GODZILLA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 5,909
- 10,542
Hakuna Kiswahili chenye wenyewe! Kiswahili kimetoka pwani ya Kenya kikaja Tanganyika na kutapakaa coastal areas zote mpaka zanzibar.Unajua kwamba Kiswahili kina wenyewe ?
Ufasaha kila mtu anaweza kuwa nao lakini sharti ajifunze kwa mtu anae jua Kiswahili hicho,na lazima arudi kwenye asili.
Unatakiwa kuelewa maneno. Kiswahili kina wenyewe ila kila mtu anaweza kuwa fasaha.
Umiliki wa lugha au kukataa umiliki wa lugha ni kuupinga ukweli na kuipinga misingi ya lugha. Ndio maana pakawa na waswahili kwa maana ya watu wa ukanda wa pwani lakini si kila aliyeko ukanda wa pwani ni Mswahili.
Wakati huo kukazuka lahaja za kila aina! Kimtang'ata, Kingazija, Kimakunduchi na nyingine nyingi! Wakoloni wa kijerumani wakafanya usanifishaji wa Kiswahili (standardization) tukapata sarufi moja ambayo iliandikwa katika vitabu na kamusi mbalimbali kwa ajili ya rejea.
Kiswahili sanifu kinarejelewa katika sarufi iliyosanifiwa, sio watu au nchi! Wacha nadharia za kubabaisha!