Mkuu Ngabu labda nianze kwa upya kwa mtazamo wa lugha ya Umombo kidogo tukaelewana.
Kwa mujibu wa tafrisi kutoka kamusi ya Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, neno kipaji limetoholewa kama ifuatavyo:
kipaji nm vi- ki-/vi ability, talent, endowment, gift, aptitude, flair, genius.
Pia katika moja ya chapisho nililowahi kulisoma mtandano limetoa tafsiri ifuatayo ya neno kipaji:
Kipaji ni UWEZO wa ASILI wa KIPEKEE alionao MWANADAMU,kutoka kwa MUNGU.
Kuna aina nyingi za vipaji kulingana na kila mwanadamu alivyojaaliwa, vipo vipaji ambavyo matokeo yake ni tangible na vipo vingine ambavyo matokeo yake hayashikiki.
Wanadamu waliojaaliwa uwezo mkubwa wa kufikiri, kuhifadhi kumbukumbu muda mrefu na kung'amua njia rahisi za kukabiliana na vikwazo vihitajivyo kunoa mbongo, watu hawa husemakana wana
Kipaji cha Utashi ,huku kwetu ndio neno Vipaji Maalumu vya Akili limetumiwa na serikali.
Vipaji vilikuwepo, na vitakuwepo. Na kama kuna kitu kinapatikana kwa USAWA kabisa, pengine ni VIPAJI, maana vinatoka kwa MUNGU. Hivyo, kazi kubwa kwetu sisi binadamu,inakuwa ni KUVIGUNDUA,KUVIBORESHA NA KUVIENDELEZA.
Hizo K's tatu ndizo ambazo nchi yetu ilikuwa na imekuwa ikijaribu kufanya kwa wale walio na vipaji maalumu vya kiakili, ndivyo ambavyo Rais wa sasa wa TFF anajaribu kufufua mpira wa miguu Tanzania, ndivyo ambavyo mataifa yalioendelea yamefanikiwa kuzalisha WAVUMBUZI na WAGUNDUZI katika nchi zao.
Kutokana na maelezo hayo hapo juu sasa nijibu maswali yako:
Kwa hiyo inawezekana kabisa kuwa mtu asiye na kipaji chochote kile kilicho maalum akachaguliwa kwenda kusoma kwenye hizo shule kutokana na yeye kufaulu vizuri (kwa vigezo vya NECTA) kwa sababu ya bidii na juhudi zake za kujisomea na kuwa attentive darasani, siyo?
Na pia inawezekana kabisa mtu asiye na kipaji chochote kile kilicho maalum na wala asiye na juhudi wala bidii lakini ambaye kwa namna moja ama nyingine anafaulu vizuri (kwa vigezo vya NECTA) mtihani wa mwisho kutokana na kuiba mtihani akapata udahili kwenye hizo shule, siyo?
Mkuu vigezo na masharti ya kujiunga na shule aina nne za serikali nilifafanua kwa kirefu ukurasa wa kwanza wa thread hii, tafadhali rejelea huko
Naomba nitajie shule na vyuo vya hivyo kwenye nchi za Marekani na Uingereza, tafadhali.
Sijawahi kuishi nchi hizo mbili mkuu, la hasha nimeshawahi kuishi nchini China na huko kuna vyuo kama Fudan, Tsingua, Shanghai Jiaotong, Renming n.k vina research centre maalumu kwa wanafunzi tu.