A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Mbezi ya Kimara nilihitimu Kidato cha Nne kwa kufanya mitihani ya PC (Private Candidate) Mwaka 2020, Kituo change cha Mitihani kilikuwa Shule ya Sekondari Vituka, ipo Wilaya ya Temeke Mtaa wa Buza.
Kutokana na changamoto za kimaisha nikachelewa kwenda kuchukua cheti cha kuhitimu, mimi na wenzangu kadhaa tukaenda hadi kwenye kituo hicho lakini tukazuiwa getini na kutakiwa kutoa Shilingi 30,000 ili tuweze kupata vyeti vyetu.
Tumeuliza wenzetu kadhaa nao wametuambia kuwa walipofika Shuleni hapo nao wakatakiwa kutoa hizo hela na bila hivyo haupati cheti.
Ukiuliza kiasi hicho cha fedha tunatakiwa kukitoa kwa sababu zipi, hawatoi majibu zaidi ya kusema tumechelewa kwenda kuchukua vyeti, hivyo wanatutoza hela na maelekezo hayo yanaolewa getini na Mlinzi.
Mlinzi anasema ampewa maelekezo hayo na Mwalimu ambaye ndiye anayehusika na utoaji vyeti.
Mlinzi wa Shule ya Vituka ambaye alisisitiza bila kutoa Sh 30,000 hatupati vyeti kama alivyoelekezwa.
Kuna mmoja ambaye tulifanya naye mitihani hapo alifika na mzazi wake ambaye ana nafasi fulani nadhani ni Afisa Elimu, alipewa bure bila kutozwa chochote.
Nimeenda kulalamika hadi katika ukurasa wa NECTA lakini sijapata mafanikio yoyote mpaka sasa wala kujibiwa chochote.
Kinachoniuma kwa sasa nimetoka Tarime, nimekuja Dar kwa ajili ya cheti changu lakini mpaka sasa wananizungusha.