Shule moja ya sekondari ya Suzhou nchini China ikiwa ni shule ya majaribio ya ujumuishaji wa elimu na mchezo wa mpira wa miguu, imeiga vilabu vya kulipwa vya mchezo wa soka kujenga chumba cha kubadilishia nguo, chumba cha mazoezi na maonyesho ya utamaduni wa mpira wa miguu ili kuweka mazingira ya utamaduni wa mchezo wa soka.