Shule za VIPAJI maalum: Nini dhumuni lake hasa?

shule za wenye vipaji maalumu zipo hata nchi zingne kama usa.
HADI university zipo kwa mfano qualification za kuingia stanford univ.havard,m.i.t ni za juu zaidi ya vyuo vingine.lakini nao bado wana consider academic qualification

Wapi imeandikwa kuwa Harvard ni chuo cha watu wenye vipaji maalum? Wapi imeandikwa Stanford ni chuo cha wenye vipaji maalum?

Mimi binafsi nawajua watu waliosoma kwenye hivyo vyuo ambao hawana vipaji maalum.

Sasa wewe hizo habari za hivyo vyuo kuwa ni vya watu wenye vipaji maalum umezitoa wapi?

Hebu nitajie shule (ambazo siyo vyuo) za USA ambazo ni za watu wenye vipaji maalum, tafadhali.
 

Kaka Ngabu tokea mwanzo kama umenisoma niliweka bayana kuwa kigezo pekee kitumiwacho na serikali kudahili wanafunzi katika shule hizi ni alama au viwango vya ufaulu.

Msamiati "kipaji maalumu" kuna uwezekano unatumika ndivyo sivyo au lengo lake silo linalotekelezwa, na nimeandika hivi kutokana na vigezo vitumikavyo kuwapata wanafunzi wasomao katika shule hizi.

Ukiniuliza mimi nina vipaji au kipaji gani maalumu naweza kukutajia lakini mwisho wa siku hakijawahi kuwa kigezo kilichonipa fursa ya kusoma shule hizo.

Kigezo pekee ni kupata maksi kubwa ana darasa la saba, idadi kubwa ya A's kidato cha nne na sita na kuendelea.

Huenda lengo la serikali ilikuwa ni kujaribu kuvumbua Watanzania wenye vipaji maalumu, wakiamini kwa kuanzia watumie kigezo cha ufaulu baada ya incubation fulani wanaweza kupata hivyo vipaji maalumu (hivi ndivyo ninavyodhani sina uhakika).

Hata nchi zilizoendelea zina shule kama hizi na pia kuna vyuo vikuu vya namna hii, walichotuzidi ni kuwa wenzetu hawana longolongo.
 
Je unachokariri hadi unakikeshea kinatoka kwenye mtihani? Kama wana vipaji basi wengi wao wana vipaji vya uwezo mkubwa wa kukariri masomo.

Mosi naomba uisome post yangu hapo juu....

Pili, uwezo wa kuelewa unachosoma na kipaji ni mambo mawili tofauti isipokuwa kuna wakati mambo hayo hutegemeana...

Tatu, neno sahihi linalotumiwa na serikali ni vipaji maalumu vya kiakili and otherwise....
 
Kigezo pekee ni kupata maksi kubwa ana darasa la saba, idadi kubwa ya A's kidato cha nne na sita na kuendelea.

Kwa hiyo inawezekana kabisa kuwa mtu asiye na kipaji chochote kile kilicho maalum akachaguliwa kwenda kusoma kwenye hizo shule kutokana na yeye kufaulu vizuri (kwa vigezo vya NECTA) kwa sababu ya bidii na juhudi zake za kujisomea na kuwa attentive darasani, siyo?

Na pia inawezekana kabisa mtu asiye na kipaji chochote kile kilicho maalum na wala asiye na juhudi wala bidii lakini ambaye kwa namna moja ama nyingine anafaulu vizuri (kwa vigezo vya NECTA) mtihani wa mwisho kutokana na kuiba mtihani akapata udahili kwenye hizo shule, siyo?

Naomba nitajie shule na vyuo vya hivyo kwenye nchi za Marekani na Uingereza, tafadhali.
 

Ubishi mwingine haujengi ndugu yangu, nadhani kuna kitu mnapishana ambacho wewe unakijua ila umeamua kubishana na vijana humu jamvini. Ili mtu awe daktari (ama tunaposema huyu ana kipaji cha udaktari) tunampima kwa vigezo vipi? .Pia usisahau kipaji lazima kikuzwe (ni njia zipi zinatumika kukikuza hicho kipaji?)

Tanzania waliweka mfumo- ili ukitaka kujua mtoto yupi anakipaji cha udakitari tutawafundisha darasani halafu tutawapa mtihani. Atakayefaulu 145/150 huyo ndiye mwenye kipaji (Kwa vigezo vya wizara ya elimu). Halafu wakaendelea mbele kwa njia ile ile kwa miaka 4 (atakayepata 3A kwa maana ya biology ,chemistry na Physics -atakuwa kipaji maalumu ukiongeza na sifa chache za ziada). Baadae mtu huyu anapelekwa chuo cha udakitari .Mengine unayajua

Sasa huu uongo unaotaka kutuaminisha hapa kuwa harvard wanaingia wanafunzi wa kawaida naomba uukane ama ulete majina ya hao unaowajua wamesoma havard ambao ni watz na hawakuwa na marks na vigezo kama vile vilivyowekwa na wizara ya elimu (kwamba hawa ni vipaji maalumu).

Nipo tayari kujifunza zaidi kutoka kwako' TAFADHALI. Pia ningependa kujua chuo ulichosoma wewe mwanafunzi aliyepata GPA 4.0 alikuwa anauwezo kiasi gani kama utaweza !?
Harvard University - GPA and Test Scores for Admission
Ad

ITT Tech - Official Sitewww.itt-tech.eduAssociate, Bachelor Degree Programs Browse Programs Now & Learn More.


See the real-time chart and learn your chances of admission to Harvard with the Cappex 'What are my chances?' calculator
Data provided by Cappex.com


Compare GPA and Test Score Data for Other Ivy League Schools: Brown | Columbia |Cornell | Dartmouth | Harvard | Penn | Princeton | Yale
With a single-digit acceptance rate, Harvard University is the most selective university in the United States. This member of the Ivy League sends out a remarkable number of rejection letters. In the graph above, the blue and green dots represent accepted students, and you can see that most students who got into Harvard had 4.0 GPAs, SAT scores (CR+M+W) above 2100, and ACT composite scores above 30. Also realize that there's a lot of red hidden beneath the blue and green in the upper right corner of the graph. Many students with perfect GPAs and test scores in the top 1% still get rejected from Harvard. Even the most qualified students should consider Harvard a reach school.
At the same time, don't give up hope of getting into Harvard if you don't have a 4.0 and a 2400 on the SAT. Harvard has holistic admissions, and they are looking for students who bring to campus more than good grades and test scores. Students who have some kind of remarkable talent or have a compelling story to tell will get a close look even if grades and test scores aren't quite up to the ideal.
To learn more about Harvard University, high school GPAs, SAT scores and ACT scores, these articles can help:
 

Ubishi wangu ni wa msingi kabisa. Labda tatizo lako ni kushindwa kuelewa tu.

Tanzania waliweka mfumo- ili ukitaka kujua mtoto yupi anakipaji cha udakitari tutawafundisha darasani halafu tutawapa mtihani.

Huh? Kwa hiyo udaktari ni kipaji? Ama kweli ndo maana tupo kwenye hali tuliyonayo!!

Atakayefaulu 145/150 huyo ndiye mwenye kipaji (Kwa vigezo vya wizara ya elimu).

Naam, hapo ndo ninapogomba napo. Kufaulu vizuri tu hakumaanishi mtu ana kipaji maalum. Na nimeshatoa mifano kuwa mtu mwenye average intelligence anaweza akajisomea tu kwa juhudi na bidii zake na kufaulu vizuri mitihani yake ya taifa na nyie mkamweka kwenye kundi la watu wenye vipaji maalum. Au mtu ambaye kaiba mitihani anaweza kabisa kufanya vizuri kwenye hiyo mitihani aliyoiiba na kwa vigezo vyenu mkaingia mkenge na kumweka kwenye kundi la watu wenye vipaji maalum ilhali hana kipaji chochote kile kilicho maalum. Sasa hii ni hoja nyepesi sana ila kwako na wengine inaonekana ni ngumu sana kuiona. Sijui kilicho kigumu kukiona hapo ni nini!!!

Halafu wakaendelea mbele kwa njia ile ile kwa miaka 4 (atakayepata 3A kwa maana ya biology ,chemistry na Physics -atakuwa kipaji maalumu ukiongeza na sifa chache za ziada). Baadae mtu huyu anapelekwa chuo cha udakitari .Mengine unayajua

Flawed selection/ identification methodology.


Well, George W. Bush, rais wa zamani wa Marekani kasoma Harvard na Yale na hakuwa na grades zozote zile za kutisha. Alikuwa ni average (C) student. Huo ni mfano wa mtu ambaye hata wewe unamjua/ at least umewahi kumsikia. Ana kipaji gani kilicho maalum huyu?

Nipo tayari kujifunza zaidi kutoka kwako' TAFADHALI. Pia ningependa kujua chuo ulichosoma wewe mwanafunzi aliyepata GPA 4.0 alikuwa anauwezo kiasi gani kama utaweza !?

Chuo nilichosoma mimi watu kibao waliokuwa hawakosi kwenye dean's list ni wale ambao walikuwa serious na masomo yao hatukuwa tunakuwa designated kama exceptionally gifted students.

Many students with perfect GPAs and test scores in the top 1% still get rejected from Harvard. Even the most qualified students should consider Harvard a reach school.
At the same time, don't give up hope of getting into Harvard if you don't have a 4.0 and a 2400 on the SAT. Harvard has holistic admissions, and they are looking for students who bring to campus more than good grades and test scores.


Naomba upasome hapo pekundu.

Students who have some kind of remarkable talent or have a compelling story to tell will get a close look even if grades and test scores aren't quite up to the ideal.


Na hapo.


 

Haya mtaalamu nimejaribu kukuelewa na nitaongeza juhudi niwe nakuelewa zaidi .Mimi nilijua Bush ana kipaji kumbe ni bogus tu kwa utaalamu wako. Leo ndio nimepata maarifa kuwa mtu anaweza akawa kiongozi mkubwa wa taifa kama marekani na akawa ni Bogus. I salute you...
 
ORODHA ya vichwa waliopitia shule yA ilboru NA IMPACT ZAO kwa jamiii pima mwenyewe
1.tundu lissu
2.mwigulu nchemba
3.SUMAYE
4.LOWASA
5.MIMI


R I P WALIMU WANGU mr mgaya,chief,shembilu
 
ORODHA ya vichwa waliopitia shule yA ilboru NA IMPACT ZAO kwa jamiii pima mwenyewe
1.tundu lissu
2.mwigulu nchemba
3.SUMAYE
4.LOWASA
5.MIMI


R I P WALIMU WANGU mr mgaya,chief,shembilu

Duh! Hatari tupu!
 
Mkuu Ngabu labda nianze kwa upya kwa mtazamo wa lugha ya Umombo kidogo tukaelewana.

Kwa mujibu wa tafrisi kutoka kamusi ya Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, neno kipaji limetoholewa kama ifuatavyo:

kipaji nm vi- ki-/vi ability, talent, endowment, gift, aptitude, flair, genius.

Pia katika moja ya chapisho nililowahi kulisoma mtandano limetoa tafsiri ifuatayo ya neno kipaji:

Kipaji ni UWEZO wa ASILI wa KIPEKEE alionao MWANADAMU,kutoka kwa MUNGU.

Kuna aina nyingi za vipaji kulingana na kila mwanadamu alivyojaaliwa, vipo vipaji ambavyo matokeo yake ni tangible na vipo vingine ambavyo matokeo yake hayashikiki.

Wanadamu waliojaaliwa uwezo mkubwa wa kufikiri, kuhifadhi kumbukumbu muda mrefu na kung'amua njia rahisi za kukabiliana na vikwazo vihitajivyo kunoa mbongo, watu hawa husemakana wana Kipaji cha Utashi ,huku kwetu ndio neno Vipaji Maalumu vya Akili limetumiwa na serikali.

Vipaji vilikuwepo, na vitakuwepo. Na kama kuna kitu kinapatikana kwa USAWA kabisa, pengine ni VIPAJI, maana vinatoka kwa MUNGU. Hivyo, kazi kubwa kwetu sisi binadamu,inakuwa ni KUVIGUNDUA,KUVIBORESHA NA KUVIENDELEZA.

Hizo K's tatu ndizo ambazo nchi yetu ilikuwa na imekuwa ikijaribu kufanya kwa wale walio na vipaji maalumu vya kiakili, ndivyo ambavyo Rais wa sasa wa TFF anajaribu kufufua mpira wa miguu Tanzania, ndivyo ambavyo mataifa yalioendelea yamefanikiwa kuzalisha WAVUMBUZI na WAGUNDUZI katika nchi zao.

Kutokana na maelezo hayo hapo juu sasa nijibu maswali yako:


Mkuu vigezo na masharti ya kujiunga na shule aina nne za serikali nilifafanua kwa kirefu ukurasa wa kwanza wa thread hii, tafadhali rejelea huko

Naomba nitajie shule na vyuo vya hivyo kwenye nchi za Marekani na Uingereza, tafadhali.

Sijawahi kuishi nchi hizo mbili mkuu, la hasha nimeshawahi kuishi nchini China na huko kuna vyuo kama Fudan, Tsingua, Shanghai Jiaotong, Renming n.k vina research centre maalumu kwa wanafunzi tu.
 

Hujajibu kabisa hayo maswali yangu mawili.

Ngoja niulize tena:

Kwa hiyo inawezekana kabisa kuwa mtu asiye na kipaji chochote kile kilicho maalum akachaguliwa kwenda kusoma kwenye hizo shule kutokana na yeye kufaulu vizuri (kwa vigezo vya NECTA) kwa sababu ya bidii na juhudi zake za kujisomea na kuwa attentive darasani, siyo?

Na pia inawezekana kabisa mtu asiye na kipaji chochote kile kilicho maalum na wala asiye na juhudi wala bidii lakini ambaye kwa namna moja ama nyingine anafaulu vizuri (kwa vigezo vya NECTA) mtihani wa mwisho kutokana na kuiba mtihani akapata udahili kwenye hizo shule, siyo?
 
ORODHA ya vichwa waliopitia shule yA ilboru NA IMPACT ZAO kwa jamiii pima mwenyewe
1.tundu lissu
2.mwigulu nchemba
3.SUMAYE
4.LOWASA
5.MIMI


R I P WALIMU WANGU mr mgaya,chief,shembilu

With exception ya Mwigulu na wewe pengine; nina uhakika hao wengine hawajasoma wakati shule hizo zikiwa ni maalumu.
 

Kwa kuwa umesisitiza sana, jibu ni kuwa kuna uwezekano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…