DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Habari Watanzania,

Nawasalimu kwa jina la muungano..

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano Walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kukataa kumpokea Mtoto ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na Mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kapangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma, Mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea Mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara

Sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo, wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti.

Naomba kuwasilisha

🤝
Si una bando la kushitaki? Basi tafuta na bando la kusajili mwanao

Jokes aside… cheza na mamlaka za wilaya ili wakusaidie. Pia husisha ndugu mmalize hizo requirements
 
Ukiona elim ghali jaribu ujinga..ss hyo hla ya bundle c ungelipia vifaa?! Acha kupenda dezo
 
Back
Top Bottom