Shutuma za Diamond Platnumz dhidi ya Forbes, sasa naanza kuamini maneno ya Vijiweni kuwa Bakheresa ni tajiri zaidi ya MO

Shutuma za Diamond Platnumz dhidi ya Forbes, sasa naanza kuamini maneno ya Vijiweni kuwa Bakheresa ni tajiri zaidi ya MO

Basi hastaili kuwepo kwenye reference kama hujui anachomiliki.
Mimi nimenukuu maneno ya shutuma zake vipi unibebeshe mzigo wa lawama wakutaka kujua kipi anamiliki
unajua nani anayeshikilia soko la kusafirisha korosho za Tanzania nje na nani ana kibali pekee cha kuingiza bidhaa za lg pamoja na pikipiki boxer.....halafu next time ukikurupuka na kusema sijui bakhresa anamiliki shamba la miwa ukiwa unaelekea Tanga na kuona yale mashamba ya mkonge unayaangalia hadi unalala ukiamka hujamaliza ujiulize ni nani/...maana kwa uwezao wako wa kuchambua hoja hata nikikuambia ukafuatilie walipaji wakubwa wa kodi TRA kati ya MO na BAKHRESA bado ntakuchosha…… mo ni Tajiri bahili kuliko bakhresa ujue tu mwenzio ndo anaongoza kuajili watu wengi Afrika mashariki na kati baada ya serikali yako
Sawa, ila mbona inakuwa ngumu kwa watu wa kawaida kuamini Mo ni tajiri kuliko SSB?
 
Mkuu,huyo mleta thread ni kati ya wale vijana wanaoangalia vitu juu juu na kuleta mabishano yasomaana! Anadhani anavyoona magari ya Bakhresa yanavyopita road na ile mibango anaamini ndo utajiri! Anadhani kuimiliki Azam media,kuwa na kiwanja Chamanzi na kumiliki timu ndio utajiri!! Hamjui MO vizuri huyu!!
Wewe unayemjua MO vizuri nadhani ungemuelezea maana naona umezidi kuungana na Watu wa Vijiweni wanao amini kuwa SSB ni tajiri kwa kuataja baadhi ya utajiri wake
 
Mimi nimenukuu maneno ya shutuma zake vipi unibebeshe mzigo wa lawama wakutaka kujua kipi anamiliki

Sawa, ila mbona inakuwa ngumu kwa watu wa kawaida kuamini Mo ni tajiri kuliko SSB?
ndo maana wakawa watu wa kawaida wanaoamini diamond ni Tajiri kisa anamiliki prado na share kidogo kwenye kituo cha redio….jifunze kuamini wataalamu na sio vijiwe vya kahawa
 
Nimegundua Diamond ana akili fupi sana au anatafuta kick tu. Hauwezi kuja na kuanza kuisema Forbes wakati wewe mwenyewe unajijua hauna utajiri wa kujilinganisha na Davido au Wazkid. Utajiri wa mtu huwa unapimwa na thamani ya Asset, Cash au Shares ambazo anazo kwenye kampuni. Sasa Diamond Asset ngapi hapa mjini au Shares ngapi? Ni ujinga tu.
Dhana ya Diamond ni kuwa Forbes walipaswa kumfuata na kuwapatia full details toka kwake labda angewatajia hizo assets, Cash na liabilites na hapo sio lazima Diamond awe juu ya Davido
 
Nyie wapumbavu tajiri yeyote anapimwa kwa ulipaji wake wa kodi na tozo za serikali,.Forbes hawaji Vijiweni kuuliza punguani kama nyie mnaohesabu Utajiri wa mtu kwa macho. Nini MO, Bakhresa hamfikii hata Rostam kwa Utajiri.
 
ndo maana wakawa watu wa kawaida wanaoamini diamond ni Tajiri kisa anamiliki prado na share kidogo kwenye kituo cha redio….jifunze kuamini wataalamu na sio vijiwe vya kahawa
Acha kudharau Vijiwe vya kahawa, kule kuna watu wa kila aina hata hao unaowaita wasomi huwa jioni wakirudi toka makazini wanaenda Vijiwe vya Kahawa kubadilishana mawazo na walalahoi.
 
Nyie wapumbavu tajiri yeyote anapimwa kwa ulipaji wake wa kodi na tozo za serikali,.Forbes hawaji Vijiweni kuuliza punguani kama nyie mnaohesabu Utajiri wa mtu kwa macho. Nini MO, Bakhresa hamfikii hata Rostam kwa Utajiri.
Punguza ukali wa maneno, Mpumbavu mwenyewe
 
Habari, Jana msanii tajika sana nchini Tanzania, Afrika Mashariki na kati na pengine kuliko wote kusini mwa jangwa la Sahara Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, alisaini dili kubwa na moja kati ya recording label kubwa ya muziki dunia, Warner Music Group, kuhusu usambazaji wa kazi za muziki wake na Wasanii walio katika label yake ya WCB WASAFI.

Muda mfupi baada ya Diamond kusaini mkataba huo alitumia page za mitandao ya kijamii ya Instagram na Twitter kutoa shutuma kwa kampuni kubwa ya Kimarekani inayojihusisha na tafiti za kubaini watu wenye ukwasi (UTAJIRI), FORBES, kuwa hawakufanya tathimini vizuri juu ya ukwasi aliona kupitia ile list waliyoitoa last week inayonesha Wasanii matajiri zaidi barani Afrika ambapo kwenye list hiyo Naseeb hayumo hata kwenye top 20!

Sio mara ya kwanza hawa FORBES kulalamikiwa na baadhi ya watu juu ya takwimu zao kwa mfano ni mwaka jana tu rapper Mkubwa toka "STATE", Kanye West, alilalamika na kuwapa makavu hao FORBES kwa kumkadilia kiduchu juu ya utajiri wake kitu achapo kilizua gumzo sana Dunia nzima na ikapelekea kwa hao FORBES kuingia chimbo kumkadilia tena Kanye na hatimaye wakamtangaza kuwa yuko katika orodha ya Ma-rapper billionares sambamba na Jay Z, P.Diddy na Dr Dree.

Kwa huku kwetu Tanzania, kila mwaka FORBES wamekuwa wakitoa orodha ya watu matajiri zaidi nchini na kwa mara zote wamekuwa wakimtaja Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (METL), Mohammed Dewji - Mo, kuwa ndiye billionaire kinara hapa kwetu na pengine ndiye billionare kijana kuliko wote Afrika. Hii imekuwa ikipingwa na baadhi ya watu hasa katika "vijiwe vya kahawa" kwani wengine wanaamini kuwa mmiliki wa Makampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB Group of Companies) - Saidi Bakheresa kuwa ndiye mwenye pesa nyingi kuliko wote hapa Tanzania kwani ana mali zisizo amishika zinazo onekana na kujilikana na kila mtu tofauti na huyo MO.

Kwa scenerio hizo, nami kama naanza kuamini hayo maneno ya Vijiweni kuwa Bakhresa ndiyo tajiri namba moja hapa kwetu Tz kwani kila mtu anaziona mali zake kama Wiwanda vyake kila kona hapa nchini na kwa DSM Mfano ni pale Buguruni, Mwandege, Uwekezaji Mkubwa pale Chamazi - Azam complex, kuleze Zanzibar ana uwekezaji mkubwa sana sitaweza kutaja wote ila chukulia mfano wa Hotel Verde na ule Mji wa kitalii wa Fumba. Ana mradi mkubwa wa uzalishaji wa miwa pale Bagamoyo ambapo itapelekea kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha sukari nchini. Pia bidhaa za Azam zimekuwa nambari moja katika nchi nyingi za Afrika na ni nadra sana kwa Mtanzania wa kawaida kupita siku bila kutumia bidhaa hata moja ya Azam hasa za Vyakula na Vinywaji!.

Mwisho napenda kuhitimisha kuwa pengine Diamond yuko sahihi kuwa Forbes memkadilia vibaya na pia Forbs wamemkadilia vibaya Bakhera (kwa Bakhersa nina asilimia kubwa hii ni kutokana na hulka yake ya kutopenda kuweka mambo yake hadharani na huwa hapendi kujionesha wala kuonekana onekana tofauti na MO au matajiri wengine tunao wajua).

Nawasilisha na asanteni.
Diamond anashida ya kuji overrate his just a regular musician just above average sema kwa kuwa kashika head lines za East Africa ndio kachanganyikiwa na kujitoa kwenye uhalisia hao anaotaka kushinda nao wanamiliki nyumba adi USA na foreign cars tupu izo toyota V8 used zinampa kiburi kijana wz tandale.He should consider himself luck ata Forbes wamemtaja ata..

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Huwa sikurupuki kuandika mambo ambayo sijayafanyia utafiti wa kina kwa kutegemea vichwa vya habari vya magazeti ya udaku.
Sasa lipi la udaku? kuwa Bakheresa tajiri? kuhusu la Bagamoyo sugar wala sio udaku ni la kweli na hata huyo muwekezaji wa kwanza kaishtaki Tanzania sasa ungekuwa specific lipi la udaku.
 
Acha kudharau Vijiwe vya kahawa, kule kuna watu wa kila aina hata hao unaowaita wasomi huwa jioni wakirudi toka makazini wanaenda Vijiwe vya Kahawa kubadilishana mawazo na walalahoi.
huwezi kua Msomi na ukapata mda wa kukaa hivyo vijiwe...labda uwe usalama/..ila kwakua umeamua kubeba ujinga...sina mda wa kukusaidia huo mzigo….mjinga bnafundishika...mpumbavu ni kumuacha tu
 
ukiwa unaelekea Tanga na kuona yale mashamba ya mkonge unayaangalia hadi unalala ukiamka hujamaliza ujiulize ni nani
hayo mashamba ya mkonge unayozungumzia ni yale ambayo aliyanunua kiujanjajanja serikalini enzi za utawala wa mkapa na sera yake ya ubinafsishaji?.

ni mashamba haya ambayo aliyatumia kama dhamana kuchukulia mikopo mikubwa kwenye mabenki ya nje?.

ni mashamba haya ambayo yalimpelekea jiwe kutumia umafia kumteka MO na kumpeleka mafichoni abinywe makende ili akiri kuyarudisha serikalini au atoe pesa kama fidia?.
 
haya mawazo yako ndo maana yanakufanya wewe uwe masikini na yeye kua billionea….na ukiendelea nayo ukizeeka lazima uwe mchawi…. hamnaga utajiri wa haki mzee ndo maana wakizeeka wanaishia kutoa sana misaada kujisafisha
 
Nyie wapumbavu tajiri yeyote anapimwa kwa ulipaji wake wa kodi na tozo za serikali,.Forbes hawaji Vijiweni kuuliza punguani kama nyie mnaohesabu Utajiri wa mtu kwa macho. Nini MO, Bakhresa hamfikii hata Rostam kwa Utajiri.

Vere vere truu
 
Back
Top Bottom