Shule za English medium za serikali

Shule za English medium za serikali

Changamoto za shule hizi ni kupata nafasi., zimetawaliwa na rushwa sana .
Pili zina wanafunzi wengi sana mtoto anatakiwa awe na uwezo wake tu maana walimu hawana uwezo wa kumudu kufundisha na kieleweka vizuri idadi kubwa ya wanafunzi
Tatu kwa dar shule hizi karibu zote zipo city centre , ili mwanao asome vizuri inabidi uwe unaishi ¹maeneo karibu na mjini la sivyo mtoto atataabika sana usafiri .
 
Kwa wenye kumbukumbu nzuri, mtakumbuka kipindi Rais akitanganza azimio la kuondoa ada kwa shule za msingi za umma. Rais alitaja shule sita kuwa shule hizi zitaendelea na utaratibu wa ada na kati ya shule zilizotajwa ni Bunge(Dar), Mlimani (Dar) na Olimpio (Dar).

Kwa utafiti wangu mdogo niligundua kuwa shule hizi wanafunzi wake wanajifunza (medium of instruction) kwa kutumia lugha ya Kingereza, yaani English medium.

Hoja yangu...

Kwanini serikali isianzishe shule za namna hii atleast shule 50 kila mkoa?

Mchakato wa kupata wanafunzi wa shule hizi ukoje, kwani niligundua kuna watoto wanatoka Madale kwenda Upanga, je mchakato ni wa wazi?

Ni watoto wa Watanzania wenye hadhi hudailiwaa pale na kiwango cha ada kikoje?

Naomba kuwasilisha.
Tanga mjini ziko mbili mwaka huu imeanza mpya ya tatu. Ada zinalipwa ila ni affordable
 
Nilisoma olympio kipindi hicho ada ili kuwa elf 50 tu ambayo elf 25 sikumbuki ilikuwa ya nini na elf 25 nyingine ndio ilikuwa ada, nilisoma na wahindi plus wazungu wa somali na nilikuwa natokea mbagala ila nimepita kipindi flani hapo nadhani 2022 kuna maswala flani nilikuwa nafuatilia nikauliza hivi bado Hawa ndugu zetu wahindi na wazungu wanasoma hapo jibu nililopata ni hapana kwa sasa ni ngozi nyeusi tu
 
Back
Top Bottom