Shule za Afrika Kusini kuanza kufunza Kiswahili baada ya kuingia makubaliano na Kenya

Shule za Afrika Kusini kuanza kufunza Kiswahili baada ya kuingia makubaliano na Kenya

Kaka Mkwawe hamna Kiswahili cha Mtanzania, hii ni lugha asili ya watu wa Pwani zetu ambayo tuliipokea na kuifanya kuwa rasmi kwenye katiba zetu.
Kuna baadhi ya Wakenya na Watanzania waliokubali kuitumia ipasavyo na kwa ufasaha, japo kunao sugu ambao hawataki kujiboresha.
Kawaida yetu Wakenya huwa tunapambana kuongea lugha kadhaa, lakini Watanzania wengi asilimia kubwa wameganda kwenye Kiswahili hawataki kujiongeza, japo sio kosa maana masuala ya lugha ni maamuzi ya kila mmoja kwenye Uhuru wake, ila kinachosikitisha kwa Watanzania wengi ni kwamba, uandishi wao kwenye Kiswahili unatia huruma, nimefanya kazi na Wabongo ambapo kuna kipindi nilikua nawaomba waandike ripoti, sasa kwa vile kingereza hawakijui, nilikua nawaagiza waandike kwa Kiswahili mwenyewe nitatafsiri.
Usitake kuona upupu waliokua wanaandika, Kiswahili kibovu kupita maelezo.
Angalia hata humu JF, mtu anaandika ovyoo na ukimrekebisha anatokwa povu la kufa mtu.
ila wakenya wengi hukidharau kiswahili bwana na humuona mtu ni makini zaidi akiongea kiingereza lakini kwa watanzania kesi ni tofauti maana ukitaka mtanzania akudharau mcheke kwamba hajui kiingereza atakuina ni zwazwa wa dunia

Kwa kifupi makosa ya kiuandishi na utumiaji wa lugha yapo kila mahali iwe Kongo, kenya, Burundi, Tanzania, china hata Marekani si suala la utaifa
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Kwanza kiongozi nakupa Heshima yako unajua mambo mengi ya Tanzania.

Katiba yetu ni kweli ni yakikoloni lakini tuliifanyia marekebisho 1977.
Hahaha huyo anaipenda Tanzania ila hana namna na usikute anaishi na familia yake huku

Ukimfuatilia vizuri ana ustaarabu fulani wa kitanzania ambao wakenya wenzake wamekosa
 
Mr @Janeroso Mzalendo, hiko kiswahili kiko katika kamusi gani ya Kiswahili sanifu inayotambuliwa na (BAKITA)?
Katika kiswahili chetu tuna maneno kama Hospital, Daktari, na Dereva. Haya maneno yametoholewa kutoka katika lugha ya kiingereza (English) na si kwamba hayana kiswahili chake la hasha! Yanacho.
Back in the word "COUNTY"
Tanzania na Zanzibar hakuna sehemu wala mtu yeyote anaetambua neno "COUNTY" kama kiswahili sanifu.
Tanzania tuna Majimbo ambayo ndio huzalisha wabunge wa JMT, You Kenyans mna "Mna maeneo Bunge" sasa sijui ndio nini 😏😏 neno kaunti halijawahi kutoholewa
Kweli wewe ni DRIPboy. Mtu ambaye hajui kutofautisha jinsia kwa kuangalia majina ya watu ni juha kabisa.

Kwani hao bashite sijui bakita ndio wanamiliki kiswahili? Kwa taarifa yako, kuna wakenya wengi ambao wameandika vitabu vya kiswahili. Usidhani lugha inayozungumzw mtaani ndio inafundishwa shuleni.
K.m. mwanafunzi atasema 'iko wapi book yangu ' ' yule dem ni msupuu' ila ataandika kitu tofauti. Hakuna mwalimu yeyote was kiswahili Kenya ambaye anaweza vumilia kusahihisha insha ambayo imeandikwa kwa hiyo lugha.He/she will just cancel ❌ it na akuandikie MAKINIKIA KAZI YAKO
 
ila wakenya wengi hukidharau kiswahili bwana na humuona mtu ni makini zaidi akiongea kiingereza lakini kwa watanzania kesi ni tofauti maana ukitaka mtanzania akudharau mcheke kwamba hajui kiingereza atakuina ni zwazwa wa dunia

Kwa kifupi makosa ya kiuandishi na utumiaji wa lugha yapo kila mahali iwe Kongo, kenya, Burundi, Tanzania, china hata Marekani si suala la utaifa
Sababu za mtu kuonekana kuwa mwenye akili kila akizungumza kingereza ni ile kwamba watu wengi huwa makini sana wanapozungumza kwa Kingereza, yaani watu wengi huwa wanajishtukia sana wanapotumia Kingereza, ila kwa Kiswahili unatiririka maneno bila kuwa na wasiwasi hata ukiboronga.
 
Kwanza kiongozi nakupa Heshima yako unajua mambo mengi ya Tanzania.

Katiba yetu ni kweli ni yakikoloni lakini tuliifanyia marekebisho 1977.

Nimeishi na kufanya kazi Tanzania kwa miaka kadhaa, nimekatiza mikoa na wilaya nyingi sana zaidi ya wengi wenu, miradi yangu ilihusu kusafiri sana huko mikoani na Zanzibar.
Hilo la marekebisho kwenye katiba ya mkoloni ni kitu tulikua tunafanya sana, ila tukaamua kuipiga chini yote na kuandika mpya yetu wenyewe, tena iliandikwa na wazawa wataalam baada ya kuitembelea nchi yote wakikusanya maoni. Ni baada ya katiba mpya nchi yetu ilianza kukua kiuchumi kwa kasi na mambo mengi yameendelea.
Nakumbuka nilikua Tanzania wakati mlianza mchakato wa kutengeneza katiba mpya, jinsi suala la serikali tatu liliwapa tabu hadi Kikwete akaupiga chini mchakato wote, mzee wa watu Warioba alivyodhalilishwa na Makonda.
 
Sababu za mtu kuonekana kuwa mwenye akili kila akizungumza kingereza ni ile kwamba watu wengi huwa makini sana wanapozungumza kwa Kingereza, yaani watu wengi huwa wanajishtukia sana wanapotumia Kingereza, ila kwa Kiswahili unatiririka maneno bila kuwa na wasiwasi hata ukiboronga.
lakini kumbe ni ujinga tu kuona unakosea kiswahili halafu unatiririka tu
Ila huko wanakushangaa sana na kiswahili chako
 
lakini kumbe ni ujinga tu kuona unakosea kiswahili halafu unatiririka tu
Ila huko wanakushangaa sana na kiswahili chako

Mara nyingi watu hawakosoani wakiboronga Kiswahili, hata humu JF utakuta Mtanzania anaandika Kiswahili kibovu lakini hamna anayehoji, subiri aandike kwa Kingereza kibovu ndio uone atakavyojibiwa. Hili nililiona Bongo, kwamba mkiwa kikao ambapo Kingereza ndio kinatumika, watu wanaonekana kujali sana ufasaha wa lugha zaidi ya mantiki ya unachokisema, hivyo kikao watu wengi wanaogopa kuchangia, ila ukibadilisha na kuomba muendeshe kwa Kiswahili, aisei kila mtu anataka aseme na hakuna anayeonekana kujali ufasaha wa mwenzie.
Tatizo ni pale humo kwenye kikao kuna wageni kutoka Ulaya, hivyo mnalazimika kutumia Kingereza muda wote.
 
Unakwenda kwa kanisa leo..

Hicho ndio kiswahili mnaenda kuwafundisha wenzenu, hivi Wakenya mbona mna hivyo
 
Unakwenda kwa kanisa leo..

Hicho ndio kiswahili mnaenda kuwafundisha wenzenu, hivi Wakenya mbona mna hivyo

Rekebisha hapo nimeweka nyekundu, kajifunze ngeli, na viambishi viwakilishi vya nomino.
 
Bora wangekuja tu kuchukua walimu wetu ambao wengi wapo tu mtaani tangu awamu hii ya tano iingie madarakani. Kuwachukua walimu wa Kenya ndiyo muendelezo ule ule wa kuiharibu tu lugha yetu tarajiwa ya bara la Afrika!

Wakenya wanaharibu sana kiswahili! Misemo yao huwa haijulikani wanaitoa wapi! Mifano ni mingi! Kama nawaonea basi "wakuje hapa" wathibitishe.
 
Watanzania hadi leo viongozi wetu wa wizara ya elimu na mambo ya nje, hawajui Kuwa Kiswahili ni mtaji mkubwa na kunafursa nyingi kupitia lugha yetu, tunahitaji kuweka mkakati makini ili Kiswahili kituingizie pesa za kigeni, vijana wanasoma lugha lazima wawekewe mikakati.
 
awamu ya kisee...hii wao kazi yao ni kudeal na upinzani na kuwaibia korosho wa wakulima diplomasia ya kufatilia fursa kama hizi hakuna
 
Bora wangekuja tu kuchukua walimu wetu ambao wengi wapo tu mtaani tangu awamu hii ya tano iingie madarakani. Kuwachukua walimu wa Kenya ndiyo muendelezo ule ule wa kuiharibu tu lugha yetu tarajiwa ya bara la Afrika!

Wakenya wanaharibu sana kiswahili! Misemo yao huwa haijulikani wanaitoa wapi! Mifano ni mingi! Kama nawaonea basi "wakuje hapa" wathibitishe.
Fursa mbalimbali Duniani hutafutwa, na huwa zipo kwaajili ya watu werevu. Hazidondoki tu. Unaweza ukawa na bidhaa nzuri sana lakini ukikosa marketing strategies and skills, zitakuozea.

Sisi tumeamua kujifungia ndani, tutajuaje kuwa kuna fursa? Tupo kwenye laiti traki ya kuhakikisha tunajitenga na fursa za Dunia kwa kuwa sisi ni matajiri sana.
 
Kenya Kiswahili Chao kibovu sana mfano "wewe kunjanga haba kambula sijakunjanga gani.
Aki unamkuta bibi'ako ananzurura(zurura) na nyaya ako then unapata wako kwa...........[emoji13] [emoji13]

Anyways, hatuna namna. Ndo kama ivo washakula shavu.

Wacha wakawalishe kande tu huko bondeni. Hakuna namna!
 
Eti apart from Kenya, Tanzania and zanzibar........, amenikera sana huyo mwandishi inakuaje hajui zanzibar iko ndani ya Tanzania
 
Tukale korosho, tuongeze nguvu za kiume tuzaane kwa wingi kama Ntwara.
 
Back
Top Bottom