May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Dunia inaenda kasi sana na hakuna wa kumsubiri mwingine eti ndio tuende sawa.
Ni dhahiri kuwa Mataifa yaliyoshika hatamu za dunia hii wao wamewekeza sana kwenye sayansi na teknolojia, gunduzi mbalimbali zinazofanywa na Wananchi wao ndio zinazogeuzwa bidhaa na wengine tuliobaki tunakuwa Wateja.
Hakuna kinachokuja kama zawadi bila mikakati madhubuti, hivyo nasi Tanzania tujiulize ni nini mchango wetu kwenye hili? Ni nini tunafanya kukuza na kuwaendeleza Wabunifu wetu?
Nadhani ipo haja ya kuanza kuwatambua wale Wanafunzi wote wanaoonesha uwezo wa kubuni ili walau mara moja kwa wiki kuwa na muda nao maalumu kwa ajili ya wao kujinafasi ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi (vya kuchokonoa) wangali wadogo.
Nina wasiwasi kuwa tunawapoteza Wabunifu wengi sana kwa kuwaacha tu wakimezwa na mfumo wetu huu wa elimu tuliojiwekea, yaani Mtoto anatoka nyumbani asubuhi na kushinda Darasani na kisha baadae anarudi nyumbani akiwa amechoshwa na ma theory ya "Mali empire" wanayojazwa na Walimu wao.
Kuwe na mikakati ya kuhakikisha wale ambao wataonekana na muelekeo huo basi watakuwa na fursa ya kuunda kitu chochote kile, kuanzia mpira wa makaratasi mpaka Magari ya matairi ya visoda, walau kila siku Mtoto aunde kitu.
Bila ya hivyo tutabaki kuwa Wasindikizaji tu tena waliokata tamaa hapa Duniani.