Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
- Thread starter
- #21
Wewe ndiye unajipendekeza kwetu!!
Kwenu wapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ndiye unajipendekeza kwetu!!
TULIA WEWE NYANI WA TRUMPKwenu wapi?
Nimeona waliberia wameanza kutimuliwa nyie kina Mange mtapona kweli?!!!Yanayoendelea huko Kenya kuhusu suala la uraia wa Miguna Miguna yanasikitisha.
Lakini mwisho wa siku naamini Miguna atawabwaga tu mahakamani.
Na yote haya yamemfika kwa sababu tu alianza kumkosoa sana Uhuru Kenyatta.
Nakumbuka kwenye ule uchaguzi wa 2013 alivyokuwa anapendwa na watu wa Jubilee kwa sababu alikuwa akimnanga Odinga.
Alialikwa hadi kwenye hafla ya kusherehekea uapisho wa Kenyata.
Muda wote huu, hata kipindi akiwa mshauri wa Raila Odinga kipindi ni waziri mkuu, suala la uraia wake halikuwa na utata!
Kagombea mpaka ugavana wa Nairobi na uraia wake ulithibitishwa na tume yao ya uchaguzi.
Hata kitambulisho cha uraia wa Kenya anacho. Achilia mbali kuwa kazaliwa Kenya.
Sasa ghafla baada ya kuanza kumkosoa sana Uhuru eti ndo suala la uraia wake limeibuka.
Sasa huyu Miguna huwa namfananisha na Tundu Lisu kwa umachachari wao wa kuweza kuongea bila hofu.
Kwa mtaji huo, naamini kuwa kama Lisu angekuwa ni mzaliwa wa mikoa iliyo mipakani mwa Tanzania na nchi inayopakana nazo, kudhani au kuhisi kuwa uraia wake ungekuwa ushahojiwa si jambo la ajabu.
Baadhi ya kesi alizofunguliwa Lisu zinachekesha mno kiasi cha kuweza kumfanya mtu adhanie kuwa hao waliotoa maagizo ya yeye kukamatwa na kufunguliwa kesi ni wanafanya hivyo ili kumsumbua tu na si kwa nia ya kwamba wanamfungulia kesi ili hatimaye wampate na makosa na wamfunge jela.
Nadhani huwa wanajua kabisa kuwa kesi zao hazina mashiko.
Hata kwa Miguna Miguna nako ni vivyo hivyo tu.
Watawala wengi wa Afrika wanafanana kwa mengi. Hawapendi kukosolewa na hawana uvumilivu mwingi wa watu wanaotofautiana nao kimtazamo.
Na hulka hii haijalishi kama mtu yupo upinzani au la. Ni kwamba, mtu huyo akishapata madaraka na mamlaka makubwa anabadilika na kutaka kuwa mungu mtu!
Tuna safari ndefu sana na sidhani kama hata njia ya kutufikisha huko twaijua.
Haka hata elimu hakana,, kanashikaga mikuyati ya vizee vya Kimarekani wakati kanaviogesha!!Nimeona waliberia wameanza kutimuliwa nyie kina Mange mtapona kweli?!!!
Mkuu haijalishi unaogopa ama jasiri mwisho wa siku utaumizwa na maamuzi ya hii serikali.....Boss idawa Hauogopi Watu Wasiojulikana???!!! Haujui kukosoa ni Kosa la Jinai???!!! Umeongea vizuri na ukweli. Boss Mkuu alianza vizuri sana. Ila sasa sijui kalewa sifa au wanaomshauri na kujishauri wanamdanganya na kujidanganya.
Amesoma,Leseni yake ni Kubwa....Nawe wajipendekeza kwangu?
Africa ingefaa itawaliwe tena?Yanayoendelea huko Kenya kuhusu suala la uraia wa Miguna Miguna yanasikitisha.
Lakini mwisho wa siku naamini Miguna atawabwaga tu mahakamani.
Na yote haya yamemfika kwa sababu tu alianza kumkosoa sana Uhuru Kenyatta.
Nakumbuka kwenye ule uchaguzi wa 2013 alivyokuwa anapendwa na watu wa Jubilee kwa sababu alikuwa akimnanga Odinga.
Alialikwa hadi kwenye hafla ya kusherehekea uapisho wa Kenyata.
Muda wote huu, hata kipindi akiwa mshauri wa Raila Odinga kipindi ni waziri mkuu, suala la uraia wake halikuwa na utata!
Kagombea mpaka ugavana wa Nairobi na uraia wake ulithibitishwa na tume yao ya uchaguzi.
Hata kitambulisho cha uraia wa Kenya anacho. Achilia mbali kuwa kazaliwa Kenya.
Sasa ghafla baada ya kuanza kumkosoa sana Uhuru eti ndo suala la uraia wake limeibuka.
Sasa huyu Miguna huwa namfananisha na Tundu Lisu kwa umachachari wao wa kuweza kuongea bila hofu.
Kwa mtaji huo, naamini kuwa kama Lisu angekuwa ni mzaliwa wa mikoa iliyo mipakani mwa Tanzania na nchi inayopakana nazo, kudhani au kuhisi kuwa uraia wake ungekuwa ushahojiwa si jambo la ajabu.
Baadhi ya kesi alizofunguliwa Lisu zinachekesha mno kiasi cha kuweza kumfanya mtu adhanie kuwa hao waliotoa maagizo ya yeye kukamatwa na kufunguliwa kesi ni wanafanya hivyo ili kumsumbua tu na si kwa nia ya kwamba wanamfungulia kesi ili hatimaye wampate na makosa na wamfunge jela.
Nadhani huwa wanajua kabisa kuwa kesi zao hazina mashiko.
Hata kwa Miguna Miguna nako ni vivyo hivyo tu.
Watawala wengi wa Afrika wanafanana kwa mengi. Hawapendi kukosolewa na hawana uvumilivu mwingi wa watu wanaotofautiana nao kimtazamo.
Na hulka hii haijalishi kama mtu yupo upinzani au la. Ni kwamba, mtu huyo akishapata madaraka na mamlaka makubwa anabadilika na kutaka kuwa mungu mtu!
Tuna safari ndefu sana na sidhani kama hata njia ya kutufikisha huko twaijua.
Africa ingefaa itawaliwe tena?
Umeiweka vizuri mwanzo lakini kuna maeneo umepindisha na kucheza siasa badala kuzingatia ukweli ili hoja ijadiliwe ipasavyo, Miguna amekua akikosoa serikali na kuropokwa yote, kwanza kipindi alikua anagombea ugavana alitapika maneno ya kila aina, na akaachiwa bila ya kufuatwa. Tatizo limekuja pale alipitiliza kwa kumlisha kiapo cha urais Raila Odinga, hapo Jubilee walihisi kama ametoboa jicho, ikabidi wamkumbushie kale kadhambi kake ka kuukana uraia na kutafuta uraia wa nchi nyingine.
Kumbuka kipindi hicho Kenya hatukua na uraia pacha, ilikua kwamba ukiupata uraia wa nchi nyingine unapoteza wa Kenya. Kwa kifupi awamu ya Kibaki/Raila walifanya figisu na kuvunja shria na kumpa pasipoti ya Kenya bila ya kufuata taratibu za kisheria. Hiyo dhambi ameishi nayo na imekua ikifumbiwa macho hadi alipoichokonoa serikali kwenye macho.
Aliidhinishwaje na IEBC kugombea ugavana wa Nairobi 2017????
Narudia tena, serikali ya awamu ya awali ilitenda kosa kumpa pasipoti bila ya kufuata taratibu za kisheria, serikali ya sasa ikafumbia macho hako 'kadhambi', ikamuacha akaidhinishwa kugombea ugavana tena kwa mlengo wa upinzani huku akikosoa serikali balaa.
Sasa serikali ilizidiwa uzalendo au uvumilivu pale aliichokonoa hadi kwenye jicho kwa kutenda kosa la 'uhaini' la kumuapisha Raila. Ndio ikabidi kufukua mifupa yake.
Sasa mbona mpaka hivi sasa mahakamani anawabwaga hao watu wa serikali?
Na sheria ya uraia ya sasa inasemaje kuhusu Wakenya waliokuwa na uraia wa nchi nyingine kabla ya katiba ya sasa?
Nakwambia mahakamani Miguna atawagaragaza hao serikali.
Believe me [emoji16]
Sssssh usiseme sana.Na CHADEMA walitangaza kumuunga mkono Uhuru [emoji16][emoji16][emoji16]
Kwa kweli..Siasa ni biashara chafu, ukweli hugeuzwa uongo na uongo hugeuzwa ukweli kwa maslahi ya kisiasa.
Mara nyingine huwa najiona mjinga sana kushabikia biashara hizi chafu za watu.