Shule ya msingi Mseta ipangiwe matumizi mengine baada ya kufungwa tokea mwaka 2012 kwa kukosa wanafunzi

Shule ya msingi Mseta ipangiwe matumizi mengine baada ya kufungwa tokea mwaka 2012 kwa kukosa wanafunzi

Ludomkenda_Tz

New Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
1
Reaction score
1
Shule ya Msingi Mseta iliyopo wilaya ya Rombo Kata ya Kirwa Keni Kijiji cha Kirwa Imefungwa toka mwaka 2012 kwa kukosa wanafunzi, Shule hii ipo katika Mazingira mazuri na ina majengo ya fedha za Serikali mazuri na yanayofaa kutumika. Mimi kama mdau nimeona kama Shule ilifungwa kwa tatizo la kukosa wanafunzi ni kwanini majengo hayo yasitumike kwa mambo mengine yanayoendana na mahali hapo?

Tumewahi kupendekeza kuwa majengo hayo wataalamu waangalie ikiwezekana pafungulie Chuo cha Wanyamapori kwani eneo hilo ni zuri na lipo karibu na Msitu wa Mseta, kufanya hivyo itasaidia sana kukuza na kuendeleza maeneo hayo na maeneo mengine ya Rombo kwani Rombo inakabiliwa na changamoto kubwa kwa Shule nyingi kuingia kwenye hatari ya kukosa wanafunzi.

Asantee

Naomba mtusaidie kupaza sauti
 
Rombo wanaume pulling imekufa mpaka kina mama wanavuka boda kwenda kushusha uzito
 
Boss kudos kwa wazo zuri. Unaonaje ukiweka historia ya shule ili tufahamu kisa cha kujengwa hapo hali ya kuwa hakuna wakazi?

Majengo yakikaa bila matumizi ni hasara kwa Taifa.
 
Ina maana hakuna watu huko,waipwleke kigo.a waone ndani ya wiKi imejaa
 
Back
Top Bottom