English medium wasigeuza wazazi vitega uchumi.
Naomba Afisa elimu mkoa wa Songwe akawasaidie hao watoto wana haki ya kupumzika darasa la nne hakuna mtihani mgumu wa kufanya mtoto ashindwe kwenda likizo.

Hiyo shule ipo Mlowo jirani na daraja la treni uelekeo wa kwenda Isansa!