Shule hiyo yenye Wanafunzi wapatao 900 ina madawati yasiyozidi 60, inapofika nyakati za Mitihani, Wanafunzi hulazimika kutembea umbali usiopungua Kilomita 3 kufuata madawati yanayoazimwa kwenye shule ya sekondari ya kata hiyo.
Wakimaliza mitihani huyarudisha baada ya kumaliza mitihani.
Hiki kinachoendelea naona sio salama kwa hawa Wanafunzi, Wizara ya Elimu na TAMISEMI waje waone Watoto wetu wanavyoteseka.