DOKEZO Shule ya Msingi Irunda (Sengerema - Mwanza) ina Wanafunzi 900 ila madawati yapo 60

DOKEZO Shule ya Msingi Irunda (Sengerema - Mwanza) ina Wanafunzi 900 ila madawati yapo 60

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mbunge wa huko si yule jamaa alitangaza demu wake ni marehemu atalea Watoto wa marehem
 
Mwendazake alisema wazae elimu ni bure hata kama wakikaa chini
 
Waende pale Wilaya ya Rombo Mkuu wakachukue madawati,kuna shule zimebaki na wanafunzi mpaka 30
 
Shule ina wanafunzi 900, walimu 9,ama kweli tembea uone. Ni kwamba shule ziko chache au watu wanazaliana sana?
 
Waende pale Wilaya ya Rombo Mkuu wakachukue madawati,kuna shule zimebaki na wanafunzi mpaka 30
Sio Rombo ,hata upareni shule lina darasa lina wanafunzi 15, wakizidi sana ni 45. Madawati ya kutosha. Unaweza ukawa na dawati lako mwenyewe. Iko hivyo toka zamani. Sisi darasani kwatu tulikuwa 30, madawati mengine yalikuwa yanapangwa huko nyuma maana ni mengi kuliko wanafunzi
 
Kwa hiyo wameshindwa hata kujichangisha
Mbona Kili huko walijenga mpaka barabara wao wenyewe?
Ukisubiri hawa mafisi utakufa
 
Hapana, kwa hili nakuwa na mtazamo wa tofauti wakuu.
01.Hiyo shule imeanzishwa tangu lini?

02. Kuna jitihada gani zimechukuliwa na jamii husika juu ya kupunguza uhaba wa madawati shuleni hapo?

03. Serikali ya mtaa imeshirikishwaje na imefanya nini kUtatua tatizo?

04. Ni upi mtazamo wa kielimu wa hiyo jamii tukirejerea na hali iliyopo?

Pengine, wenye shule wameridhia hilo. Sisi wengine wa mbali tufanye nini sasa!
Kama suala ni lako na unaweza kulifanya pana haja gani ya kusubiri msaada wa mbali?(hata kama msaada ni halali yako).

Hivi sisi watanzania tuna shida gani sana kiasi cha kuwa wategemezi namna hii?

Siku nikiwa na wa ng'ambo ile nitakuwa na ujasiri kweli wa kuiongelea Tanzania yangu?

Nevertheless, the villest situation can't ruin the place amenities.
 
Walimu mnalalamika nini wakati nyie ndiyo mmatuletea haya matatizo,
Waaambie hao watoto wake 15 kwenye kila dawati.
 
Back
Top Bottom