Shule za binafsi zifutwe

Shule za binafsi zifutwe

Je Watanzania, are we ready for mabadiliko katika sekta ya Elimu??? au bado tunataka tupotee zaidi kabla ya kuanza kuitafuta njia kwa gharama kubwa kuliko ilivyo sasa???

Nadhani tumeshapotea kiasi fulani na mabadiliko yanayoweza kuipa challenge sekta ya elimu ni kutumia ujanja wa ICT kutoa elimu, kwani hii fursa inaweza kuwa nafuu zaidi katika kutoa elimu bora, hapo kuwawezesha hata watoto wa familia zisizokuwa na uwezo zaidi kuifaidi elimu.
Kumbuka, vigezo vya bei mbaya katika ST Fulani ni kuwa, wanao walimu bora, mazingira bora na pengine kuwa na hii mpya ya ICT classes. Mkongo wa fibre umesha tandazwa nchini kwa hiyo iwe ndio njia mbadala ya kutoa elimu. Katika hili sidhani kama ishu ni nani wa kutoa elimu, serikali inao uwezo wa kutayarisha elimu kwa njia hii au tuitupie mguvu kazi ya open amrket kufanya kweli?...
 
Hoja hii ya kupendekeza shule binafsi zifutwe nimeiona kwa takriban juma moja sasa na nafikiri ni bora nikaijibu kwa kuzingatia uzalendo na mapenzi kwa nchi yangu ya Tanzania. Nina imani huyu mwandishi anahitaji tu kufahamishwa kwamba utafiti uliofanyika duniani kote kupitia watafiti maarufu wa elimu (Unaweza kupata walichoandika kwa kuandika majina yao kwenye google. Hawa ni Hanushek, Woessman, Patrinos, Psycharopolous na wengineo) unaonyesha kwamba nchi zote kumi na moja ambazo zinatoa elimu bora duniani zimeweza kufanya hivyo kwa kushirikisha sekta binafsi. Watafiti hawa wameonyesha kwamba hata kukua kwa nchi hizi kiuchumi licha ya kuwa na raslimali chache sana kulitokana na kuwekeza katika elimu. Kinyume chake, nchi kubwa kubwa kama Marekani ambazo hazishirikishi sana sekta binafsi haziko katika kumi bora licha ya kutumia fedha nyingi sana katika bajeti yake kugharamia elimu.
Kwa hivyo SWALA LA KUPENDEKEZA KUUA SHULE BINAFSI NI SWALA LA KUPENDEKEZA KUUA ELIMU NA HATIMAYE UCHUMI WA NCHI.
Baada ya maelezo hayo ya jumla, nitajibu kila hoja kama ilivyotolewa na kuonyesha kwamba huyu ndugu ameandika haya mambo aidha kwa kusukumwa na chuki zake kwa shule binafsi au kwa hasira tu za kibinadamu.
1. hawa jamaa wamegeuza elimu ya taifa hili kuwa ni biashara.... ada kubwa yaani wizi wa kuaminiwa
unamaanisha nini kusema “ada kubwa”. Kanuni inayotumika kukokotoa gharama ya mwanafunzi mmoja kwa mwaka ni hii:
Gharama za uendeshaji wa shule kwa mwaka gawanya kwa idadi ya wanafunzi
Gharama za uendeshaji kwa mwaka zinajumlisha mishahara, vifaa vya kufundishia (vitabu, vifaa vya maabara n.k.), utwala (afya, chakula, usafiri, umeme, maji n.k.)
Kwa kuzingatia kanuni hii, utafiti uliofanywa na benki ya dunia mwaka 2010 kwa kutumia mtafiti wake Steve Lee unaonyesha kwamba serikali inatumia US$ 2,000 au Tshs milioni tatu (3,000,000/=) kwa mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari ya kata wakati shule binafsi hutumia wastani wa Tshs milioni moja (1,000,000/=) tu. Ada ys shule binafsi inaonekana kubwa kwa sababu mzazi anachangia kwa asilimia 100% kupitia karo wakati serikalini mzazi anachangia kwa kiwango kisichozidi 3%
Maana ya utafiti huu ni kwamba, kama bajeti ya moja kwa moja ingepelekwa shule binafsi ina maana kwamba wangedahiliwa wanafunzi zaidi ya mara mbili.
2. Shule zibaki kuwa za mashirika ya dini, taasisi za umma na serikali tu.
Hii kauli pia siielewi maana karo za shule mashirika ya dini zina karo sawa na shule za binafsi au makampuni. Hebu linganisha karo ya kanisa ya St. Francis Mbeya (zaidi ya sh 1.5m) na karo ya shule ya mtu binafsi St. Matthew (1.4m).
Mfanyabiashara ni yupi hapo? Au unaona tu mtu binafsi hatakiwi kuwa na shule?
3. Hebu fikiria wizi wa mithani ni hizi english medium
Kati ya wanafunzi 9,000 waliofutiwa mtihani wa kumaliza elimu ya msingin mwaka 2011, zaidi ya asilimia 70 ni wa shule za serikali (angalia www.moe.go.tz/ taarifa matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2011. Usiangalie orodha ya majina. Angalia sehemu ya taarifa ndio utakuta asilimia ya wanafunzi waliofutiwa mitihani kwa aina ya shule)
4. elimu duni yaani watoto hawafundishwi kama ambavyo inatengazwa na kuonekana kwa TV, Je mtoto atapata elimu kwa lugha asiyoijua?? as lower as class 1 or 2 at 7&8yrs of age????
Lugha “asiyoijua” mtoto ni ipi? Ni lugha ipi anayoijua? Kisaikolojia, mtoto aliyetoka tumboni mwa mama yake hajui chochote zaidi ya kunyonya kwa mama yake na kulia tu. Akifika umri wa miaka miwili akili yake inakuwa ina upeo mkubwa sana wa kuelewa lugha (mimicry).
Shule binafsi zinachukulia ukweli huu kuanza kumfunda mtoto kuelewa lugha atakayoitumia hadi chuo kikuu. Shule hizi hazitaki kumbadilishia mtoto lugha anapohama kutoka ngazi moja ya elimu kwenda nyingine kwa sababu asilimia kubwa ya wanafunzi hushindwa na ndio sababu, katika shule za serikali, wanafunzi wanafaulu darasa la saba na hatimaye kuja kupata divisionzero form four
Kama sera ya elimu ya mwaka 1995 ingeruhusu wanafunzi kufundishwa kwa kutumia lugha ya Taifa (kiswahili kwa Tanzania) katika kiwango cha sekondari na vyuo vikuu kama inavyofanyika kwa Ulaya nzima (Isipokuwa Uingereza), basi shule zote binafsi zingefundisha kwa kiswahili kuanzia shule za msingi. Matumizi ya lugha ya Taifa ndio njia pekee ya kumwandaa mwanafunzi kuwa mbunifu wa teknolojia badala ya “ubunifu” wa usanii na mitindo ya mavazi ambayo ndio imeshamiri kwa sasa Tanzania.
Tunashukuru kwa sera mpya ambayo sasa inaruhusu shule za sekondari kufundisha kwa kutumia Kiswahili. Hii itafanya shule binafsi kuanza kufundisha kwa kutumia kiswahili
5. Elimu biashara inamchango mkubwa kwenye kufa kwa elimu TZ, eti mtu anafaulu hajui kusoma wala kuandika haya ni mambo ya elimu biashara.
Wanao”faulu” bila kujua kusoma na kuandika ni wale wa shule za serikali tu. Hebu kamuulize Mulugo na Kawambwa walitumia vigezo gani kuwatangaza kwamba wame”faulu”. Nadhani ulikuwa usingizini siku ile anatangaza kwamba HAKUNA MWANAFUNZI ALIYEDAHILIWA KATIKA SHULE BINAFSI AMBAYE AMEMALIZA DARASA LA SABA, KIDATO CHA NNE AU CHA SITA BILA KUJUA KUSOMA WALA KUANDIKA

Ndugu yangu: Ninajua kwamba unatamani sana kumleta mtoto wako katika shule binafsi na najua kwamba ungependa nchi hii ifunguliwe kutoka katika lindi la umaskini. Hatuwezi kufunguka bila kuwa watafiti wa kuelewa chimbuko la elimu bora na ukuaji wa uchumi. Hima anza leo kufanya utafiti na utaungana na mimi kusema kwamba “SEKTA BIANFSI NDIO CHOMBUKO LA ELIMU BORA NA UKUAJI WA UCHUMI”
 
Hivi ni kwanini watoto wa viongozi wa kitaifa wanasoma nje ya nchi???? suala ni lile lile kuwa ubora ktk elimu hapa hakuna na hivyo ili kuandaa matabaka ya watwana na watwaliwa lazima, wakubwa sio wale wa middle class, wasomesha kunako elimu bora.

Hapa hakuna elimu bora, ni bora elimu tena mbaya zaidi wizi wizi ndo umezunguka taaluma ya TZ, ni kama afya watasema kila neno eti muhimbili kuko safi, lakini je, mbona wakiugua wanaenda nje??? ukimwambia mkulima hali ya muhimbili anakwambia hajaona hospital nzuri kama ile na yuko tayari kufa kama hatapona muhimbili, hii haina maana muhimbili ni nzuri-hapana, ni ushamba wa huyu mkulima.

Vile vile shule za saints hapa tz sio nzuri kama unavyofikiria ndo maana vigogo wanasoma nje ya nchi; shule binafsi pesa kwanza taaluma baadae, shule binafsi kufaulu kwanza taaluma baadae; kama unaona huzo shule ndo kiboko ktk utoaji elimu bora ni ushamba wako tu. TUDAINI MAZINGIRA SAWA KWA KILA MTANZANIA, matabaka ni janga pia.
 
1. Ina maana hakuna profit component? Uongo huo, Pili iweje gharama ya kiserikali iwe 3mil kwa mwaka kwa mwanafunzi mmoja na gharama hiyo iwe 1mil kwa mwaka kwa shule binafsi??? Huu pia ni ushahidi kuwa kuna madingo yanafanyika huko shule binafsi kama hilo ni kweli, Zaidi kuna wakati rais aliwapiga mkwara upandishaji wao wa ada, ina maana yeye hajui kuwa kwa shule binafsi watz wanaserve pesa mara 3 ya zinazotakiwa kwa serikali??? Uongo mwingine umeleta.

2. Ninachosema mimi ni kile unacholipa na elimu unayopata, shule za dini ziko fair sana ktk kudeliver hakuna urafi wa mtu mmoja mmoja, dini ni umma na tofauti ya umma na mtu iko wazi. Sauti ya wengi ni ya Mungu. Huoni tofauti ya kulipa 1.5m ukapata unacholipia na kulipa 0.75m ukapata magumashi??? Huioni? elimu feki feki imelitesa taifa hili.

3 .Shule za binafsi wako smart sana katika kuiba maana imo ktk strategic objective yao, na wanatoa fedha nzuri hakuna mtu atawakamata. Wanaojaribu tu kuiba (out of curiosity kwa dhana kwamba mbona wengine wanaiba) bila kujipanga shule za serikali hizo ndo hukamatwa, believe me or not.


4. Kama tija ipo kwenye kufundisha kwa kiingereza kwanini serikali wanagoma kutumia kiingereza primary school?? Kimsingi tunaelekea kwenye kiswahili hadi chuo kikuu na sio kinyume chake maana tija iko huko, nchi zilizofanikiwa zimefundisha kwa lugha zao.

5. General fikiria elimu tuliyopata sisi miaka ya shule za serikali na dini au taasisi za umma na elimu ya leo; Hapo pia huoni tofauti??? Shule binafsi zimetuchanganyia sana mada, maana kuna wakati watu waliona ndo kimbilio baada ya kushindwa mfumo wa serikali lakni sasa ni zig zag ambayo lazima tuiondoe. Na serikali ifanye yale ya kiserikali ikiwemo kutoa elimu bora.
 
Sikubaliani na kufutwa kwa shule za binafsi hata kidogo, Serikali ijaribu kuwajali na kuwaheshimu Waalimu wa shule za Serikali, sio viongozi kuwagaia vimada wao fedha ya nchi na kuwaacha wawekezaji wafanye wanavyotaka na madini yetu, Serikali iwe makini katika ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali na kutumia kwa manufaa ya Wananchi wake na Taifa kwa ujumla sio kujijengea majumba kama mahekalu, wao, watoto wao na vimada wao, wawajali waalimu, madaktari na wafanyakazi wengine wa ofisi zao, unafikiri shule za binafsi zikifungwa mfumo mbovu katika elimu ndio utaisha kabisa, hao waalimu watakaotoka huko wanaweza kuamua kufanya shughuli nyingine, kama biashara, kufanya kazi kwenye mabenki au kwenda kufundisha kwenye shule nyingine nchi za jirani, na wazazi wenye uwezo kuwapeleka watoto wao wakasome nchi za jirani au Ulaya, cha msingi boresheni mazingira ya utoji elimu kwa ujumla na kuwajali Waalimu, ili wawe na moyo na ari ya kufundishwa kama taaluma yao inavyohitaji wafanye, msiwafanye wajute kuwa waalimu, waupuuze uwalimu na kufanya shughuli nyingine, hao wanaouza mitihani kwani hawajulikani miaka yote hii?!, wao na wizara yao wawajibishwe, kila mara wimbo ni huo huo, mbona hawatajwi ili wawajibishwe, wanaendelea kuachwa wakitajirika na biashara hii kwanini?!, who are they?!
 
Dah mkuu wewe si mdau wa sekta ya elimu maana ungekuwa mdau, usinge toa kauli hii. Hebu jaribu hii kwanza uone madhara yake KUFUTA HOSPITALI BINAFSI. Mzigo unaobebwa na shule binasfi ni mkubwa sana
 
Dah mkuu wewe si mdau wa sekta ya elimu maana ungekuwa mdau, usinge toa kauli hii. Hebu jaribu hii kwanza uone madhara yake KUFUTA HOSPITALI BINAFSI. Mzigo unaobebwa na shule binasfi ni mkubwa sana

Mimi nimeweka hoja zangu kwanini napendekeza zifutwe, unachonijibu wewe ni woga wa mabadiliko, the natural concept of the community to resist changes regardless of the level of education so attached to the community. ungejua kituko kilichopo hospital binafsi usingeandika tena hilo jambo hadi unakufa, do you know about 40% of all sickpeople attending this hospitals are killed due to poor management of the patients? in my family it has happened twice, with one incident involving me where i survived narrowly (sio dispensary ni hospitali ya hadhi ya mkoa, ukitoka pale ni rufaa tu). In summary ndo maana viongozi hawatibiwi hapa jamaani tuwaambieje muelewe watanzania maskini?????? Unadhani wanapenda kutumia ovyo fedha zao, umekosea wanafata matibabu ya uhakika. ukifika hospital ukiwa bado mzima lazim utabapata ahueni, kama sio terminal disease lazima upone, sio hapa hata kama ni ugonjwa wa kawaida unakufa na dktari hajibu kwa mtu yeyote; wanasaidia kuandika ripoti ya kumugandamiza marehemu full stop. Do you know about expired medicines, do you know about overdosage, do you know about wrong doses administered to patients, do you know about the concept of sell everything to patients, yaani unatakiwa kula dawa za minyoo, unapewa na za malaria ili ulipe zaidi; do yo know about vipimo feki, kwa sababu zifaa zimechakaa sana, hata darubini za malaria ni issue. mionzi mikali kuliko recommeded kutokana ka uchaavu wa vifaa, harafu wanajua ila pesa haiachwi.

Back kwenye suala la elimu, ninachosema mimi labda nimekiwahisha sana, lakni time will tell, unajua umaskini unaambatana na vitu vingi sana, mojawapo ni kutotaka kufikiri kwa kina zaidi ya vikwazo, mtu anayesema serikali haiwezi kutoa hizi huduma ni kwamba amepotea kabisaa, maana serikali sio kuchukua kodi zetu harafu kugawana posho na mishahara; no ni kutoa huduma na lazima watoe, kama watz hatupati ni vile hawa jamaa wanabank on ujinga wa watz. TUNAPASWA KUDAI hii HAKI YA ELIMU BORA kwa kila mtanzania anayehitaji. NA UHAKIKA MTU BINAFSI HAWEZI KUTOA ELIMU BORA HAPA TZ, anatafuta pesa sio elimu bora tofauti na mabepari kama huko ulaya wanaanzisha shule sometimes kwa lengo la kurejesha sehemu ya utajiri wao kwa jamii. Huku ni mtu anataka atajirikie hapo.
 
Elimu ni haki ya kila mtoto!
Watoto wote wanapaswa kupewa elimu ya kuwasaidia kujitegemea na kuchangia uchumi wa nchi.
Tatizo lililopo ni serikali kuacha mamlaka ya kusimamia elimu na kuruhusu wachache kuchukua nafasi hiyo kujinufaisha.
shule za serikali zimeachwa ili shule za binafsi zipate soko?
Kinachotakiwa:
Shule za serikali ziwepo na zitoe elimu inayostahili kumsaidia mtanzania.
Shule za binafsi ziwepo kwa wenye uwezo na ziendeshwe kibiashara. zilipe kodi kama biashara zingine!
Huku kujificha kwenye kivuli cha St. english medium wakati ada tunazotozwa ni za kibiashara ni kuliibia taifa kodi.

Suala la mzazi kumkazania mtoto ili afauli vizuri zaidi sio tatizo la kitaifa, hilo ni la mtu binafsi. Watoto wakifundishwa vizuri shuleni watajua kusoma na kuandika hata bila mzazi. Sasa wewe unayetaka mtoto wako afanye vizuri zaidi ndio ufanye juhudi binafsi.
kinachotakiwa ni hata yule mtoto ambaye wazazi wake hawakufanikiwa kupata elimu au hawapo nao wapate nafasi ya kusoma kwa vile nao ni watanzania na wana haki.
Tusisahau kuwa ni asilimia ndogo sana ya watanzania wana elimu zaidi ya sekondari.

Shule za binafsi zinalipa kodi kama kawaida nenda kaulize kwa kamishina wa kodi za ndani. Unaposema shule za serikali zimeachwa ili kunufaisha shule binafsi si sahihi kwa sababu shule zote za serikali zimejaa watoto mpaka wanakaa chini wakati shule binafsi vyumba vya madarasa havina wanafunzi.
 
Karibu nchi zote shule za binafsi zipo.. na zinajitahidi kufanya vizuri ili watoto wapate elimu bora..hebu chukua mfano wa Rocken Hill ya Kahama Shinyanga ... wako juu hawa wanafuata mtaala wa Tanzania.. chukua Savannah Plains ya Shinyanga hawa wanafuata mataala wa Kimataifa... wanafanya vizuri... Tanzania elimu yetu ni ngumu saana (Katika shule za serikali) .. anzia primary hadi sekondary mpaka vyuo... mie nimesoma kwa kupitia mfumo huo... siyo user friendly.. tena vyuoni ndiyo mbaya sana watu wanatungiwa mitihani migumu isiyoendana na mitaala yao ya masomo ili wafeli.. hii nchi tunaiua anzia katika mfumo wetu wa elimu.. ndiyo maana wenye pesa zao wanawapeleka watoto wao English Medium Schools au International schools!!
 
Karikenye umetaja baadhi tu ya matatizo ya mfumo wetu wa elimu, hebu chukulia wenye pesa wasingekuwa na pakupeleka watoto wao?? tungeungana kuihimiza serikali, kitu ambacho ndo sahihi, sasa divide and rule inatumika, pili matabaka yanajengwa mchana kweupe, tufanyeje??? TUFUTE SHULE ZA BINAFSI HARAFU TUONDESHE NA MATATIZO MENGINE MADOGO MADOGO.

Kwa nchi tajiri sawa maana hata wenyeshule ni matajiri wa ktupwa, wanarejesha tu kiasi fulani kwa jamii yao, KWETU NCHI MASKINI tunafanyakosa kubwa mno kila kitu kuiga, hakika tutapasuka msamba. Ukikaa kufikiria gtu kila jambo hakika hutatenda lolote la maana dunia, suala lilikuwa tumeona shubiri ya hizi shule piga chini tukutane na changamoto zingine sio hii ya shule binafsi elimu feki hela kubwa kisa kuiba mitihani ili watoto wafaulu. Hatutaki vyeti vyenye first class wakati mmliki hana uelewa wa kutosha. AIBU, sasa unafikiri kwa nini watz wanadhani kwaKE watuchukua ajira zao???
 
Nilipoweka mchango wangu mwaka jana May 2012, watu walikajeli. Chamsingi sasa tunatafuta mchawi, matokeo yanakuwa ya kupikwa kama samaki, Swali ni JE, bado tunataka kuona zaidi elimu ikiwa chini ya biashara au tunakubali sasa imetosha, elimu isifanyiwe biashara hata kidogo? shule binafsi ni kufaulu bila taaluma. sorry to be so open for you.
 
Back
Top Bottom