DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

DOKEZO Shule ya Kibaigwa Girls imekataa kumpokea Mtoto wangu sababu sijamaliza Hela za Michango

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sasa wewe mpumbavu mwanao unampelekaje shule bila vitabu si bora abaki nyumbani tu,seems hata nursery hujawahi kupeleka mtoto
Mada inasema amekataliwa kupokelewa kwa sababu kuna vifaa hana, hakuna shule inayokataa kumpokea mwanafunzi sababu hana kitabu
Inaonuesha hujawahi hata kwenda shule, tuliosoma tunajua vitabu sio lazima kwenda navyo mara ya kwanza unavyoripoti, unaweza kutumia vitabu vya shule, au ukaazima vya wanafunzi wenzako...mada za shule achia walioenda shule wajadili
 
Wanataka vya Bure na Kodi hawalipi,iwe Ili vya Bure lipeni Kodi harafu Serikali itenge Bajeti za kuendeshea shule Ili zinunue hayo mahitaji.

Haya majamaa ndio yanadanganywa na Machadema huko yanajua labda siku Chadema ikishika Dola kutakuwa na Bure 😁😁
Ni wajinga sana
 
Ili elimu yetu ikue yatakiwa watu wachangie
 
Jitahidi ulipe na umalizie michango ndugu mzazi. Hivyo vifaa ni muhimu sana kwa mwanao kujifunzia awapo shuleni... Mfano ndoo atatumia kuogea na kufulia nguo zake....
 
Habari Watanzania,

Nawasalimu kwa jina la muungano..

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano Walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kukataa kumpokea Mtoto ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na Mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kapangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma, Mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea Mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara

Sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo, wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti.

Naomba kuwasilisha

🤝
Nenda kwa afisa elimu sekondari.akigoma nenda kwa mkurugenzi.akichomoa ita MAGAZETI andika habari.
Utakuja kunishukuru
 
Sasa bila vifaa vya usafi ; usafi utafanyikaje - au ndio kesho tuanze kulika watoto wameugua sababu ya usafi kutofanyika ?

Sipo hapa kunyosheana vidole (ingawa navinyoosha kwa serikali) kwa kuleta Siasa kwenye mambo muhimu; ijulikane moja kwa moja nini kifanyike na kinafanyika vipi; na haya mambo ya kudanganyana Elimu Bure wakati wanajifanya kusaidia huku kwenye pesa ndogo alafu Chuo mamilioni ya Pesa ambayo ni mkopo na mtu hapewi mkopo ni kuleteana Usanii kwenye mambo ya msingi...
 
Nenda kwa afisa elimu sekondari.akigoma nenda kwa mkurugenzi.akichomoa ita MAGAZETI andika habari.
Utakuja kunishukuru
Ushauri bure kabisa,Sasa afisa elimu ndio atampa ndoo ya kuogea na kufulia mtoto,?afisa elimu ndio anataka watoto wakae maeneo machafu bila kufagia?anunue tu mfagio na ndoo ampe mtoto
 
Habari Watanzania,

Nawasalimu kwa jina la muungano..

Nina kero yangu haswa kwa shule za advance wanaopokea kidato cha tano Walimu wakuu wanachukua maamuzi ya kukataa kumpokea Mtoto ikiwa tu hajamaliza michango na vifaa vingine kama vile vya usafi ukiangalia umbali uliotoka na Mtoto ni mbali sana.

Mfano mimi mwanangu kapangiwa Kibaigwa Girls iliyopo Dodoma, Mwalimu mkuu na makamo Mkuu wa shule wamenigomea kumpokea Mtoto kisa nimelipia nusu ya pesa za michango na sijakamilisha vifaa vya usafi ukizingatia nimetokea mkoa wa Mtwara

Sijui cha kufanya, naomba waziri husika kufuatilia hili jambo, wazazi tunashindwa kuwapeleka shule mapema watoto kutokana na hizi changamoti.

Naomba kuwasilisha

🤝
Hizo sio shida zetu.
 
Kila mtu humu matawi, mi na mleta Uzi masikini, pole mleta mada masikini mwenzangu, kwa kushindwa michango ya shule.
 
Tafuta hela,uache kulia lia mitandaoni.
 
Mada inasema amekataliwa kupokelewa kwa sababu kuna vifaa hana, hakuna shule inayokataa kumpokea mwanafunzi sababu hana kitabu
Inaonuesha hujawahi hata kwenda shule, tuliosoma tunajua vitabu sio lazima kwenda navyo mara ya kwanza unavyoripoti, unaweza kutumia vitabu vya shule, au ukaazima vya wanafunzi wenzako...mada za shule achia walioenda shule wajadili
Itakua umri umeenda sana mkuu kipindi iko shule zenu zina maktaba,eti usome vitabu vya shule kipindi hiki,by the way hongera kwa kwenda shule mkuu
 
Kama vipi Mleta mada sema usaidiwe binti yako asome otherwise mtafutie mchumba/mume mdaidiane kumsomesha binti yako.
 
Back
Top Bottom