Shule ya Sekonari ACT Bunda Girls inavyopoteza muelekeo wake

Shule ya Sekonari ACT Bunda Girls inavyopoteza muelekeo wake

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2023
Posts
445
Reaction score
1,094
Ni shule ya wasichana iliyo katika halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.Inamilikiwa na kanisa la Anglican dayosisi ya Mara.

Taaluma katika shule hii ni ya wastani sana ukilinganisha na hadhi yenyewe ya "u private".

Kwa kifupi inazidiwa kiwango cha Taaluma na shule nyingi tu kata zilizo ndani ya halmashauri isipokuwa huwa inabebwa na idadi ndogo ya watahiniwa!

Binafsi naliona anguko kubwa sana la shule hii ndani ya miaka michache ijayo kama uendeshaji wa shule utaendelea kwa staili iliyopo.

Inavyoonekana shule haina kabisa vision wala mission za kuiongoza ila inategemea tu mtu fulani kesho atasema nini!

Walio na mawazo chanya hawana nguvu za kuwasilisha mawazo yao na kutokana na hofu huamua kukaa kimya ili wasije kupoteza ajira zao.

Matokeo yake sasa "dreva anayekabidhiwa gari kuliendesha ataliendesha kwa utashi wa mabosi na siyo kuzingatia taratibu na kanuni za usalama barabarani!

Naamini shule haiendeshwi kitaasisi bali Kwa utashi tu wa mtu mmoja

Ukweli shule hii inaenda kujichimbia kaburi la futi nyingi na itazifuata shule nyingine za private zilizokwishapotea kwenye ramani kama Elly's,Olympus na nui!Muda utaongea,sisi tutabaki mashahidi!

Siku za baadae nitakuja kuanika mengi ila kwa leo tarehe 28.11.2024 nimesikitika sana kuona shule ikifukuza wanafunzi wa kike takribani 16 wasishiriki mahafali huku wakiwa tayari wamechangia pesa za mahafali! Uko wapi utu? Shule Ina mwamvuli wa dini ila huruma zero!

Sababu kubwa eti hawajakamilisha ada kwa 100%. Mbona mliunda group la whatsap mkahamasisha wazazi wachange na baada ya wazazi kuchanga mmechukua pesa na kuwabadilishia gia angani kwa kuwafukuza watoto wao?

Watoto wamealika wageni kuhudhuria mahafali ghafla mnawafukuza!Ina make sense kweli? Mnajua mlivyowaathiri kisaikolojia hawa watoto?

Unamfukuzaje mtoto siku mbili kabla ya mahafali
Halafu mpaka walimu wanashangaa mtu kujiita askofu na hana hata chembe ya huruma tena Kwa watoto wa maskini ambao wengi ni under 18!Watoto wamezagaa mtaani Kwa uzembe tu wa mtu mmoja!

Ushauri wangu mzazi ukitaka kupeleka mtoto ACT Bunda girls secondary school tafakari kwa kina sana. Narudia tena tafakari kwa kina sana! Nionavyo siyo mahali stahiki kwa mwanafunzi kulelewa vizuri!

Nakala kwa waziri mheshimiwa Mb.Dr. Dorothy Gwajima,we ni mpambanaji sana,tusaidie kukemea huu uozo!
 
Back
Top Bottom