Mkwawe
JF-Expert Member
- Jun 10, 2016
- 3,132
- 5,508
ila wakenya wengi hukidharau kiswahili bwana na humuona mtu ni makini zaidi akiongea kiingereza lakini kwa watanzania kesi ni tofauti maana ukitaka mtanzania akudharau mcheke kwamba hajui kiingereza atakuina ni zwazwa wa duniaKaka Mkwawe hamna Kiswahili cha Mtanzania, hii ni lugha asili ya watu wa Pwani zetu ambayo tuliipokea na kuifanya kuwa rasmi kwenye katiba zetu.
Kuna baadhi ya Wakenya na Watanzania waliokubali kuitumia ipasavyo na kwa ufasaha, japo kunao sugu ambao hawataki kujiboresha.
Kawaida yetu Wakenya huwa tunapambana kuongea lugha kadhaa, lakini Watanzania wengi asilimia kubwa wameganda kwenye Kiswahili hawataki kujiongeza, japo sio kosa maana masuala ya lugha ni maamuzi ya kila mmoja kwenye Uhuru wake, ila kinachosikitisha kwa Watanzania wengi ni kwamba, uandishi wao kwenye Kiswahili unatia huruma, nimefanya kazi na Wabongo ambapo kuna kipindi nilikua nawaomba waandike ripoti, sasa kwa vile kingereza hawakijui, nilikua nawaagiza waandike kwa Kiswahili mwenyewe nitatafsiri.
Usitake kuona upupu waliokua wanaandika, Kiswahili kibovu kupita maelezo.
Angalia hata humu JF, mtu anaandika ovyoo na ukimrekebisha anatokwa povu la kufa mtu.
Kwa kifupi makosa ya kiuandishi na utumiaji wa lugha yapo kila mahali iwe Kongo, kenya, Burundi, Tanzania, china hata Marekani si suala la utaifa