SoC04 Shule za msingi za serikali zifundishe masomo yote kwa lugha ya kingereza ili kuwatengeneza watoto wanaojua kusoma na kuandika lugha hiyo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
1,012
Reaction score
2,317
Ni wazi unakubaliana na mimi kuwa kwa asilimia kubwa watoto wengi wanaosoma shule za English medium ni watoto wanaojua kusoma na kuandika lugha ya kingereza kuliko wale wanaosoma shule za msingi za serikali, kwa kweli watoto wanaosoma English medium ni watoto wanaojua sana kingereza hasa kwenye upande wa kusoma na kuandika kuliko wale wa shule za serikali.

Katika uhalisia mara nyingi watoto wanaosoma shule za msingi za serikali, kwa asilimia kubwa huwa hawajui kusoma wala kuandika lugha ya kingereza, huku baadhi yao unakuta wanajua baadhi ya maneno machache sana ya lugha hiyo tena kwa kukalili, ambapo ni tofauti na wale wanaosoma shule za English medium ambao wanajua lugha hiyo kupita kiasi. Hali hii kwa asilimia kubwa naweza kusema inachangiwa na aina ya ufundishaji uliopo katika shule hizo za serikali, ambapo kwa mara nyingi shule hizo zimekuwa zikifundisha lugha ya kiswahili katika masomo yote kasoro somo la kingereza tu, ambalo pia somo hilo hufundishwa kama kwa kugusia tu tena unakuta ni kwa mara chache sana katika shule hizo. Hali inayopelekea asilimia kubwa ya watoto wa shule hizo za msingi za serikali kutokujua kuandika wala kusoma lugha hiyo, kwasababu ya kufundishwa kwa uchache sana, tofauti na wale wa shule za English medium ambao masomo yote hufundishwa kwa kingereza hali inayopelekea kuizoea zaidi lugha hiyo na kuifahamu zaidi.

Unakuta watoto wa shule za English medium wanakuwa wapo vizuri kweli kwenye kusoma na kuandika kingereza, kwasababu shuleni kwao wanafundishwa kila kitu kwa kingereza, mfano kwenye upande wa uandishi kila somo wanaandika kwa kingereza, alafu kwenye upande wa kusoma pia wanasoma kwa kingereza hali inayopelekea kuizoea zaidi lugha hiyo na kuifahamu kwa undani kuliko wale wa shule za serikali ambao vitu vingi hufanyika kwa kiswahili, kama vile kusoma unakuta wanasoma kwa kiswahili na kwenye upande wa kuandika huwa ni kwa kiswahili, alafu kwenye upande wa somo la kingereza wenyewe wanakuwa wanagusia gusia tu, hali inayopelekea watoto hao kushindwa kuizoea na kuifahamu lugha hiyo ya kingereza kwa undani hasa kwenye upande wa kuandika na kuisoma kwasababu kila kitu wao unakuta ni kwa kiswahili.

Kwa kweli unajua lugha ya kingereza ni lugha pana sana na inahitaji ifundishwe kweli kweli ili iweze kueleweka, kwasababu lugha ni yenye maneno mengi, lakini kama ikifundishwa mara chache inakuwa ni ngumu sana kuifahamu. huwezi kuielewa lugha hiyo ya kingereza kwa miujiza ni lazima kuwe na ufundishaji wa hali ya juu wa lugha hiyo ndipo utaielewa, endapo kama itafundishwa kwa uchache basi matokeo yake yatakuwa hasi na kama ikifundishwa kwa ukubwa na undani zaidi basi ni lazima itaeleweka na matokeo yatakuwa chanya.

Naweza kusema watoto wengi wa shule za msingi za serikali wanakuwa hawanauwezo mzuri wa kusoma na kuandika kingereza, kwasababu kwanza ufundishaji wake wa lugha hiyo ni mdogo sana, yani unakuta wao aina ya ufundishaji uliopo kwenye shule hizo kila kitu ni kiswahili, mfano mtoto kuongea na mwalimu wake kila kitu anaongea kwa kiswahili, kwenye kuandika ni kiswahili na kwenye upande wa kusoma ni kiswahili alafu lugha ya kingereza unakuta inafundishwa kwa kugusiwa gusiwa tu kwa mara chache sana, kwa kweli ni mara chache hata kumkuta mwalimu wa shule hizo akiongea kwa kingereza na wanafunzi, yani wao kila kitu ni kiswahili na kama ukiwakuta wanaongea kingereza labda wakiwa kwenye somo la kingereza tu lakini nje ya hapo ni mwendo wa kiswahili. Sasa kwa hali hii ni lazima kunakuwa na uwezekano mkubwa wa watoto wa shule hizo wengi kutoijua lugha hiyo ya kingereza ukilinganisha na wale wa English medium.

Sasa hali hubadilika kabisa watoto hao wanapoingia elimu ya sekondari ambapo huko hukutana na hali ngumu kimasomo kutokana na lugha wanayoikuta huko ni tofauti na ile waliyoizoea wakiwa shule za msingi, lakini hii inakuwa ni tofauti na wale wengine waliomaliza English medium wao wanakuwa wanaona kuwa hali ya sekondari ni ya kawaida alafu unakuta wanafanya vizuri sana kwenye masomo yao. Lakini wale waliomaliza shule za msingi unakuta tatizo lao lipo kwenye lugha hali inayopelekea wafanye vibaya kwenye masomo hayo ya sekondari kwasababu lugha kwao ni changamoto sana na siyo kwamba hawana akili hapana ni kwasababu walikuwa wakifundishwa lugha hiyo kwa uchache sana. Yani wao kila kitu kwenye shule zao ni kufundishwa kwa lugha ya kiswahili.

Kwa kweli ufundishaji wa lugha ya kiswahili kwenye masomo ya shule za msingi za serikali kwa namna moja ua nyingine zinachangia watoto wanapoingia elimu za sekondari kufanya vibaya kwenye masomo kwasababu ya lugha, ukilinganisha na wale wa shule za English medium.

Mapendekezo
Kila mtu hapa anakubaliana na mimi kuwa ufundishaji wa English medium umekuwa ukiwaanda watoto wanaomaliza katika shule hizo kwaajili ya kukabiliana na elimu za juu hasa kwenye upande wa lugha ya kingereza, kuliko wale wa shule za msingi. Kwa mfano watoto hao kutoka kwenye shule tofauti wanapokutana kwenye elimu za sekondari, unakuta watoto wa English medium wanafanya vizuri kuliko wale wa shule za msingi kwenye upande wa lugha ya kingereza. kwahiyo ni wazi kwamba shule za English medium wanakuwa wanamuandaa mtoto kwaajili ya kukabiliana na elimu za juu, lakini kwa upande wa shule za serikali ni kama vile wanampoteza kabisa mtoto kwasababu kile wanachomfundisha siyo kile atakachokutana nacho sekondari, alafu mwisho wa siku tunakuwa tumetengeneza watoto wasiojua kusoma wala kuandika.

Nashauri katika masomo yote ya shule za msingi za serikali yafundishwe kwa lugha ya kingereza ili kuwatengeneza watoto wanaojua kusoma na kuandika lugha hiyo, ili hata watakapoingia kwenye elimu za sekondari wasipate shida, tunapaswa kurekebisha hapo kwasababu wote tunafahamu kuwa sekondari kwa asilimia kubwa inatumia lugha ya kingereza, hivyo kuna haja ya kuwaanda watoto wetu kwenye shule zetu za msingi kwaajili ya hilo. tusijekuwa tuna wafundisha watoto lugha ya kiswahili kwa asilimia kubwa, alafu tuje kutegemea labda watoto hao watakapo kutana na lugha ya kingereza kwenye elimu za sekondari kuwa labda kutatokea muujiza wakati kumbe haiko hivyo. Kwahiyo nashauri kwenye shule zote za msingi za serikali zifundishe masomo yote kwa lugha ya kingereza.

Hitimisho
Tanzania bora tuitakayo ni ile ambayo itakayokuwa na elimu bora yenye matokeo chanya, sio tunakuwa na elimu yenye matokeo hasi.
 
Upvote 28
Brother kingereza Ni lugha ya Dola zenye nguvu duniani kiuchumi na kijeshi na kila kitu kwa Kizazi hiki hivyo inalazimika kwa kila mtu kukifaham ili anufaike na utajiri huo. Lugha haipendwi au kuenea kibahati mbaya lazima Kuna msukumo. Hata kiswahili kilienea zamani kipindi Cha ukoloni kwasababu wakoloni walikuwa na Nguvu kiuchumi. Narudia kingereza kingekuwa lugha ya watu maskini kisingeenea Wala kupendwa. Hata ikitokea Leo mataifa yenye hati miliki ya kingereza yakaanguka kiuchumi na kingereza kitakufa Kama zilivyokufa lugha za kale zilizokuwa na Nguvu Kama Kiyunani kilatini Kama sijakosea
 
Huo ni Ukoloni mambo leo.....!!! Ujerumani, china, korea na japan wanasoma kwa lugha zao na wamefanikiwa.....Shida afrika ukiongea kingereza unaonekana bora......!! Cha msing na sekondar ni kuwa na mitaala ambayo itakizi mabadiliko ya hal halis na inayoondoa utegemez wa ajira....!! Kuanzia shule za msing kuwe na masomo ya ufund na stad za kaz za miaka ya 90' na 2000' nakumbuka tukiwa shule ya msingi tulipika keki, maandaz na tulitengeneza mapambo na tukasoma NOTI na ALA za mziki mpaka now zimenipa experience katika mziki....HII NDIO ELIMU TUITAKAYO KWA VIJANA WA SASA ACHANA NA KINGEREZA ambapo zaid ya 80% ya watanzania na afrika hawana uwezo wa kwenda ulaya....!!!
 
Wakuu kingereza kwa sasa hakilazimishwi kujifunza na mataifa yenye nguvu wala hakihusiani na ukoloni ila tunajifunza ili kukitumia kama daraja la kuwasiliana na mataifa mengine ambayo haya kifahamu kiswahili sawa.

Hebu nielweke kwamba endapo tusipo jifunza kingereza hatutaweza kuwasiliana na mtu wa kimataifa, na watu wakimataifa hawatoweza kuwasiliana na sisi kwahiyo kwasababu hii tunakitumia kingereza kama lugha ya kuwasiliana duniani yani kama daraja la mawasiliano na sio eti kinalazimishwa na mataifa tajiri kwasababu za kiuchumi.
 
Sisi tunalazimika kujifunza kingereza kwa sababu tunufaike na fursa zilizopo katika kingereza Kama vile, ajira, biashara, n.k ,, Tanzania tungekuwa Nchi tajiri Kama ufaransa, uchina, au ujerumani tusingehangaika na kingereza kwa kiasi hiki . Tunalazimika kujifunza kingereza kwasababu sisi Ni duni kiuchumi na sii vinginevyo
 
Sio mawazo mabaya Kama unavyo dhani nafikiri nikukosa kwako uelewa tu. Lugha ambacho nikipengele Cha utamaduni huwezi kutenganisha na Uchumi nivitu vinavyotegemeana. Uchumi unakuza lugha na lugha unakuza uchumi. Lugha haiwezi kujua na kukubalika bila kuwa na Nguvu ya uchumi. Leo hii Uingereza inalo shirika la British kanseli ambalo hutengewa mabilioni kila mwaka kwaajili ya kukuza kiingereza duniani mataifa mengine kuendelea kujifunza lugha ya mataifa yenye hakimiliki ya kingereza Kuna faida za kiuchumi wanapata ndiposa wamewewwkeza katika kueneza lugha Yao kwasababu Wana uchumi IMARA. Tanzania Kuna shirika gani linaloeneza kiswahili na utamaduni duniani? ...Leo hii hata kampuni ya matangazo ya Google AdSense haiweki matangazo ya biashara katika tovuti za kiswahili kwakuwa wanaamini hakuna biashara ya maana inaweza kufanyika kwasababu inaaminika wazungumzaji wa kiswahili Ni duni kiuchumi.
 
Sababu ya kufikiria hivyo ni nini. Kwanini isiwe Kiswahili hadi chuo Kikuu. Hii nchi fushafeli bora tuanze upya tu kivyetuvyetu.
 
Sababu ya kufikiria hivyo ni nini. Kwanini isiwe Kiswahili hadi chuo Kikuu. Hii nchi fushafeli bora tuanze upya tu kivyetuvyetu.
Kwasababu ikiwa hivyo kiswahili mpaka chuo watanzania watakuwa wanafahamu lugha moja tu ya kiswahili hali inayoweza kupelekea tushindwe kuwasiliana na mataifa mengine mengi ambayo hayakifahamu kiswahili chetu hivyo ni muhimu na sisi kwenye shule zetu tujifunze kingereza
 
Sio kuwasiliana nje tu hata ajira za ndani tutakosa kutokana na kuwa lugha inayotumika huko Ni kingereza. Kwa ufupi Tanzania hatuna ubavu wakujitegemea hata kwenye lugha
 
 
Wachina
Wakorea
Wajapani
Wanasema kwa kiingereza?
 
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…