Si ajabu wangekuwa washadai yeye si Mtanzania!

Nimeona waliberia wameanza kutimuliwa nyie kina Mange mtapona kweli?!!!
 
Boss idawa Hauogopi Watu Wasiojulikana???!!! Haujui kukosoa ni Kosa la Jinai???!!! Umeongea vizuri na ukweli. Boss Mkuu alianza vizuri sana. Ila sasa sijui kalewa sifa au wanaomshauri na kujishauri wanamdanganya na kujidanganya.
Mkuu haijalishi unaogopa ama jasiri mwisho wa siku utaumizwa na maamuzi ya hii serikali.....
 
Kijana Nyani Ngabu unakosea unapomfananisha Lissu na Miguna....Lissu ni mvuta bangi na mla unga na hana usawa wowote na Miguna.
 
Reactions: Oii
Nawe wajipendekeza kwangu?
Amesoma,Leseni yake ni Kubwa....
Ni Dereva mzoefu tatizo lake ni Mkuda....
Magari ya Wagonjwa Hayapishi...
Waenda kwa miguu,Ambao amewagonga Hawahesabiki....
Hili basi analiendesha Vibaya... matuta Anafukia....
Najuta kulidandia........
Kauzu....... Anatupeleka Puta Abiria..
Wengine Sauti zimewakauka Kwa Kulia..
 
Africa ingefaa itawaliwe tena?
 
Umeiweka vizuri mwanzo lakini kuna maeneo umepindisha na kucheza siasa badala kuzingatia ukweli ili hoja ijadiliwe ipasavyo, Miguna amekua akikosoa serikali na kuropokwa yote, kwanza kipindi alikua anagombea ugavana alitapika maneno ya kila aina, na akaachiwa bila ya kufuatwa. Tatizo limekuja pale alipitiliza kwa kumlisha kiapo cha urais Raila Odinga, hapo Jubilee walihisi kama ametoboa jicho, ikabidi wamkumbushie kale kadhambi kake ka kuukana uraia na kutafuta uraia wa nchi nyingine.

Kumbuka kipindi hicho Kenya hatukua na uraia pacha, ilikua kwamba ukiupata uraia wa nchi nyingine unapoteza wa Kenya. Kwa kifupi awamu ya Kibaki/Raila walifanya figisu na kuvunja shria na kumpa pasipoti ya Kenya bila ya kufuata taratibu za kisheria. Hiyo dhambi ameishi nayo na imekua ikifumbiwa macho hadi alipoichokonoa serikali kwenye macho.
 

Aliidhinishwaje na IEBC kugombea ugavana wa Nairobi 2017????

 
Reactions: Oii
Michezo ya kisiasa kama hii siyo ipo Afrika tu. Hata nchi zilizoendelea kama USA ipo. Ni sawa tu na Billy Bush alivyoukalia mkanda wa video uliokuwa unamuonyesha Trump akiwazungumzia wanawake kwa matusi; siku za mwisho kuelekea uchaguzi uliompa Trump urais ndiyo Billy Bush akautoa huo mkanda, presumably in an attempt to help stop Trump from becoming president.
 
Aliidhinishwaje na IEBC kugombea ugavana wa Nairobi 2017????


Narudia tena, serikali ya awamu ya awali ilitenda kosa kumpa pasipoti bila ya kufuata taratibu za kisheria, serikali ya sasa ikafumbia macho hako 'kadhambi', ikamuacha akaidhinishwa kugombea ugavana tena kwa mlengo wa upinzani huku akikosoa serikali balaa.
Sasa serikali ilizidiwa uzalendo au uvumilivu pale aliichokonoa hadi kwenye jicho kwa kutenda kosa la 'uhaini' la kumuapisha Raila. Ndio ikabidi kufukua mifupa yake.
 

Sasa mbona mpaka hivi sasa mahakamani anawabwaga hao watu wa serikali?

Na sheria ya uraia ya sasa inasemaje kuhusu Wakenya waliokuwa na uraia wa nchi nyingine kabla ya katiba ya sasa?

Nakwambia mahakamani Miguna atawagaragaza hao serikali.

Believe me [emoji16]
 

Kesi iliyowasilishwa mahakamani haihusiani na mambo ya uraia, hivyo ana kila sababu za kuwabwaga maana kilicho mbele ya mahakama ni tofauti kabisa.
Kwa sasa kinachotendeka ni kuhakikisha haruhusiwi kuingia ndani maana hana stakabadhi za uraia wa Kenya.
Wakenya wote waliokua wameukana uraia enzi zile waliombwa waje wawasilishe maombi ya uraia pacha, yeye hakufanya hicho, alitumia mbinu za kifisadi na kupata pasipoti kinyume na sheria.

Kwa kifupi, kama nilivyojibu kwenye hoja zingine, unapoichokoa serikali, hakikisha huna mifupa ya kufukuliwa, leo hii hata Magufuli kuna makaburi ya awamu ya nee anafukua, na kunayo anaachia tu. Ndiovyo siasa za Afrika zilivyo.
 
Na CHADEMA walitangaza kumuunga mkono Uhuru [emoji16][emoji16][emoji16]
Sssssh usiseme sana.
Utawaudhi chadema.

Wanapenda sana style ya Kenyatta..na kwao Kenyatta hakosei..ila sasa Magu akifanya hata moja tu la Kenyatta ndo utaijua kelele ya Chadema.

Hawajalaani mauaji na mateso ya watu kibao huko Kisumu wakati wa uchaguzi, hawajalaani mauaji ya risasi ya waandamanaji watano waliokuwa wakimpokea raila airport, hawajalaani hata kidogo kiongozi mkubwa wa upinzani kunyanyaswa na kufutwa uraia wake wa kuzaliwa, hawajalaani mpendwa wao kukaidi amri za mahakama wazi wazi katika kesi ya Miguna..

Hapa ndio huwa nawashidwa hawa 'makamanda'.
 
Siasa ni biashara chafu, ukweli hugeuzwa uongo na uongo hugeuzwa ukweli kwa maslahi ya kisiasa.
Mara nyingine huwa najiona mjinga sana kushabikia biashara hizi chafu za watu.
Kwa kweli..
Wanasiasa ni watu hatari.
Wengi ni waongo, vigeugeu sana.
 
Reactions: Oii
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…