Shule za Afrika Kusini kuanza kufunza Kiswahili baada ya kuingia makubaliano na Kenya

Hakuna Kiswahili chenye wenyewe! Kiswahili kimetoka pwani ya Kenya kikaja Tanganyika na kutapakaa coastal areas zote mpaka zanzibar.

Wakati huo kukazuka lahaja za kila aina! Kimtang'ata, Kingazija, Kimakunduchi na nyingine nyingi! Wakoloni wa kijerumani wakafanya usanifishaji wa Kiswahili (standardization) tukapata sarufi moja ambayo iliandikwa katika vitabu na kamusi mbalimbali kwa ajili ya rejea.

Kiswahili sanifu kinarejelewa katika sarufi iliyosanifiwa, sio watu au nchi! Wacha nadharia za kubabaisha!
 
Mara hii umeshasahau. Hii ni elimu na si wasi wasi ulio mili kwake.

Nipo ...
"Tamko la sarufi" maana yake nini? Maana naona unang'aka tu bila mpango! Tamko??? Ndio nini?
 
Hii inatutia aibu na kutuchoma.. hongera kwenu.
Nyie swahili yenu mnajua ni mbovu.. ila nchini kwetu watendaji wengi nao hawajui kujiongeza. Unaweza kukuta hata ombi la haya lilipokelewa ila wakalikalia kimya na sasa watafukia kabisa.
 
"Tamko la sarufi" maana yake nini? Maana naona unang'aka tu bila mpango! Tamko??? Ndio nini?
Nani ameandika "Tamko la Sarufi" ?

Sasa unakataa Sarufi sio tamko ? Au umekariri matamko ya wana siasa ?

Tamko ni neno lenye asili ya kiarabu,lisomekalo "an-Natk" chenye kutamkwa au lenye kutamkwa yaani "Mantuuk"

Hivi "Sarufi" likitamkwa huitwa nini ?
 

Ila unajichanganya sana,sasa huko kiliko toka si ndio kwa wenyewe kikaja mpaka ruvuma kikaenda msumbiji,somalia mapaka mayote.

Sasa unapokataa Kiswahili hakina wenyewe wakati hapo umewataja wenyewe ? Unadhihirisha ujinga wako ulio chupa mipaka.
 
Ila unajichanganya sana,sasa huko kiliko toka si ndio kwa wenyewe kikaja mpaka ruvuma kikaenda msumbiji,somalia mapaka mayote.

Sasa unapokataa Kiswahili hakina wenyewe wakati hapo umewataja wenyewe ? Unadhihirisha ujinga wako ulio chupa mipaka.
Wewe ni JUHA! Ninakueleza kuhusu 'chimbuko' la Kiswahili, sio 'umiliki' wa Kiswahili!

Au unataka nianze kukudadavulia tofauti kati ya 'chimbuko' na 'umiliki' kama kinda la njiwa!?? Ebo!!!

Kiswahili kilichimbuka toka pwani ya Kenya (nadharia) kisha kikasambaa maeneo mengine, kwa hivyo, kikamilikiwa na wengi katika lahaja tofauti tofauti! Baadae kikasanifiwa tukapata Kiswahili kimoja kinyoofu ambacho kimerasimishwa katika vitabu vya marejeo!

Mmiliki wa sasa wa Kiswahili sanifu ni SARUFI, sio mkenya wala mtanzania!
 
Hebu nipe muhtasari acha mbwembwe maana hata sikuelewi! Nyoosha maelezo!
 
Utasikiwa " Niko kwa job nikitoka naii nitapita kukuja pita wewe twende kwa mama ngina "

Tangu lini watu wa korogocho wakajua kiswahili
Ukiwaambia watamke neno IBADA utasikia IMBANDA nyang'auz na kiswahili wapi na wapi!
 
Jimbo la kati----- central province
serikali ya ugatuzi -- county government
County kaunti ni utohozi
 
Jimbo la kati----- central province
serikali ya ugatuzi -- county government
County kaunti ni utohozi

Hawa kwao bado wanatumia katiba ya zamani ya mkoloni, walishindwa kutengeneza mpya kama tulivyofanya sisi.
Hivyo wao bado wanatumia mkoa, wilaya, jimbo, hawana gatuzi au kaunti, akiona hilo jina anapata maruerue.
 
MK254 una kiswahili kizuri kama cha mtanzania na nina uhakika mkubwa umejifunza kiswahili huku naomba usikane hilo

Kaka Mkwawe hamna Kiswahili cha Mtanzania, hii ni lugha asili ya watu wa Pwani zetu ambayo tuliipokea na kuifanya kuwa rasmi kwenye katiba zetu.
Kuna baadhi ya Wakenya na Watanzania waliokubali kuitumia ipasavyo na kwa ufasaha, japo kunao sugu ambao hawataki kujiboresha.
Kawaida yetu Wakenya huwa tunapambana kuongea lugha kadhaa, lakini Watanzania wengi asilimia kubwa wameganda kwenye Kiswahili hawataki kujiongeza, japo sio kosa maana masuala ya lugha ni maamuzi ya kila mmoja kwenye Uhuru wake, ila kinachosikitisha kwa Watanzania wengi ni kwamba, uandishi wao kwenye Kiswahili unatia huruma, nimefanya kazi na Wabongo ambapo kuna kipindi nilikua nawaomba waandike ripoti, sasa kwa vile kingereza hawakijui, nilikua nawaagiza waandike kwa Kiswahili mwenyewe nitatafsiri.
Usitake kuona upupu waliokua wanaandika, Kiswahili kibovu kupita maelezo.
Angalia hata humu JF, mtu anaandika ovyoo na ukimrekebisha anatokwa povu la kufa mtu.
 
Jimbo la kati----- central province
serikali ya ugatuzi -- county government
County kaunti ni utohozi
Mr @Janeroso Mzalendo, hiko kiswahili kiko katika kamusi gani ya Kiswahili sanifu inayotambuliwa na (BAKITA)?

Katika kiswahili chetu tuna maneno kama Hospital, Daktari, na Dereva. Haya maneno yametoholewa kutoka katika lugha ya kiingereza (English) na si kwamba hayana kiswahili chake la hasha! Yanacho.

Back in the word "COUNTY"
Tanzania na Zanzibar hakuna sehemu wala mtu yeyote anaetambua neno "COUNTY" kama kiswahili sanifu.

Tanzania tuna Majimbo ambayo ndio huzalisha wabunge wa JMT, You Kenyans mna "Mna maeneo Bunge" sasa sijui ndio nini 😏😏 neno kaunti halijawahi kutoholewa
 
Maeneo Bunge- Constituency
 

Nyie bado mnatumia katiba ya mkoloni ambayo inatambua wilaya na mikoa, sisi tuliandika katiba mpya na kubuni maeneo yanayoitwa gatuzi au kaunti.
 
Maeneo Bunge- Constituency
Ny'ie mnaleta utani kwenye lugha yetu.
What's "Eneo bunge"? Tanzania ukija ukauliza hii kitu you'll wonder my brother watu watakushangaa ndio nini?
Mnajaribu kufanya kama USA na UK kwamba American English got some difference na UK English.
(HATUTAKI KUONA HII KITU INATOKEA MTUACHIE KISWAHILI CHETU)
Kiswahili cha KE. .Kiswahili cha Tz
--------------------------- --------------------------
Maeneo bunge. Majimbo.
Mashambani. Vijijini.
Ako. Yuko/Wako.
Alfu mia moja. Laki moja.
County. Jimbo.
State. Nchi.
Tafadhalini sana waacheni watu wa Lamu na Mombasa tu ndio wazungumze kiswahili Wengineo Just continue speaking Queen Elizabeth language
 
Nyie bado mnatumia katiba ya mkoloni ambayo inatambua wilaya na mikoa, sisi tuliandika katiba mpya na kubuni maeneo yanayoitwa gatuzi au kaunti.
Kwanza kiongozi nakupa Heshima yako unajua mambo mengi ya Tanzania.

Katiba yetu ni kweli ni yakikoloni lakini tuliifanyia marekebisho 1977.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…