Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mwanzo mwanzoni niseme wazi kuwa mimi si na sijawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA au chama kingine chochote cha siasa hapa Tanzania au kwingineko duniani. Hilo linatosha kutoa maoni yangu huru kuhusu siasa za nchi yangu kwakuwa nazifuatilia.
CHADEMA wanapaswa kufanya uchaguzi mkuu wa kichama kitaifa mwaka huu(kwa mujibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa wameshachelewa/ na wao CHADEMA wanadai waliusogeza uchaguzi wao mbele kwa kikao hadi Disemba mwaka huu.
Katika uchaguzi huo, nafasi mbalimbali zitagombewa. Lakini, nafasi ya juu kabisa ya kichama ni ya Mwenyekiti wa Taifa. Nafasi hii ni nyeti kwenye chama chochote-isipokuwa ACT Wazalendo yenye Kiongozi Mkuu wa Chama. Sababu ni kuwa Mwenyekiti ni nembo na kielelezo cha chama.
Mwenyekiti anapaswa kujaa busara, hekima, utulivu, ubunifu, uimara, ukali na upole ambavyo vitatumika kwa nyakati tofauti kulingana na matakwa yaliyo mezani. Si kila wakati huhitajika moja au lingine, hutegemea na mazingira. Mwenyekiti ndiye mtu wa mbele.
Chama ni itikadi na imani. Chama ni nidhamu na utii kwa sheria,taratibu na kanuni zinazokiongoza. Chama ni kukubali au kukataa vikaoni; kupongeza au kukosoa vikaoni. Mwenyekiti hapaswi kuwa mkurupukaji au mfuata upepo au mpendasifa.
Kwa maoni yangu, na kwa sifa nilizozianisha hapo juu, si Cecil Mwambe wa Ndanda wala John Heche wa Tarime wanaofaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa. Wanapaswa kuwa darasani kiuongozi kwa muda kidogo kabla ya kukabidhiwa chama hicho.
Mapendekezo yangu yangekuwa John John Mnyika wa Kibamba au Joseph Selasini wa Rombo. Lakini, Mbowe anapaswa kupumzika na kuketi benchi la washauri wa chama.