Ludomkenda_Tz
New Member
- Jul 18, 2022
- 1
- 1
Shule ya Msingi Mseta iliyopo wilaya ya Rombo Kata ya Kirwa Keni Kijiji cha Kirwa Imefungwa toka mwaka 2012 kwa kukosa wanafunzi, Shule hii ipo katika Mazingira mazuri na ina majengo ya fedha za Serikali mazuri na yanayofaa kutumika. Mimi kama mdau nimeona kama Shule ilifungwa kwa tatizo la kukosa wanafunzi ni kwanini majengo hayo yasitumike kwa mambo mengine yanayoendana na mahali hapo?
Tumewahi kupendekeza kuwa majengo hayo wataalamu waangalie ikiwezekana pafungulie Chuo cha Wanyamapori kwani eneo hilo ni zuri na lipo karibu na Msitu wa Mseta, kufanya hivyo itasaidia sana kukuza na kuendeleza maeneo hayo na maeneo mengine ya Rombo kwani Rombo inakabiliwa na changamoto kubwa kwa Shule nyingi kuingia kwenye hatari ya kukosa wanafunzi.
Asantee
Naomba mtusaidie kupaza sauti